ki2c
JF-Expert Member
- Jan 17, 2016
- 7,719
- 14,506
Sasa wewe unaona kuna matumizi sahihi ya kikopwacho?Hata tukiuzwa hakuna wakutununua.
Dunia ya Sasa Serikali kukopa haishangazi, muhimu matumizi mazuri ya hizo fedha.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa wewe unaona kuna matumizi sahihi ya kikopwacho?Hata tukiuzwa hakuna wakutununua.
Dunia ya Sasa Serikali kukopa haishangazi, muhimu matumizi mazuri ya hizo fedha.
Fedha tulizokuwa Tunawadai Barick gold Mbona Maza kupiga kimya? Kuna wakati walitulipa usd 100 milion wakati wa JPM.Kipindi cha mwendazake Budget asilimia 62 ilikuwa fedha za ndani 38 ndio ilikuwa za wahisani na mikopo lakini bajeti hii ya sasa nakwambia tutarudi kulekule zaidi ya nusu ya bajeti kutegemea wahisani . Sasa tujiandae kabisa na kupokea masharti yao ya kibepari maana pesa zao tunakula.
Mimi naona kama vile serikali yetu inakopa tu bila mpangilio maalumu.Mimi sina matatizo na mikopo kama mikopo ni ya masharti na riba nafuu, inaleta tija katika uchumi, inaimarisha ukuaji wa uchumi kwa kasi zaidi na inarudishika kwa wakati bila kuongeza maumivu kwa watu.
Katika uchumi wa dunia ya leo, hata serikali tajiri zinakopa, tena ukiangalia nchi kama Marekani na Japan zina debt to GDP ambazo zimezidi 100%. Yani madeninyao ni makubwa kuliko GDP.
Kwa data zaidi angalia hapa
National Debt by Country / Countries with the Highest National Debt 2024
worldpopulationreview.com
Kwa kweli Tanzania kwa sasa haijafikia asilimia mbaya sana za debt to GDP ratio, hata tukilinganishwa na majirani zetu kama Kenya, ila hili pia halitakiwi kutubwetesha tuzoee kukopa tu, kwani debt to GDP ratio itapanda sana.
Tanzania tuna debt to GDP ratio ya around 40%, Kenya wako 70%. Mozambique wako 124%. Eritrea wako 127%. Zambia wako 80%.
Matatizo machache ninayoyaona ni haya.
1. Serikali haina uwazi. Hatujui terms za mikopo. Hatujui riba, hatujui muda wa kulipa, hatujui masharti, hatujui tutapata wapi habari hizi kutoka serikali ya Tanzania, hatujui kwa nini serikali haitangazi habari hizi. Yani tunaweza kupata habari hizi kwa urahisi zaidi kutoka IMF, kuliko kutoka serikali yetu.
2. Serikali haina track record nzuri ya matumizi ya fedha hata kama mikopo ina terms nzuri. Ripoti ya CAG iliyopita imedhihirisha hili. Hivyo, wananchi wana haki ya kuwa skeptical.
3. Wananchi hawana imani na serikali, na hivyo wanaanza kupinga mikopo bila hata kujua data za riba, terms za mkopo etc. Hivyo hata kama mikopo ina tija, wananchi wanapinga by default tu, bila data.
Huku sarakasi za Mlimani City zikiendelea Serikali ya Samia imeomba mkopo wa 1.1 billion US dollars kutoka IMF kwa mujibu wa msemaji wake Zuhura Yunis, IMF wako nchini kujadili, one thing is clear walipaji wa haya madeni ni sisi wananchi!
View attachment 2221901
Bloomberg - Are you a robot?
www.bloomberg.com
Zanzibar wanakopa au wanasubiri mgao wa mkopo then bara waje walipe mkopo?Kukopa ni sawa kama mkopo ni riba ya chini ya 5% na miaka ni 10 au zaidi
Mwisho itabidi tukate sehemu ya taifa letu tuwape.Yetu macho.Huku sarakasi za Mlimani City zikiendelea Serikali ya Samia imeomba mkopo wa 1.1 billion US dollars kutoka IMF kwa mujibu wa msemaji wake Zuhura Yunis, IMF wako nchini kujadili, one thing is clear walipaji wa haya madeni ni sisi wananchi!
