Rais Samia Kufanya Ziara ya Siku Tatu Nchini Angola na Kuhutubia Bunge la Nchi Hiyo

Rais Samia Kufanya Ziara ya Siku Tatu Nchini Angola na Kuhutubia Bunge la Nchi Hiyo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
40,476
Reaction score
26,173
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.Mama wa shoka , chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya Matumaini anatarajiwa kufanya ziara Nchini Angola.

Ambapo pia atapata nafasi na heshima kubwa ya kuhutubia Bunge la Nchi Hiyo Kwa Mwaliko maalumu wa Speaker wa Bunge hilo. Ambapo taarifa zinaonyesha kuwa hotuba yake inasubiriwa kwa kiu na hamu kubwa sana na waafrika mbalimbali Barani Afrika.

Hasa kwa kuzingatia uwezo wake mzuri wa kuhutubia na kujenga hoja .ikumbukwe hotuba za Rais Samia ndizo zimekuwa zikitoa Muelekeo ,mstakabari na Dira ya Afrika nzima na misimamo ya masuala mbalimbali.

Ikumbukwe ya kuwa ni Majuzi juzi tu hapa ambapo Rais wetu Mpendwa alipata mualiko na heshima kubwa ya kuhudhuria Uapisho wa Rais wa Namibia na kutoa hotuba yake iliyoteka Bara zima la Afrika pamoja na kupongezwa na watu mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika.

Hivyo Ziara hii na nafasi ya Rais wetu kupewa nafasi na heshima ya kuhutubia Bunge hilo ni Muendelezo wa Bara la Afrika kuendelea kutambua mchango wa Rais Samia katika maendeleo na ustawi wa Afrika na waafrika. Kutokana na mawazo na mtazamo wake chanya katika kuwakwamua waafrika na kuwaondoa katika lindi la Umaskini pamoja na kuondokana na utegemezi kwa nchi za ulaya na Magharibi.​

Screenshot_20250406-153615_1.jpg
Screenshot_20250406-153622_1.jpg
 
No reform, no election.
Uchaguzi utafanyika na CCM itashinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima. Ninyi endeleeni kuvurugana na kuraruana huko wakati CCM ikiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania na kufanya maandalizi mazito mazito. Mkimaliza kutoboa mtumbwi wenu na kuzama mtakuta tupo kwenye sherehe za Uapisho wa Rais wetu Mpendwa na kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan
 
NIMEONA MLETA MADA NI HUYO MASHIMBA NIKASHANGAA NIMEPAPITA KAMA UPEPO
 
Ndaga Lucas Mwashambwa, nisogezee Jina la kijana wangu, he is a teacher ajira ndo hamna
Awe mtulivu na mwenye subira maana hakuna atakayebakia Mtaani pasipo ajira wakati huu wa uongozi wa Mama yetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Shule zinaendelea kujengwa na hivyo walimu wataendelea kuhitajika na serikali itaendelea kutoa ajira za waalimu kwa kadri bajeti na uchumi utakavyo ruhusu. Ni katika hali hiyo ambapo kijana wako naye ataweza kuingia katika utumishi wa umma .
 
Usinipake mafuta kwa mgongo wa chupa.

But NAWATAKIA kila la heri huko safarini
 
🤣🤣🤣Angola Kuna mkono wa Urusi na Uchina, ndio Sababu Upinzani walizuiwa .
 
TOKA MAKTABA:

13 March 2025
Luanda Angola

Viongozi wa Vyama rafiki vya UNITA wazuiwa uwanja wa ndege nchini Angola
exemplo.

1741888788245.jpeg

Photo : Tundu Lissu líder do partido Chadema

13 March 2025
Luanda, Angola

LIVE AIRPORT : WAJUMBE WA MKUTANO WA IDC WAONDOKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA FEBRUARI 4 LUANDA ANGOLA

Tundu Lissu akielekea Intercontinental Hotel Luanda Angola usiku huu, :

View: https://m.youtube.com/watch?v=hwTMxBWaiHo

Tundu Lissu ashangaa maafisa uhamiaji walipodai hapo awali kuwa wamrundika rumande, kusubiri kuondoshwa nchini Angola kabla ya kupandishwa ndege

View: https://m.youtube.com/watch?v=H8EKTS6Rek8

Walioshikiliwa hapo awali Airport kwa masaa 8 ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar mheshimiwa Othman Masoud Othman, Tundu Lissu, Dorothy Semu, balozi HE Lieutenant General Matthew Edward Mkingule, Zitto Kabwe ...wote kutoka Tanzania...
16 March 2025

Makamu wa Rais Othman OMO Amshangaa Wasira Kupotosha Yaliyotokea Angola, Asema Ameipaka Matope Serikali​

View: https://m.youtube.com/watch?v=h6ZZfMC_gCg
 
Usinipake mafuta kwa mgongo wa chupa.

But NAWATAKIA kila la heri huko safarini
Uwe na imani na serikali ya Rais Samia .ambayo inaendelea kufanya kazi usiku na mchana kugusa Maisha ya watanzania na kuleta tabasamu na matumaini kwa wote. Hakuna Atakayeachwa nyuma katika uongozi wa Mama.

Rais wetu Mpendwa anadhamira ya kujenga uchumi unaogusa Maisha ya watu na kadri uchumi unavyokua na kuimarika Ndivyo Maisha ya watu yanavyobadilika na kuwa bora na mazuri zaidi.
 
Uchaguzi utafanyika na CCM itashinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima. Ninyi endeleeni kuvurugana na kuraruana huko wakati CCM ikiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania na kufanya maandalizi mazito mazito. Mkimaliza kutoboa mtumbwi wenu na kuzama mtakuta tupo kwenye sherehe za Uapisho wa Rais wetu Mpendwa na kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan
No reform, no election.
 
Kweli kabisa Africa nzima kiongozi?Usisahau pia vyombo vya habari vya kimataifa kama CNN,BBC,Aljazeera,FOX watakuwa live kwenye hili tukio la kidunia.

HOVYO KABISA
 
Kweli kabisa Africa nzima kiongozi?Usisahau pia vyombo vya habari vya kimataifa kama CNN,BBC,Aljazeera,FOX watakuwa live kwenye hili tukio la kidunia.

HOVYO KABISA
Vyombo mbalimbali vya habari vya Kimataifa vimeweka Kambi kusubiri ujio wa Rais Samia Nchini Angola.
 
  • Kicheko
Reactions: IIS
Back
Top Bottom