Rais Samia kuitetemesha kwa kishindoo Arusha Kesho

Rais Samia kuitetemesha kwa kishindoo Arusha Kesho

Itakuwa unashinda umejifungia chumbani kwako halafu unakuwa unaota ndoto zako za kitoto hapa. Rais Samia anakubalika Nchini ni haijapata kutokea katika Historia ya Taifa LetuView attachment 3080829View attachment 3080831View attachment 3080832View attachment 3080834.
Huyo mama yenu akienda kule Kanda ya Ziwa anapata wakati mgumu sana inabidi malori yakawasombe wanafunzi kutoka Maswa, Bariadi, Meatu, Magu kuwapeleka Kirumba kuujaza uwanja. Hilo hata yeye mwenyewe analijua kwamba Kanda ya Ziwa hakubaliki hata chembe.
 
Endelea kupiga porojo wakati mama akiendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge anakwenda kuitetemesha kwa kishindo kikuu jiji la Arusha.

Ambapo siku ya kesho Rais wetu Mpendwa anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa kikao kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma.

Ambapo leo hii baada ya kutoka Nchini kenya ametua kwa kishindo katika uwanja wa KIA na kupokelewa kwa mapokezi mazito na wakuu wawili wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.Ambapo katika Mapokezi hayo Alikuwepo pia Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda Kijana Jasiri kusini mwa jangwa la Sahara.

Ambaye alionekana kuwa mwenye tabasamu , unyenyekevu na mtulivu wakati wote wa mapokezi hayo ya Amiri Jeshi Mkuu wetu. ambaye ni miongoni mwa wanawake mia moja wenye ushawishi zaidi Duniani.lakini pia ndio kinara wa kupigania matumizi ya nishati safi na bora Duniani Kwote katika kumuepusha mwanamke na matumizi ya kuni na mkaa katika kupikia ,ambayo yamekuwa na athari kubwa sana kiafya na kimazingira.

Kwa hiyo tukae kwa kutulia tusubiri hotuba nzito na ya kusisimua itakayotolewa na Rais huyu Mwenye uhodari mkubwa wa kutoa hotuba kama ilivyo kwa akina Barack Obama au Michell Obama au Hillary Clinton wa Marekani. Rais huyu mwenye kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania anatua katika jiji la Arusha ikiwa ni siku chache tokea atoe maagizo mazito sana yaliyo itetemesha Arusha na kanda ya kaskazini.

baada ya kutoa maagizo yaliyomaliza mgomo na maandamano ya Wamasai na kuwaacha wakiwa wenye furaha na tabasamu huku wakiruka ruka juu kwa furaha na shangwe kumshukuru na kumpongeza Rais wetu mpendwa kwa usikivu wake,utu , uungwana na moyo wa upendo kwa watanzania wote.View attachment 3080817

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Watanzania wabubujikwa na machozi!
 
Itakuwa unashinda umejifungia chumbani kwako halafu unakuwa unaota ndoto zako za kitoto hapa. Rais Samia anakubalika Nchini ni haijapata kutokea katika Historia ya Taifa LetuView attachment 3080829View attachment 3080831View attachment 3080832View attachment 3080834.
We ndo utakua hufahamu unaone
Itakuwa unashinda umejifungia chumbani kwako halafu unakuwa unaota ndoto zako za kitoto hapa. Rais Samia anakubalika Nchini ni haijapata kutokea katika Historia ya Taifa LetuView attachment 3080829View attachment 3080831View attachment 3080832View attachment 3080834.
Sasa mbona picha zenyewe zinaonyesha ni watoto wadogo tu ndo wamejaa. Inafahamika wazi kua ccm wanapokua na jambo sehemu basi shule za maeneo hayo huagizwa kufungwa wakati huo na wanafunzi ote kutakiwa kwenda kwenye jambo la ccm.

