Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Hivi kwanini kiongozi wa China Urusi au Marekani na hata Brazil hawana ziara nyingi hivi kama hawa wa huku kwetu?
Au ndio huwa wanakwenda kuomba?
Wapo busy na nchi zao kule hakuna utani na mali za umma ndiyo maana hakuna V8 kama huku na wakati nchi zao ndiyo zinatengeneza. Poor leader
 
JK party 2
Jamii ya pwani haifai kabisa kupewa mamlaka makubwa kuongoza nchi...wanapenda sana sherehe na kusafiri!.
Uongozi wa Sa100 na ule wa JK unashabihiana sana kwa mengi!.
Well basicaly jamii za watu wa pwani hawapendi shida, wavivu, watu wa starehe sana. Hawapendi challenge.
Althought kuwa few exeptions ambao wanweza uongozi but overall si kitu chao kabisa
 
Safari moja tu ya jirani yetu wa Kenya nchini USA, William Ruto imekuwa na tija kubwa kuliko safari zote zaidi ya 50 za Mama tangu achukue uongozi wa nchi. Tujifunze kwa jirani uzalendo wa ukweli si mambo ya kuchezea kodi za maskini na kwenda kupiga mnada nchi yako kwa faida ya familia yako na washirika wako wachache.
 
......nadhani ndo ziara hii alizungumza juzi kwamba ataambatana na baadhi ya wasanii wa filamu wakapate uzoefu mpya huko.....
 
Kazi pekee anaweza ni kusafiri, kuteua, kutengua na kuhamisha hakuna la maana anaweza
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais.au unafikiri anakwenda kule kutalii tu? Hufahamu anakwenda kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa letu? Hufahami ni katika ziara hiyo kutasainiwa mikataba mbalimbali pamoja na makubaliano mengi katika masuala tofauti tofauti?
 
Safari moja tu ya jirani yetu wa Kenya nchini USA, William Ruto imekuwa na tija kubwa kuliko safari zote zaidi ya 50 za Mama tangu achukue uongozi wa nchi. Tujifunze kwa jirani uzalendo wa ukweli si mambo ya kuchezea kodi za maskini na kwenda kupiga mnada nchi yako kwa faida ya familia yako na washirika wako wachache.
Acha unafiki wako wewe..kwani hujaona ziara aliyofanyaga china ilipelekea kusamehewa Deni la takribani Billion 31?

Unafahamu kuwa Rais wa kenya alikodi ndege binafsi ambayo wakenya wanalalamika kuwa imetumia gharama kubwa sana?

Acha ulimbukeni na ushamba ndugu yangu.
 
Well basicaly jamii za watu wa pwani hawapendi shida, wavivu, watu wa starehe sana. Hawapendi challenge.
Althought kuwa few exeptions ambao wanweza uongozi but overall si kitu chao kabisa
Acha mawazo ya kibaguzi na chuki kwa watu.dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu ambapo huwezi kuacha wala kukoma.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara nzito sana ya kikazi Nchini Korea ya Kusini. Ambapo huko anatarajiwa kufanya mazungumzo mazito sana na Rais wa nchi hiyo.

Ambapo ni katika ziara hiyo nzito Tanzania inatarajia kupata mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola za kimarekani Billion 2.5 kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Narudia kusisitiza hapa mkopo huo ni wa mashariti NAFUU na ambao utawekezwa katika miradi ya maendeleo.ikumbukwe kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini na mashariti ya mkopo yapoje .ndio maana nimesisitiza hapa kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu kabisa.

Lakini vilevile Rais wetu mpendwa atashiriki mkutano utakaowakutanisha viongozi wa nchi na serikali kati ya Korea na wale kutoka Afrika kuanzia Tarehe 4 June hadi Tarehe 6 June. Ambapo katika mkutano huo Rais wetu mpendwa atapata fursa ya kuhutubia mkutano huo na kushiriki mjadala mzito juu ya kuimarisha masuala ya usalama wa chakula na madini.

Mambo mengi na makubaliano mbalimbali yatashuhudiwa yakifanyika na kusainiwa katika ziara hiyo ya kihistoria kwa Rais wetu kipenzi kuanzia kilimo,madini ya kimkakati,masuala ya sanaa na utamaduni na mengine mengi sana. Ni ziara ambayo tunakwenda kupata na kufaidika na mambo mengi sana.

Lakini pia ziara hiyo itashuhudiwa na Dunia nzima Rais wetu mpendwa akipewa na kutunukiwa Udaktari wa Heshima,kwa kutambua mchango Chanya wa uongozi wake ulioleta mabadiliko chanya katika maeneo mbalimbali.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Mama atuongoze maisha yake yote mpaka kifo kitutenganishe... Hakuna na hakuwahi na hatotokea kama yeye.. Sasa nchi inakwenda kufaidika na MIKOPO ya Bei nafuu....
Bravo Sana!!!!
 
Acha unafiki wako wewe.kwani sisi ziara za Mheshimiwa Rais mara ngaoia tumeona taifa zake.kwani hujaona ziara aliyofanyaga chini ilipelekea kusamehewa Deni la takribani Billion 31?

Unafahamu kuwa Rais wa kenya alikodi ndege binafsi ambayo wakenya wanalalamika kuwa imetumia gharama kubwa sana?

Acha ulimbukeni na ushamba ndugu yangu.
Punguza munkari na presha tulia andika vizuri ulipokea basi edit, mbona umepaniki???

Nani hajui mama anaupiga mwingi???
 
Nilishangaa sana juzi kwenda ziara kwa Harmonise huku wafanyakazi wake akiwakimbia mei mosi
Nani kakwambia kuwa aliwakimbia? Hufahamu kuwa alikuwa nje ya Nchi? Hata kama pia angekuwepo na kwenda vipi kama hana dhamira ya kuwaongezea mishahara,kuwapandisha madaraja na kuboresha maslahi yao kwa ujumla? Si angekwenda tu na kuzungumza na kuondoka? Lakini watumishi wa umma wana imani kubwa sana na uongozi na serikali ya Mheshimiwa Rais kwa kuwa wanatambua namna anavyowajali na kuwapenda.kwa sababu wanafahamu ya kuwa ni wakati wake ndio wamepata kupandishwa madaraja,kulipwa stahiki zao,kupewa nyongeza ya mshahara ya kila mwaka,kulipwa malimbikizo ya madeni yao n.k.
 
Back
Top Bottom