Rais Samia kuijengea Nyumba familia ya mtoto anaeuza ndizi

Rais Samia kuijengea Nyumba familia ya mtoto anaeuza ndizi

Mwanzoni kabisa nilifikiri raisi samia ni mtu makini kumbe ni mtu wa hovyo na asiyeelewa hata anafanya nn pale ikulu
Tanzania ina jumla ya watoto 2m wanaoishi katika mazingira hatarishi (Ovcs) yatima unamjengeaje nyumba mmoja tu? Kisa kaibuliwa/ kapangwa ili makonda apige nae picha?
Na wale wanaolala nje kariaakoo je?
Ccm kuweni serious kidogo bhana
Siasa hizi za mkate ni za kipumbavi sana
Mnawafanya watzania ni mazuzu kiasi hichi?
Mkuu haya unayoyaona katika nchi hii ndo uhalisia wa Watanzania wengi walivyo ni mazuzu.
 
Mkuu haya unayoyaona katika nchi hii ndo uhalisia wa Watanzania wengi walivyo ni mazuzu.
Kabisa aisee. Yule aliyeenda kuomba msamaha leo anatengenezewa mazingira ya uteuzi ni sula muda tu. Yaani pamoja na tuhuma zote zile ila atarudishwa tena kama bashite tu
 
Ikiwa ni siku moja tangu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda kupokea changamoto ya kijana Alhaji Yahya Abdallah ambaye anafanya biashara ya kuuza ndizi kumsaidia Mama yake na wadogo zake 4 na Mwenezi Makonda kwa niaba ya CCM kumuahidi kumsomesha na Kumpatia kiasi cha Fedha kwaajili ya vitendea kazi na sare za shuleni.

Leo 4 Februari, 2024 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha kuguswa zaidi na jambo hilo na kumsaidia Mwanamama huyo mjane kwa kumpatia kiwanja na kumjenga Nyumba kubwa ya kuishi na watoto wake wote ambapo ujenzi wa nyumba hiyo utaanza Ijumaa tarehe 9 Februari, 2024.

Pia, Dkt. Samia kuwasomesha Watoto wote 5 wa Mwanamama huyo pamoja na kughariamiwa vifaa vyote vya shule na sare.

Aidha, Dkt. Samia amempatia Mwanamama huyo Kiasi cha Tsh Milioni 5 itakayokuwa inatolewa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigoma Mjini kwaajili ya kufanya shughuli zake za biashara kujikwamua kiuchumi.

Credit - Bongo5
Sijaelewa kabisa mpendwa wetu anatupa ujumbe gani hapa.
 
WASOMI WAKISHAANZA KUUKOSOA UTAWALA NI HATARI KUBWA:-

Na:
Thadei Ole Mushi.
Kada wa CCM.

Wasomi Nguli nchini wameendelea kuongea, wameendelea kukosoa Mkataba wa Bandari, Ukiona wasomi kaliba ya kina Shivji wameanza kutoka Vyumbani mwao na kuja kufanya Press fahamu kuwa wakati umefika wa aidha ukubali kubadilika au ubadilishwe kwa Nguvu.

Ipo hivi

Serikalibyoyote dalili zake za kuobdoka madarakani kwa kutokuchaguliwa kwa Kura au kwa kupinduliwa hupitia vipindi viwili muhimu:-

Normal- Ni hatua ya kwanza ni kuona mambo yapo sawa wakati hayapo sawa. Pamoja na Kelele za wananchi watawala hujiona wapo tu sawa. Mfalme Luise wa XVI na mkewe Marine Antoniete pamoja na kelele za Wafaransa kulalamika maisha magumu na kupinga hali ya matabaka (Nobles na Clerks) ambao walikuwa wakila na kisaza na mfalme, Louise aliwapuuza.

Criticism- Hii ni hatua ya pili ambayo huusisha intelectuals kama hawa kina Shivji na wengineo kuanza kupinga aidha kwa kuandika au kwa kusema waziwazi. Kipindi hiki wasomi huamua kuanika uovu
Haya maneno yataishi
 
Ikiwa ni siku moja tangu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda kupokea changamoto ya kijana Alhaji Yahya Abdallah ambaye anafanya biashara ya kuuza ndizi kumsaidia Mama yake na wadogo zake 4 na Mwenezi Makonda kwa niaba ya CCM kumuahidi kumsomesha na Kumpatia kiasi cha Fedha kwaajili ya vitendea kazi na sare za shuleni.

Leo 4 Februari, 2024 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha kuguswa zaidi na jambo hilo na kumsaidia Mwanamama huyo mjane kwa kumpatia kiwanja na kumjenga Nyumba kubwa ya kuishi na watoto wake wote ambapo ujenzi wa nyumba hiyo utaanza Ijumaa tarehe 9 Februari, 2024.

Pia, Dkt. Samia kuwasomesha Watoto wote 5 wa Mwanamama huyo pamoja na kughariamiwa vifaa vyote vya shule na sare.

Aidha, Dkt. Samia amempatia Mwanamama huyo Kiasi cha Tsh Milioni 5 itakayokuwa inatolewa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigoma Mjini kwaajili ya kufanya shughuli zake za biashara kujikwamua kiuchumi.

Credit - Bongo5
Asiishie hapo tu wapo wengi mno wa namna hiyo, atasaidia wangapi ??

Bora aboreshe uchumi kila mtu anufaike na uchumi imara.
 
Chawa, Kunguni Toka Lumumba Hawajaiona Thread Hii Kuja Kumsifia SSH
 
Cheap politics kuelekea 2025, afanye hivyo kwa watoto wote wanaouza ndizi tena kwa mshahara wake binafsi siyo kwa bajeti fulani iliyotengwa serikalini kwa ajili ya mambo kama hayo

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Samia kazi ya urais imemshinda anatafuta cheap popularity kwasababu hicho ni ki alhaji.
Tumpongeze jamani

Hili si suala dogo...

Vuta picha huyo mama aliyesaidiwa akiona comment yako atajisikiaje...

Kikubwa hii inadhihirisha mh Samia anaona shida za watu na kuchukua hatua.
 
Hakuwahi kuandaliwa ,kujiandaa au kuota kuwa rais kujiamini kudogo .makonda anajua kucheza na victims mind si kwa yatima na wajane hata mama samia is a victim too
 
Back
Top Bottom