Kama kweli mnaamini watu wanajaa kwenye mambo yenu kwa mahaba, basi fanyeni bila kujaza watu kwa mtindo huo. Tangazeni mtakuepo then acheni watu wahudhurie wenyewe. Tuone kama watakuja hata watu mia
 
Sisi makada anatupatia wakati mgumu sana kumpigia kampeni mwaka ujao. Yaani mambo yanabadilika kwa kasi sana, wananchi wamejaza vifua vyao na machungu mengi ya kupigika kimaisha, muda utaongea.
Napata picha ni kwa kiasi gani wasanii watajazwa kwenye kampeni za mwakani ili kuvutia watu, ili watengeneze picha ya kukubalika. Kwa sababu hiyo ndo njia pekee iliyobakia. Na wananchi kama watashtuka, mtakua na kazi sana
 
Wewe umeandika mtaani, ngoma nenda kutana na kuongea na wasaidizi wake wa chama chake na serikali ngazi ya chini kabisa huku mpaka ngazi ya juu kule anaokutana nao mara kwa mara, ndipo utajua hakubaliki kwa kiasi gan
Nilijua hakubaki ila sikujua kua hakubariki kwa kiasi hiki
 
Napata picha ni kwa kiasi gani wasanii watajazwa kwenye kampeni za mwakani ili kuvutia watu, ili watengeneze picha ya kukubalika. Kwa sababu hiyo ndo njia pekee iliyobakia. Na wananchi kama watashtuka, mtakua na kazi sana
Wasanii hawatakuwa na impact kubwa kama ilivyokuwa zamani. Itabidi tuwekeze zaidi kuhakikisha tunashinda uraisi (hilo ni lazima na litawezekana tu). Ila wabunge walio wengi itawabidi wapambane na hali zao tu, kwani wengi wao hawatorudi bila ya kuchafua uchaguzi kama 2020.
 
Uchaguzi ujao nina mashaka pia unaweza ukawa na uchafuzi sana kama wananchi hawatokua macho. Kitendo cha uchaguzi wa 2020 kuchafuliwa na maisha kuendelea kama kawaida kutawapa nguvu sana ccm kufanya kama kile wakitegemea hakutakua na kelele kudumu za kutishia usalama
 
Ngumu sana kujirudia kilichotokea 2020, wabunge wajiandae kufanya figisu kwa level zao. Sio kama ile ya 2020 iliyokuwa na backup kubwa sana ya aliyekuwa Mwenyekiti wetu. Tutakuwa na zile faulo za miaka yote ambazo majimbo mengi tu wananchi wanazimudu vyema kabisa.
 
Ngoja tuone. Japo saivi tactic yenu ya kuuvuruga upinzani itawabeba maana mpaka saivi hawaeleweki wanamsimamisha nani huku kukiwa na sintofahamu ndani yao, ni kama hakujatulia. Hilo linaweza likawapa ushindi rahisi kwenye kiti kikuu
 
28 Agosti 2024

Inaonekana anewasili kikazi zaidi hakuna msururu wa viongozi walioenda kupokea, pengine viongozi wapo field kuweka mambo sawa

1724831992964.png

Habari za kina rais Samia Hassan awasili uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akitokea Nairobi, Kenya. Na kuelekea Arusha ufunguzi wa Kikao Kazi cha Viongozi wa Taasisi za Umma

1724832239077.png
 
Ngoja tuone. Japo saivi tactic yenu ya kuuvuruga upinzani itawabeba maana mpaka saivi hawaeleweki wanamsimamisha nani huku kukiwa na sintofahamu ndani yao, ni kama hakujatulia. Hilo linaweza likawapa ushindi rahisi kwenye kiti kikuu
Tatizo sasa hivi kuna upinzani mkubwa toka kwa wananchi wenyewe ingawa hatuuoni waziwazi. Pia kuivuruga CDM itakuwa si rahisi kwani tumeshabugi mapema kwa TAL. Mch naye kawakacha CDM kwa timing mbovu, hajawaumiza hata kidogo. Kiujumla huo mkakati hautotusaidia, labda tucopy tulichokifanya 2020 na ambayo ni ngumu kwani M/kiti hana ngozi ngumu kama ya mtangulizi wake
 