View attachment 2221901
Bloomberg - Are you a robot?
www.bloomberg.com
Kukopa sio sawa,I disagree.Unapaswa kuwa dependent.Misled minds ndizo zinazo-amini kwamba kukopa ni sawa,it is not.Kukopa ni sawa kama mkopo ni riba ya chini ya 5% na miaka ni 10 au zaidi
Wacha akope hadi afikie record ya Magufuli.
Madeni ya Magufuli yalikuwa world cup. Kuifikia hiyo record siyo leo. Kazi iendelee
Mama tuonee huruma watanzania. Hay madeni makubwa makubwa yatatupa shida sana mbeleni. Fanya kile unachoweza kwa vyanzo vya ndani. hata ufanyejeTanzania haiwezi kugeuka ulaya over night. wanasemaga wenyewe hata roma haijajengwa siku moja. na wala watanzania hawanaga shukurani. elewa hilo.
Leo inabidi niulize swali ambalo wenye uwezo wa kulijibu, huenda watapata wasaa mzuri wa kulijadili.IMF wako nchini kujadili, one thing is clear walipaji wa haya madeni ni sisi wananchi!
Sasa ruzuku ya kwenye mafuta hela itatoka wapi!?Huyu mama tumepigwaaaa
Leo inabidi niulize swali ambalo wenye uwezo wa kulijibu, huenda watapata wasaa mzuri wa kulijadili.
Hawa akina IMF na WB hutoa mikopo, mara nyingi mikopo ambayo ina riba nafuu, lakini mikopo inayoambatana na masharti ambayo waktati mwingine huwa ni machungu zaidi katika kuyatekeleza ndani ya nchi hizo zinazokopa.
Mikopo ya hizi taasisi ni tofauti na mikopo inayotolewa na mabenki, au maelewano kati ya serikali na serikali, ikiwa ni pamoja na riba kuwa juu, na masharti ya kurudisha hiyo pesa iliyokopwa.
Nchi inapodaiwa na nchi nyingine, mara nyingi huwa ni aibu kwa nchi mdaiwa. Mabenki ya kibiashara, yanapokopesha, halafu nchi ushindwe kulipa, hapo kuna shida kubwa sana!
Sasa swali langu ni hili: Haya mahela ya hawa jamaa wa IMF au WB, tukiyachukua mengi kadri iwezekanavyo, na tukaacha ujuha wetu (wa viongozi wasio na uchungu na nchi), mahela haya yakatumika ipasavyo. Yakajenga mashule, barabara na mambo mengine muhimu ambayo tunaona yatatusaidia kwenda mbele haraka zaidi. Baada ya yote haya, tukawa wagumu wa kuyarudisha mahela hayo kwa wenyewe, IMF na WB, kwa sababu hela kidogo iliyopo kulipa mamikopo yao tunategemea kuifanyia miradi mingine ya kimkakati.
Je, haya majamaa ya IMF au WB watatuitia polisi na kutupeleka mahakamani?Najuwa watakuwa wagumu kuendelea kutupatia mikopo mingine kabla hatujalipa hiyo waliyokwishatupa, lakini tukauma meno, na kukataa kulipa!
Hebu nifundisheni.
Binafsi, haya mahela ya IMF na WB, mbali ya masharti yanayotolewa; haya ndiyo mahela tunayotakiwa kuyazoa kwa wingi, mradi tu tuweze kuyatumia vizuri kwa kazi zetu.
Na hizo ziara za mama ughaibuni zinazovhukua wajumbe wanaojaza basi zinalipiwa na fedha kutoka wapi?Hiyo itakuwa ni stimulus loan kwa ajili ya kusawazisha hali ya kiuchumi.......muhimu ni hiyo mikopo kutumika kuleta tija zaidi.
Huenda anaingalia bei halisi ya nchi hiiNdugai sijui anasemaje?!
Hapana, wanatofautiana digrri 180.Magufuli na Samia wote akili yao moja.
Mimi sina kamba ila nimefungiwa zizini! Nitakula hapa hapa zizini ambapo hamna kitu?Mkuu popote ulipo jipimie kadiri ya urefu wa kamba yako ....
Kasema kiongozi sisi tukatae ni nani?