Rais Samia kukomba Wawekezaji na Wafanyabiashara wakubwa wa Kimarekani kuja kuwekeza Tanzania

Sasa wewe watakupa nafasi gani? Mtu hujui hata Kiswahili. Badala ya kuandika ANAJUA unaandika ANAJUWA!
 
Mwaisa ushabadilika!
 

Umekalia dudu wewe
 
Mdogo wangu Luka, unatoa sifa hizo zote huku ukiwa unaathirika na mgao wa umeme karibu kila siku iitwayo leo. Hivi kwa akili yako unadhani hayo mafuriko ya wawekezaji wa kufikirika kutoka USA hawaijui nchi hii kwa undani mpaka waje huku wakikokotwa kama mifugo!?
 
duh,hata kama ni uchawa huu umezidi kwa akili hizi umeme haurudi leo wala kesho
chawa(syphant,toady)wa kitanzania ni pro max
 
Hajui kuwa wana Ubalozi hapa na wako well informed na hali halisi ya nchi yetu kuliko huyu chawa Luka.
 
Kwanini tuongelee kuwaita wamarekani kuja kuwekeza hapa kwetu kwanini watu wa ndani wasiwezeshwe kuwekeza
 
Hivi yale mamikataba Mama alisaini kibao kule Dubai yameishia wapi?!.
Leo mmekuja na mipya.
Inaonesha hizi safari hazina tija kabisa kwa mwananchi wa kawaida zaidi ya utalii!.
Ziara na safari za mh Rais nje ya nchi Zimekuwa zenye manufaa na tija kubwa Sana kwa Taifa letu,kwa kuwa zimesaidia Sana kuimarisha mahusiano yetu ya kidiplomasia,yameimarisha na kufungua milango ya kibiashara kwa Taifa letu ambapo Sasa watanzania wanafanya biashara na mataifa mbalimbali bila bugudha,mfano kwa Sasa Tanzania na Kenya Hali Ni nzuri Sana kwa wafanyabiashara.

Ni katika ziara hizo Tumeona mh Rais akikutana na makampuni mbalimbali ya watalii na kufanya nao mazungumzo kwa lengo la kuwashawishi na kwa kuwaeleza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo hapa nchini Jambo lililopelekea kufurika na kumiminika kwa watalii hapa nchini kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu.

Ni ziara hizo na ushawishi wa mh Rais zilizopelekea kusamehewa Deni na china kiasi Cha shilling billioni 31 Fedha ambazo zitatusaidia katika miradi mbalimbali inayogusa maisha ya watanzania
 
Kwanini tuongelee kuwaita wamarekani kuja kuwekeza hapa kwetu kwanini watu wa ndani wasiwezeshwe kuwekeza
Watu wa ndani wanawezeshwa kwa kupewa kipaombele na kuwekewa mazingira mazuri ya kibiashara na kiuwekezaji, kukopeshwa kupitia mabenki ya ndani ilinkukuza mitaji yao na kupanua uwekezaji na biashara zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…