28 Agosti 2024

Inaonekana anewasili kikazi zaidi hakuna msururu wa viongozi walioenda kupokea, pengine viongozi wapo field kuweka mambo sawa

View attachment 3081226
Habari za kina rais Samia Hassan awasili uwanja wa ndege wa Kilimanjaro akitokea Nairobi, Kenya. Na kuelekea Arusha ufunguzi wa Kikao Kazi cha Viongozi wa Taasisi za Umma

View attachment 3081246
28 Agosti 2024

🔴#LIVE: RAIS SAMIA AKIFUNGUA KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZA UMMA​

Arusha ufunguzi wa Kikao Kazi cha Viongozi wa Taasisi za Umma

View: https://m.youtube.com/watch?v=ECY4Z_EsUW8
 
Mwaka huu 2024 mheshimiwa rais Dr. Samia Hassan yupo katika kikao cha viongozi wa taasisi za Umma mjini Arusha.

TOKA MAKTABA:​

Agosti 21, 2023​

1724833265840.png

Picha maktaba: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Kikao Kazi Cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kaatika ukumbi wa AICC - Arusha tarehe 19 Agosti, 2023.

Katibu Mkuu Kiongozi asisitiza maboresho Taasisi, Mashirika ya Umma! Akataa watendaji wakuu kukwamisha maono ya Rais Samia! Asema mashirika kubeba uchumi wa nchi inawezekana​

Agosti 21, 2023
Katibu Mkuu Kiongozi asisitiza maboresho Taasisi, Mashirika ya Umma! Akataa watendaji wakuu kukwamisha maono ya Rais Samia! Asema mashirika kubeba uchumi wa nchi inawezekana

Na Mwandishi Maalumu
KATIBU Mkuu Kiongozi, Mhe.Balozi Dkt.Moses Kusiluka amesema, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ina matumaini makubwa na mashirika zikiwemo taasisi mbalimbali za umma katika kutoa huduma bora kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hayo ameyabainisha Agosti 21, 2023 jijini Arusha wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Agosti 19, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akifungua kikao hicho alisema, Serikali imewekeza fedha nyingi katika mashirika ya umma huku ikiwa haioni tija, hivyo Serikali inatarajia kufanya mabadiliko makubwa.

“Ndugu zangu ma-CEO (Maafisa Watendaji Wakuu), Wenyeviti wa Bodi hatutanii, tumeshatoa fedha nyingi sana, zinaingia kwenye drainage, hatuoni tija yake.

“Sasa ni kuwekeana vigezo, ni kuwekeana vipimo vya utekelezaji au utendaji, lakini kuwekea targets za kufanya faida, ukishindwa huna sababu ya maana, kufa na shirika lako,”alisisitiza Rais Dkt. Samia.

Mbali na hayo, Dkt. Kusiluka akifunga kikao hicho ambacho washiriki walijadiliana mambo mbalimbali kwa ustawi bora wa mashirika na taasisi hizo za umma alibainisha kuwa;
“Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo mbalimbali, niungane na wote kumshukuru Mheshimwa Rais kwa maono yake na utashi wake kwamba taasisi za umma na mashirika zinafanyiwa maboresho makubwa ili kuongeza tija.

“Niwaombe mkayasimamie maelekezo ya Mheshimiwa Rais ipasavyo. Kila mtu katika sehemu yake na nafasi yake kazi ya ofisi yangu ni kuhakikisha maelezo ya Mheshimiwa Rais yanatekelezeka kwa ukamilifu nimuahidi Mheshimiwa Rais nitafuatilia na kusimamia kwa karibu.”

