Mimi sina matatizo na mikopo kama mikopo ni ya masharti na riba nafuu, inaleta tija katika uchumi, inaimarisha ukuaji wa uchumi kwa kasi zaidi na inarudishika kwa wakati bila kuongeza maumivu kwa watu.
Katika uchumi wa dunia ya leo, hata serikali tajiri zinakopa, tena ukiangalia nchi kama Marekani na Japan zina debt to GDP ambazo zimezidi 100%. Yani madeni yao ni makubwa kuliko GDP.
Kwa data zaidi angalia hapa
worldpopulationreview.com
Kwa kweli Tanzania kwa sasa haijafikia asilimia mbaya sana za debt to GDP ratio, hata tukilinganishwa na majirani zetu kama Kenya, ila hili pia halitakiwi kutubwetesha tuzoee kukopa tu, kwani debt to GDP ratio itapanda sana.
Tanzania tuna debt to GDP ratio ya around 40%, Kenya wako 70%. Mozambique wako 124%. Eritrea wako 127%. Zambia wako 80%.
Matatizo machache ninayoyaona ni haya.
1. Serikali haina uwazi. Hatujui terms za mikopo. Hatujui riba, hatujui muda wa kulipa, hatujui masharti, hatujui tutapata wapi habari hizi kutoka serikali ya Tanzania, hatujui kwa nini serikali haitangazi habari hizi. Yani tunaweza kupata habari hizi kwa urahisi zaidi kutoka IMF, kuliko kutoka serikali yetu.
2. Serikali haina track record nzuri ya matumizi ya fedha hata kama mikopo ina terms nzuri. Ripoti ya CAG iliyopita imedhihirisha hili. Hivyo, wananchi wana haki ya kuwa skeptical.
3. Wananchi hawana imani na serikali, na hivyo wanaanza kupinga mikopo bila hata kujua data za riba, terms za mkopo etc. Hivyo hata kama mikopo ina tija, wananchi wanapinga by default tu, bila data.