Tetesi: Rais Samia kubadilisha Baraza la Mawaziri hivi punde

Tetesi: Rais Samia kubadilisha Baraza la Mawaziri hivi punde

Story za vijiweni

Mama hana haja kurithi ugomvi wa JPM na watu,Mama hana haja kurithi ugomvi wa JPM na baadhi ya watu

Mama atengeneze maadui wake mwenyewe,Msilazimishe kila adui wa JPM awe adui wa Samiah

Sent using Jamii Forums mobile app

Mahakama ndio inathibitisha wezi na siyo CAG

Watu mnafahamu maana ya Auditing?

Auditor hata malipo yakiwa halali ila tarehe ya malipo watu walisahau kuandika kwenye invoice ana ona kuna hatari ana ireport na kuandika kuna malipo hewa,Sasa typing error au kusahau ni mambo ya kawaida huko serikalini

Auditor hata muhuri ukikosekana kwenye document ya muhuri wa PAID ana report kuwa kuna issue? Sasa kusahu muhuri kugonga hata Bank wanasahau sembuse huko halmashauri ni kawaida watu kusahau kugonga mihuri

Ndio maana watu wanapewa muda kujibu hoja ,La sivyo utafunga wafanyakazi wote jela serikalini

Kuna maswali mengine aachiwe Internal auditor apambane nayo na siyo CAG

Tatizo kubwa hapa Tanzania ni elimu ...elimu...elimu

Watu wengi hawajui kazi ya ofisi ya CAG na hata maana ya report yake na mpaka kuna wabunge nao hawaelewi ,Elimu ni muhimu kuhusu Auditing na kazi ya CAG
Acha kushauri ujinga. Wote waliotajwa wapigwe chini.
 
Anafanya rotation kwa watu wale wale halafu utegemee matokeo tofauti. Kwa namna hii hatuendi mahali
 
Mama Mh Rais Usiogope, Wananchi tupo na wewe. Hawa wevi wanaturudisha nyuma. Chukua hatua.
kazi iendelee
 
Kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha upigaji mkubwa wa fedha za umma, Mh Rais Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajia kutengua uteuzi wa mawaziri ambao wizara wanazozisimamia zilionyesha upigaji mkubwa. Aidha, wakurugenzi ambao halmashauri zao zilipewa hati chafu nao watafyekelewa mbali na panga la Mh Rais. Na wale waliopata hati zisizoridhisha watahamishwa vituo vyao vya kazi ili kupewa nafasi ya mwisho kujirekebisha.

Kana kwamba hii haitoshi, inasemekana vigogo wote ambao walihusika moja kwa moja au kwa kushindwa kusimamia taasisi zao na kusababisha upotevu mkubwa wa fedha za umma, nao watasombwa na mafuriko haya na wengi wao watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria. Moto wa mama umewaka. Waliodhani anatania siku alipochukia na kuwatukana stupid, msidhani alikuwa anatania. Mbivu na mbichi lazima zijulikane. Hakuna hata mtu mmoja atakayechezea fedha za umma akabaki salama. Taarifa hizi zimepenyezwa na watu walio karibu na utawala.

MAONI YANGU
Namuunga mkono mama Dr Rais Samia kwa kuwachukulia hatua watendaji waloshindwa kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na kuwashughulikia mafisadi wote lakini nashauri jambo hili lifanyike kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha kwamba ni wale tu waliohusika na uzembe au ubadhirifu ndio wanachukuliwa hatua kali. Isitokee watu wasiohusika kuingizwa kwenye mkumbo. Utawala washeria sharti uchukue nafasi yake.
Nawasilisha.
Taarifa yako haiwezi kuwa na ukweli ndani yake. Hii ripoti si ya jana wala juzi. Anayo muda mrefu uliopita. Hii ripoti ilikaliwa na spika hisijadiliwe kutokana na sababu anazozijuwa yeye.

Kama kuna mabadiliko ya baraza la mawaziri haitokani na hii ripoti iliyojadiliwa juzi, na akifanya hivyo kwasababu hiyo basi atakuwa.....
 
Back
Top Bottom