Mheshimiwa Balozi Dkt.Kusiluka alifafanua kuwa, mashirika na taasisi za umma ni kiungo muhimu baina ya Serikali na wananchi, hivyo kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali unafanyika kupitia mashirika na taasisi za umma.

“Sote tunatambua kwamba,wananchi wanahitaji huduma bora, kwa sasa bado taasisi nyingi zinatoa huduma duni. Na ni wajibu wa taasisi zote na mashirika ya umma kutoa huduma bora kama vile umeme, afya, maji, elimu na pia ziwe na ubora na ufanisi mkubwa kwa ukamilifu na kwa wakati.

“Na pale inapotokea shida wananchi wanapaswa wafahamishwe shida hiyo na ishughulikiwe kwa haraka, tambueni huu ni wajibu wenu.”

Wakati huo huo, Mheshimiwa Balozi Dkt.Kusiluka amebainisha kuwa, Ofisi ya Msajili wa Hazina ina jukumu la kusimamia mashirika na taasisi za umma na Serikali kwa sasa hivi inafanyia maboresho taasisi hizo.

“Yapo mageuzi mengi sasa hivi Serikali inayasimamia kwenye Ofisi hii.Lengo ni ofisi hii kusimamia vizuri shughuli za taasisi na mashirika ya umma.
“Na Serikali kwa sasa ipo katika mchakato wa kutunga sheria mpya itakayompatia TR (Msajili wa Hazina) uwezo mkubwa wa kusimamia uwekezaji wa Serikali katika mashirika ya umma na taasisi za Serikali.

“Sote tuhakikishe tunashiriki kikamilifu katika mchakato wa utungaji wa sheria hii ili tuwe na sheria bora itakayotuletea tija.

“Natoa wito muipatie ushirikiano Ofisi ya Msajili wa Hazina hatutarajii mkaanza kuikosoa kama unakosoa unakosoa kwa sababu ya kujenga na kwa sababu inaanza inaweza kuwa na dosari moja au mbili.

“Lakini Serikali inakusudia kuwa na ofisi yenye nguvu na tija na wataalamu wa kutosha, pia imarisheni ushirikiano na wizara mama zenu yaani wizara za kisekta.

“Pia, viongozi wa wizara wasiwashinikize kuwalipia huduma ambazo hawastahili, zingatieni sheria na miongozo na kanuni za utendaji kazi serikalini.

“Na huo ndio msingi wa Mheshimiwa Rais pia Rais alielekeza bodi zitumie mamlaka yake kwa mujibu wa sheria zilizoanzisha taasisi husika katika kuziendesha taasisi hizo.

“Hata hivyo ningependa kuwakumbusha kuepuka matumizi mabaya ya madaraka mliyopewa ikiwemo upendeleo wa ajira za watumishi na maamuzi juu ya stahili za viongozi na watumishi. Tuwe makini huko nyuma hatukufanya vizuri juu ya hili.

“Mtakumbuka pia maelekezo ya Mheshimiwa Rais alielekeza mashirika na taasisi za umma zipitiwe upya kwa lengo la kuchukua hatua stahiki ikiwemo kuongezea mitaji baadhi ya taasisi na mashirika ya umma.
“Pia kuangalia baadhi ya mashirika na taasisi za umma zingine kuzifuta.Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji inaelekeza zoezi hili lifanyike haraka na kwa umakini mkubwa.

“Ndugu viongozi, kuna hoja ya kufanya rebranding ili kuongeza ufanisi na tija katika kutekeleza adhima hiyo haihitaji fedha, bali mabadiliko ya mtazamo na fikra kwa viongozi, hivyo ni matarajio kuona ubunifu mwingi kutoka miongoni mwenu,”alifafanua kwa kina Katibu Mkuu Kiongozi.

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi,Mheshimiwa Balozi Dkt.Kusiluka amebainisha kuwa, kwa upande wa mashirika yanayofanya biashara Serikali inapenda kuona yanatengeneza faida kubwa.

