Tetesi: Rais Samia kubadilisha Baraza la Mawaziri hivi punde

Tetesi: Rais Samia kubadilisha Baraza la Mawaziri hivi punde

Alifisidi 1.5 trilion kutoka hazina; CAG Assad alipohoji akamfukuza kazi bila kufuata taratibu.
Hivi unajua kama Asad hakuondolewa mdaa wake uliisha hakuongezewa muda halafu hizo hela trillion 1.5 alizozifisadi Alifichia wapi? Au hizi stori za kuokoteza
 
Kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha upigaji mkubwa wa fedha za umma, Mh Rais Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajia kutengua uteuzi wa mawaziri ambao wizara wanazozisimamia zilionyesha upigaji mkubwa. Aidha, wakurugenzi ambao halmashauri zao zilipewa hati chafu nao watafyekelewa mbali na panga la Mh Rais. Na wale waliopata hati zisizoridhisha watahamishwa vituo vyao vya kazi ili kupewa nafasi ya mwisho kujirekebisha.

Kana kwamba hii haitoshi, inasemekana vigogo wote ambao walihusika moja kwa moja au kwa kushindwa kusimamia taasisi zao na kusababisha upotevu mkubwa wa fedha za umma, nao watasombwa na mafuriko haya na wengi wao watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria. Moto wa mama umewaka. Waliodhani anatania siku alipochukia na kuwatukana stupid, msidhani alikuwa anatania. Mbivu na mbichi lazima zijulikane. Hakuna hata mtu mmoja atakayechezea fedha za umma akabaki salama. Taarifa hizi zimepenyezwa na watu walio karibu na utawala.

MAONI YANGU
Namuunga mkono mama Dr Rais Samia kwa kuwachukulia hatua watendaji waloshindwa kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na kuwashughulikia mafisadi wote lakini nashauri jambo hili lifanyike kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha kwamba ni wale tu waliohusika na uzembe au ubadhirifu ndio wanachukuliwa hatua kali. Isitokee watu wasiohusika kuingizwa kwenye mkumbo. Utawala washeria sharti uchukue nafasi yake.

Nawasilisha.
Kuwahamisha wizara mafisadi hakusaidii kitu ni ulaghai.
 
Hii comment imeonyesha kiwango cha chini. Mwigulu au makamba wakitolewa kwenye uwaziri inasaidia nini? Kiwatoa kwenye uwaziri inahusianaa vipi na yeye kwenye uchaguzi wa 2025?

Unataka kusema kuna watu hawatampigia kura kwa kuwa mwigulu na makamba wapo? Pia unataka kusema tatizo la serikali ya sasa ni mwigulu na makamba?

Mimi nadhani hatujui tatizo letu kubwa ni lipi
Kwani tatizo la nchi hii ni nini na litatatulikaje mkuu?
 
Story za vijiweni

Mama hana haja kurithi ugomvi wa JPM na watu,Mama hana haja kurithi ugomvi wa JPM na baadhi ya watu

Mama atengeneze maadui wake mwenyewe,Msilazimishe kila adui wa JPM awe adui wa Samiah

Sent using Jamii Forums mobile app

Mahakama ndio inathibitisha wezi na siyo CAG

Watu mnafahamu maana ya Auditing?

Auditor hata malipo yakiwa halali ila tarehe ya malipo watu walisahau kuandika kwenye invoice ana ona kuna hatari ana ireport na kuandika kuna malipo hewa,Sasa typing error au kusahau ni mambo ya kawaida huko serikalini

Auditor hata muhuri ukikosekana kwenye document ya muhuri wa PAID ana report kuwa kuna issue? Sasa kusahu muhuri kugonga hata Bank wanasahau sembuse huko halmashauri ni kawaida watu kusahau kugonga mihuri

Ndio maana watu wanapewa muda kujibu hoja ,La sivyo utafunga wafanyakazi wote jela serikalini

Kuna maswali mengine aachiwe Internal auditor apambane nayo na siyo CAG

Tatizo kubwa hapa Tanzania ni elimu ...elimu...elimu

Watu wengi hawajui kazi ya ofisi ya CAG na hata maana ya report yake na mpaka kuna wabunge nao hawaelewi ,Elimu ni muhimu kuhusu Auditing na kazi ya CAG
Yaani zinapotea trillions of money wewe unasema watu walisahau kuandika tarehe?
Lazima utakuwa mjinga sana.
 
Naona waziri Ulega anaziara za vyombo vya Habari kujikomba kwa Wana chi kuomba huruma ya Wana nchi, ngoja tuone yajayo yanafurahisha
Mama anatoa mtu anaefanya kazi,anaweka akina ulega kwa sababu ya uswahili.

Kazi zao ni kumpost post mama na kusifu,wajanja wajanja tu
 
Mama anatoa mtu anaefanya kazi,anaweka akina ulega kwa sababu ya uswahili.

Kazi zao ni kumpost post mama na kusifu,wajanja wajanja tu
Ulega ni moja wa mawaziri ambao hawatarudi kwenye baraza; amefail sana
 
Kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha upigaji mkubwa wa fedha za umma, Mh Rais Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajia kutengua uteuzi wa mawaziri ambao wizara wanazozisimamia zilionyesha upigaji mkubwa. Aidha, wakurugenzi ambao halmashauri zao zilipewa hati chafu nao watafyekelewa mbali na panga la Mh Rais. Na wale waliopata hati zisizoridhisha watahamishwa vituo vyao vya kazi ili kupewa nafasi ya mwisho kujirekebisha.

Kana kwamba hii haitoshi, inasemekana vigogo wote ambao walihusika moja kwa moja au kwa kushindwa kusimamia taasisi zao na kusababisha upotevu mkubwa wa fedha za umma, nao watasombwa na mafuriko haya na wengi wao watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria. Moto wa mama umewaka. Waliodhani anatania siku alipochukia na kuwatukana stupid, msidhani alikuwa anatania. Mbivu na mbichi lazima zijulikane. Hakuna hata mtu mmoja atakayechezea fedha za umma akabaki salama. Taarifa hizi zimepenyezwa na watu walio karibu na utawala.

MAONI YANGU
Namuunga mkono mama Dr Rais Samia kwa kuwachukulia hatua watendaji waloshindwa kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na kuwashughulikia mafisadi wote lakini nashauri jambo hili lifanyike kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha kwamba ni wale tu waliohusika na uzembe au ubadhirifu ndio wanachukuliwa hatua kali. Isitokee watu wasiohusika kuingizwa kwenye mkumbo. Utawala washeria sharti uchukue nafasi yake.
Nawasilisha.
Kwa jinsi upigaji ulivyoshamiri katika nchi hii, hata kama watabadili baraza la mawaziri, ni kazi bure. Nchi hii imefika mahali pabaya sana kwenye suala zima la upigaji wa fedha za umma.
 
Back
Top Bottom