Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara nzito sana ya kikazi Nchini Korea ya Kusini. Ambapo huko anatarajiwa kufanya mazungumzo mazito sana na Rais wa nchi hiyo.

Ambapo ni katika ziara hiyo nzito Tanzania inatarajia kupata mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola za kimarekani Billion 2.5 kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Narudia kusisitiza hapa mkopo huo ni wa mashariti NAFUU na ambao utawekezwa katika miradi ya maendeleo.ikumbukwe kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini na mashariti ya mkopo yapoje .ndio maana nimesisitiza hapa kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu kabisa.

Lakini vilevile Rais wetu mpendwa atashiriki mkutano utakaowakutanisha viongozi wa nchi na serikali kati ya Korea na wale kutoka Afrika kuanzia Tarehe 4 June hadi Tarehe 6 June. Ambapo katika mkutano huo Rais wetu mpendwa atapata fursa ya kuhutubia mkutano huo na kushiriki mjadala mzito juu ya kuimarisha masuala ya usalama wa chakula na madini.

Mambo mengi na makubaliano mbalimbali yatashuhudiwa yakifanyika na kusainiwa katika ziara hiyo ya kihistoria kwa Rais wetu kipenzi kuanzia kilimo,madini ya kimkakati,masuala ya sanaa na utamaduni na mengine mengi sana. Ni ziara ambayo tunakwenda kupata na kufaidika na mambo mengi sana.

Lakini pia ziara hiyo itashuhudiwa na Dunia nzima Rais wetu mpendwa akipewa na kutunukiwa Udaktari wa Heshima,kwa kutambua mchango Chanya wa uongozi wake ulioleta mabadiliko chanya katika maeneo mbalimbali.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Asisahau kwenda na wasanii, wakatangaze muziki, wafanya biashara washaenda sana.
 
Kumbukeni tu kuwa huyu angekuwa mama wa nyumbani angekuwa anaenda vigodoro kila ijumaa. Starehe ndio jambo kuu la mtu wa mwambao.
 
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais.au unafikiri anakwenda kule kutalii tu? Hufahamu anakwenda kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa letu? Hufahami ni katika ziara hiyo kutasainiwa mikataba mbalimbali pamoja na makubaliano mengi katika masuala tofauti tofauti?
Acha ujinga, kwamba huko hakuna Balozi au Waziri wa Wizara husika?
 
Safari moja tu ya jirani yetu wa Kenya nchini USA, William Ruto imekuwa na tija kubwa kuliko safari zote zaidi ya 50 za Mama tangu achukue uongozi wa nchi. Tujifunze kwa jirani uzalendo wa ukweli si mambo ya kuchezea kodi za maskini na kwenda kupiga mnada nchi yako kwa faida ya familia yako na washirika wako wachache.
Huyu huwa anazunguka huku hajui hata anatafuta ni nini?
 
Duh!! Tulikuwa tunamkumbuka Magufuli nadhani sasa tutalazimika kumkumbuka hata Kikwete!
Labda mama wazazi wake walimwachia akafundishwa hesabu za kukopa huko shuleni 😁😁

downloadfile-3.jpg
 
Maendeleo gani anayapata mwananchi wa chini kutokana na huo mkopo?
Umesahau kuweka namba za simu kama wanavyofanya waimba sifa wenzako. Upumbavu mtupu.
 
Back
Top Bottom