Rais Samia kuingia na mlinzi wa kiume msikitini, ni jambo la kawaida. Tuache Mihemko isiyo na Tija

Rais Samia kuingia na mlinzi wa kiume msikitini, ni jambo la kawaida. Tuache Mihemko isiyo na Tija

Wenye makosa ni hao walioshindwa kumwandaa huyo mwanaume ili afanane kike

Na hata hivyo hakutakiwa awe mmoja, wengekuwa hata wanne wote wamepiga mavazi ya kuziba Uso.
 
Hivi wakati mtume anatoa hayo maelekezo binadamu tulikuwa tulishaanza kuvaa nguo?
Ndiyo, wakati Mtume Muhammad (SAW) anatoa maelekezo hayo, binadamu walikuwa tayari wameanza kuvaa nguo. utamaduni wa kuvaa nguo ulikuwa umekuwepo kwa maelfu ya miaka kabla ya wakati wa Mtume Muhammad (SAW).


Historia inaonyesha kuwa kuvaa nguo ni desturi ya zamani sana. Hata kabla ya wakati wa Nabii Adam (AS) katika hadithi za kidini, wanadamu walikuwa wakijifunika miili yao kwa njia mbalimbali kwa kutumia ngozi za wanyama, majani, na vifaa vingine vya asili.


Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha uchi wenu na nguo za pambo. Na nguo za ucha Mungu, hizo ni bora. Hayo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu ili wapate kukumbuka." (Quran 7:26)
 
Rais SSH kuingia na mlinzi wa kiume mskitini ni jambo la kawaida kutokana na sababu mbali mbali , hasa kama kuna tishio la usalama au kutokana na idadi kubwa ya watu wanaokusanyika kwa pamoja.

Tujiepushe na mihemko isiyo na tija na badala yake tufikirie suluhisho zinazojenga na kuheshimu maadili ya jamii husika na kuhakikisha usalama na utulivu wa Rais.

Katika Quran, hakuna aya inayosema moja kwa moja kuwa ni marufuku kwa mwanaume kuingia sehemu ya wanawake msikitini. hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W) pamoja na mila na desturi za Kiislamu. Kwa mfano, katika hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W), kuna maelekezo yanayohimiza heshima na mipaka baina ya wanaume na wanawake wakati wa ibada ili kuepusha fitna na kudumisha heshima.( kuepusha matamanio ya kimapenzi ndani ya ibada. )

Ibn 'Umar aliripoti kwamba Mtume Muhammad (S.A.W) alisema, "Usiwazuie wanawake wa Allah kwenda kwenye misikiti ya Allah" (Sahih Muslim, Kitabu 4, Hadithi 891). Hadithi hii inaonyesha kwamba wanawake wanaruhusiwa kwenda msikitini, lakini haina amri maalum kuhusu maeneo maalum ndani ya msikiti. Kwa hiyo, mpangilio wa ndani wa msikiti kuhusu maeneo ya wanawake na wanaume unaweza kutegemea mila, desturi, na mantiki za kiutawala za msikiti huo na siyo tamko la S. A. W.

Katika mazingira ambapo kuna haja ya kuwepo na walinzi wa kiume kwa sababu za kiusalama, ni kwamba tunahakikisha hatua hizi zinachukuliwa kwa njia inayoheshimu mipaka ya kijinsia na dini, kulinda usalama bila kuvuruga utulivu wa ibada.( na hiki ndo amefanya RAIS SSH wa JMT)

Mtazamo huu unategemea hadithi kama ile inayosimuliwa na Umm Atiyyah, ambaye alisema kwamba wanawake waliokuwa kwenye hedhi waliambiwa wakae mbali na mahali pa kusalia/swalia wakati wa sala za Eid (imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim)

Surah Al-Baqarah (2:222), "Wanakuuliza habari ya hedhi. Sema: Huu ni unajisi. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi, wala msiwakaribie mpaka watwahare.( Tusilaumu sana yawezekana mlinzi wa kike alikuwa kwenye Surah Al-Baqarah 2:222 ).

Pia soma: Mlinzi wa kiume wa Rais kuvaa juba (vazi la kike) na kuketi msikitini sehemu ya wanawake ni sawa?
Mkuu usijiropokee tu kama umekunywa pombe.
Uislam haujakataza mwanamke kwenda msikitini,ila misikiti ilitenga nafasi za wanaume na wanawake ili kuweka faragha na adabu baina ya jinsia hizo mbili.
Hairuhusiwi mwanamke na mwanaume kuchangamana sehemu moja katika ibada.
Hilo huwa linatokea wakati wa HIJJAH tu sana sana pale watu wanapozunguka kaabah.
Huyo askari hakupaswa kuingia sehemu ya wanawake ilhali yeye mwanaume.
Kwani hakukuwa na askari mwanamke!?
Je mwanamke angetaka kuweka nguo sawa ili ajistiri vizuri aanze kuswali si atakua kashamchungulia!??
HUYO ASKARI AMEKOSEA NA HUYO MAMA SAMIA NAONA AMESHINDWA KUJICHUNGA MPAKA SASA ANAVUKA MIPAKA YA DINI.
AJITIZAME ASIJE AKAKUFURU ZAIDI.
 
20240618_080522.jpg
 
Wamama wote hapo waliomzunguka Rais ama ni maafisa Usalama ama wanakonekshen na TISS kwa namna yyt.Sio rahisi mtu wa kawaida awe karibu hapo sasa nadhan mwanaume alikuwa hapo kuweka negative charge since all of them are positive.So area ikawa neutralized and calm😂😂

Mnaosema mwanaume hakutakiwa kuwa hapo mlitaka awe wap?Kwanza kapendeza ndan ya hijab nyeusi murua kabisa na yeye mwenyewe mweusi na amepiga na makeup yake😂😂😂😂😂😂
. 🤣🤣🤣🤣🤣, Na uso wake wa kung'aa Safi kabisa
 
Duu hii kali ya mwaka kwa hiyo mwana akapiga hijab aisee huu ni udhalilishaji wa dini 😂😂😂😂🙏🙏🙏🙏
Ni jambo la kawaida mkuu... Hata sheikh wa mskiti amesema ni jambo la kawaida kabisa . Hasa katika mbinu za security. 😎😎.
 
Back
Top Bottom