Rais Samia kukopa(tena) 1billion USD from IMF

Fedha tulizokuwa Tunawadai Barick gold Mbona Maza kupiga kimya? Kuna wakati walitulipa usd 100 milion wakati wa JPM.
 
Mimi naona kama vile serikali yetu inakopa tu bila mpangilio maalumu.

Hakuna efforts zozote za maana za ku address wasteful and unnecessary spending.

Tumeona juzi hapa Rais alienda Marekani akakaa takriban wiki mbili kwa ajili ya kuzindua documentary kuhusu vitu ambavyo tayari vinajulikana.

Aliongozana na rundo la watu. Na wala hakupaswa kukaa huko muda wote huo.

Serikali iliingia gharama kiasi gani toka hiyo safari yake ya Marekani? Hatujui maana hakuna uwazi.

Na wote alioambatana nao, ilikuwa ni lazima aambatane nao? Sidhani!

Tanzania tuna austerity measures gani za kueleweka kuhusu government spending, revenue collection, etc?

Pesa tunazokopa kuna ulazima kweli wa kuzikopa?

Mi naona tunakopa kopa bila hata mpangilio.
 
Kukopa ni sawa kama mkopo ni riba ya chini ya 5% na miaka ni 10 au zaidi
Kukopa sio sawa,I disagree.Unapaswa kuwa dependent.Misled minds ndizo zinazo-amini kwamba kukopa ni sawa,it is not.
 
akiisha kopa saana mwisho wa urais wake atasema madeni aliyokopa sio yeye aliyekopa ni marehemu Magufuli ndio aliyekopa na machawa zake watamsapoti kina Zito na Nape na CAG
 
Wacha akope hadi afikie record ya Magufuli.

Madeni ya Magufuli yalikuwa world cup. Kuifikia hiyo record siyo leo. Kazi iendelee

Deni la Magufuli ilikuwa ngapi unayo data au ishibiki wa chadema unauleta humu
 

Usijali deni tutambambikia magufuli watanzania wataelewa tu maana wengi ni mkumbo
 
IMF wako nchini kujadili, one thing is clear walipaji wa haya madeni ni sisi wananchi!
Leo inabidi niulize swali ambalo wenye uwezo wa kulijibu, huenda watapata wasaa mzuri wa kulijadili.

Hawa akina IMF na WB hutoa mikopo, mara nyingi mikopo ambayo ina riba nafuu, lakini mikopo inayoambatana na masharti ambayo waktati mwingine huwa ni machungu zaidi katika kuyatekeleza ndani ya nchi hizo zinazokopa.

Mikopo ya hizi taasisi ni tofauti na mikopo inayotolewa na mabenki, au maelewano kati ya serikali na serikali, ikiwa ni pamoja na riba kuwa juu, na masharti ya kurudisha hiyo pesa iliyokopwa.
Nchi inapodaiwa na nchi nyingine, mara nyingi huwa ni aibu kwa nchi mdaiwa. Mabenki ya kibiashara, yanapokopesha, halafu nchi ushindwe kulipa, hapo kuna shida kubwa sana!

Sasa swali langu ni hili: Haya mahela ya hawa jamaa wa IMF au WB, tukiyachukua mengi kadri iwezekanavyo, na tukaacha ujuha wetu (wa viongozi wasio na uchungu na nchi), mahela haya yakatumika ipasavyo. Yakajenga mashule, barabara na mambo mengine muhimu ambayo tunaona yatatusaidia kwenda mbele haraka zaidi. Baada ya yote haya, tukawa wagumu wa kuyarudisha mahela hayo kwa wenyewe, IMF na WB, kwa sababu hela kidogo iliyopo kulipa mamikopo yao tunategemea kuifanyia miradi mingine ya kimkakati.

Je, haya majamaa ya IMF au WB watatuitia polisi na kutupeleka mahakamani?Najuwa watakuwa wagumu kuendelea kutupatia mikopo mingine kabla hatujalipa hiyo waliyokwishatupa, lakini tukauma meno, na kukataa kulipa!

Hebu nifundisheni.

Binafsi, haya mahela ya IMF na WB, mbali ya masharti yanayotolewa; haya ndiyo mahela tunayotakiwa kuyazoa kwa wingi, mradi tu tuweze kuyatumia vizuri kwa kazi zetu.
 
NA ZIKIJA HIZO NI KUGAWANA NUSU KWA NUSU NA ZANZIBAR.
DISCO KAINGIA MMASAI.
HUU MUUNGANO NYERERE ALITUINGIZA CHA KIKE.
 

Unafikiri Dunia ina Nchi ngapi labda ? Na unafikiri wote hao ni wajinga na hawataki pesa za bure za kuchukuwa tu kama wewe na raisi wako mnavyodhania ?
 
Hiyo itakuwa ni stimulus loan kwa ajili ya kusawazisha hali ya kiuchumi.......muhimu ni hiyo mikopo kutumika kuleta tija zaidi.
Na hizo ziara za mama ughaibuni zinazovhukua wajumbe wanaojaza basi zinalipiwa na fedha kutoka wapi?

Vv
 
Sio jambo Baya as long as pesa ikitumika ilivyo kusudiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…