“Tujifunze kwa taasisi za Serikali ambazo Serikali ina hisa ndogo mfano NMB, CRDB ukiona wanavyofanya unajiuliza TCB, TIDB, TIB wanafanya nini?.

“Tujipange vizuri mwakani tuanze kuripoti matokeo ya ‘trend’ nzuri, jengeni mahusiano bora miongoni mwenu na muepukane na migogoro na migongano miongoni mwenu.

“Tumekuwa na taasisi ambazo zinashindana zote zinategemea resources za Serikali, wote wanajipanga kwenda kwa PST kuomba fedha kuanzisha programu ambazo zinafanana, lakini zina ubora mdogo.

“Tunapendana kuona zaidi ushirikiano badala ya mashindano ambayo hayana tija kabisa. Unakuta kwenye vyuo vikuu programu inaanzishwa mfano chuo au hospitali na pia chuo kingine kinapambama kutafuta hospitali wakati ipo nje tu ya chuo kingine, lakini hawashirikiani kila mtu anataka awe na chake.

“TR liangalie jambo hilo lengo ni kupata tija katika taasisi za serikali na mashirika ya umma na wananchi wetu wapate huduma bora na stahiki.

“Pia,viongozi niwatake mshiriki katika mchakato wa hesabu na ukaguzi wa mashirika yenu mutoe ushirikiano kwa CAG,mshiriki pia kujibu hoja kwa wakati msiwaachie watu wa chini.

“Mjiandae pia vizuri mnapokutana na Kamati za Bunge mtoe maelezo ya taasisi zenu na jinsi zilivyo, mafunzo yafanyike kabla ya bodi mpya kuanza kutekeleza majukumu yake hili litakuwa ni la lazima.

“Msajili ubainishe maeneo muhimu yanayohitaji mafunzo sambamba na kuwa na utaratibu wa na tabia ya kusoma sheria, taratibu na miongozo ili muweze kupata uelewa mzuri.

“Imekuwa ni jambo la kawaida Mjumbe wa Bodi kushiriki kikao bila kusoma nyaraka na makaburasha endapo hujasoma tambua mchango wako hauwezi kuwa mzuri.
“Pia mipango na maamuzi yenu naombeni mtumie takwimu sahihi na rasmi za Serikali hasa za sensa ambazo zimechambuliwa vizuri kabisa na kuainishwa vyema.

“Na mwisho nisisitize maazimio ya kikao kazi hiki tuyapate mapema, tuyaone yawezekana tukafanya maboresho baada ya mazungumzo haya mwakani tutakuja kupimwa,”alifafanua na kusisitiza kwa kina
Mheshimiwa Balozi Dkt.Kusiluka
 
Tatizo sasa hivi kuna upinzani mkubwa toka kwa wananchi wenyewe ingawa hatuuoni waziwazi. Pia kuivuruga CDM itakuwa si rahisi kwani tumeshabugi mapema kwa TAL. Mch naye kawakacha CDM kwa timing mbovu, hajawaumiza hata kidogo. Kiujumla huo mkakati hautotusaidia, labda tucopy tulichokifanya 2020 na ambayo ni ngumu kwani M/kiti hana ngozi ngumu kama ya mtangulizi wake
Yah kwa TAL mmeteleza pakubwa. Ila bado wananchi wengi wana uoga na elimu ndogo kwaio bado mna nafasi ya kurekebisha na kumaliza mchezo. Japo ushindani ndo kama hivyo sio mwepesi
 
Tatizo lako wewe bado mchanga sana ndani ya chama, niko CCM tangu 1995 nakuhakikishia yajayo yatawashangaza sana watu wa aina yako. Tunakwenda kuwa na vita ndani ya chama huku tukikabiliana na machungu ya wapiga kura, hali itakuwa si nzuri sana.
Umenena kweli kada,naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom