Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini Korea Kusini kuanzia Mei 31 - Juni 6

Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara nzito sana ya kikazi Nchini Korea ya Kusini. Ambapo huko anatarajiwa kufanya mazungumzo mazito sana na Rais wa nchi hiyo.

Ambapo ni katika ziara hiyo nzito Tanzania inatarajia kupata mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola za kimarekani Billion 2.5 kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Narudia kusisitiza hapa mkopo huo ni wa mashariti NAFUU na ambao utawekezwa katika miradi ya maendeleo.ikumbukwe kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini na mashariti ya mkopo yapoje .ndio maana nimesisitiza hapa kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu kabisa.

Lakini vilevile Rais wetu mpendwa atashiriki mkutano utakaowakutanisha viongozi wa nchi na serikali kati ya Korea na wale kutoka Afrika kuanzia Tarehe 4 June hadi Tarehe 6 June. Ambapo katika mkutano huo Rais wetu mpendwa atapata fursa ya kuhutubia mkutano huo na kushiriki mjadala mzito juu ya kuimarisha masuala ya usalama wa chakula na madini.

Mambo mengi na makubaliano mbalimbali yatashuhudiwa yakifanyika na kusainiwa katika ziara hiyo ya kihistoria kwa Rais wetu kipenzi kuanzia kilimo,madini ya kimkakati,masuala ya sanaa na utamaduni na mengine mengi sana. Ni ziara ambayo tunakwenda kupata na kufaidika na mambo mengi sana.

Lakini pia ziara hiyo itashuhudiwa na Dunia nzima Rais wetu mpendwa akipewa na kutunukiwa Udaktari wa Heshima,kwa kutambua mchango Chanya wa uongozi wake ulioleta mabadiliko chanya katika maeneo mbalimbali.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Vipi ndo tunaendelea "kububujikwa na machozi",au machozi siku hizi yamekwisha 😂
 
Acha unafiki wako wewe..kwani hujaona ziara aliyofanyaga china ilipelekea kusamehewa Deni la takribani Billion 31?

Unafahamu kuwa Rais wa kenya alikodi ndege binafsi ambayo wakenya wanalalamika kuwa imetumia gharama kubwa sana?

Acha ulimbukeni na ushamba ndugu yangu.
Billioni 31 za dollar au madafu? Kama madafu si kitu cha kujivunia. Wananchi wa Kenya walilalamika lakini ufafanuzi umetolewa. Mama yako anaweza kukupa gharama kiasi gani ameshafuja tangu aanze kwenda safari zisizo na tija? Akirudi ataenda kuzindua album ya nani? Zuchu?
 
Rais wetu anatumia gharama ndogo sana katika ziara zake na ndio maana husikika malalamiko ya gharama kama ambavyo ilitokea kenya. Ni wapi uliona Rais wetu akikodi ndege binafsi kwenda nje ya Nchi?
 
Tumebubujikwa na machozi ya furaha kuona Jemedari wetu hajasahau watu wa tasnia Rai yangu aziwasahau Bambu na Kingwendu au Mtango
 
Tunamtakia Kila la heri Rais Samia kwenye ziara hiyo ya mdau Wetu muhimu wa Maendeleo Korea Kusini.

Ikiwezeoana Awapatanishe Kim wa North Korea na South Korea.

View: https://www.instagram.com/p/C7jGpWPKRht/?igsh=MTJwY21qY29keXlxYQ==

Mwanadiplomasia namba 1 na Bingwa wa Biashara na Uchumi 👇👇

View: https://twitter.com/mfa_tanzania/status/1795450881489387676?t=uQx9AM40cFkizIrgBgoIeg&s=19

View: https://twitter.com/mamayukokazini/status/1795696625605640647?t=135X6E_LYITs49bY3-05Aw&s=19

ZIARA NZITOYA KIKAZI KWA MUDA WA WIKI MOJA🤣🤣

Bonge la Movie la Kikorea litegemewe muda wowote hapo.
 
Rais wetu anatumia gharama ndogo sana katika ziara zake na ndio maana husikika malalamiko ya gharama kama ambavyo ilitokea kenya. Ni wapi uliona Rais wetu akikodi ndege binafsi kwenda nje ya Nchi?
Gharama ndogo ndiyo kiasi gani? Unazo gharama za kila safari aliyokwenda uweke hapa?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Taarifa inayoendelea kusambaa Duniani kwote na kugonga vichwa vya habari ,ni kuwa Rais wetu na Jemadari Wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan anatarajia kufanya ziara nzito sana ya kikazi Nchini Korea ya Kusini. Ambapo huko anatarajiwa kufanya mazungumzo mazito sana na Rais wa nchi hiyo.

Ambapo ni katika ziara hiyo nzito Tanzania inatarajia kupata mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Dola za kimarekani Billion 2.5 kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Narudia kusisitiza hapa mkopo huo ni wa mashariti NAFUU na ambao utawekezwa katika miradi ya maendeleo.ikumbukwe kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini na mashariti ya mkopo yapoje .ndio maana nimesisitiza hapa kuwa mkopo huo ni wa masharti nafuu kabisa.

Lakini vilevile Rais wetu mpendwa atashiriki mkutano utakaowakutanisha viongozi wa nchi na serikali kati ya Korea na wale kutoka Afrika kuanzia Tarehe 4 June hadi Tarehe 6 June. Ambapo katika mkutano huo Rais wetu mpendwa atapata fursa ya kuhutubia mkutano huo na kushiriki mjadala mzito juu ya kuimarisha masuala ya usalama wa chakula na madini.

Mambo mengi na makubaliano mbalimbali yatashuhudiwa yakifanyika na kusainiwa katika ziara hiyo ya kihistoria kwa Rais wetu kipenzi kuanzia kilimo,madini ya kimkakati,masuala ya sanaa na utamaduni na mengine mengi sana. Ni ziara ambayo tunakwenda kupata na kufaidika na mambo mengi sana.

Lakini pia ziara hiyo itashuhudiwa na Dunia nzima Rais wetu mpendwa akipewa na kutunukiwa Udaktari wa Heshima,kwa kutambua mchango Chanya wa uongozi wake ulioleta mabadiliko chanya katika maeneo mbalimbali.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Korea Kusini ni mabingwa wa elimu ya vitendo,Raisi Samia aangalie hilo ili kuongeza ubunifu na elimu ya kujitegemea kwa kizazi kipya.
 
Back
Top Bottom