Rais Samia: Kuna wanaojiita wanaharakati lakini kiuhalisia matendo yao ni ya kigaidi

Rais Samia: Kuna wanaojiita wanaharakati lakini kiuhalisia matendo yao ni ya kigaidi

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Rais Samia ametoa onyo hilo leo Alhamisi, Julai 9, 2026, Ikulu ya Zanzibar wakati akihutubia hafla ya tamko la pamoja la maridhiano ya kisiasa Zanzibar baina ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo.

Pia Soma:

"Nataka nitumie pia fursa hii kuwaonya wale wote wanaojiita wanaharakati kwa jina ili wapate kutambulika duniani, lakini kiuhalisia matendo yao ni ya kigaidi.

Nataka niseme kidogo tafsiri ya ugaidi. Ugaidi unajumuisha vitendo vya uvunjifu mkubwa wa amani, uharibifu wa mali na miundombinu, vinavyokusudia kuitishia jamii au kuishurutisha serikali kukubaliana na matakwa ya watu au kundi fulani kwa ajili ya kutimiza haja za kisiasa, kiitikadi au kidini.


Lakini, kwa mustakabali wa sasa, dunia tunayokwenda nayo, unaweza ukafanyika pia ukikusudia kuirudisha nyuma nchi inayoendelea kwa kasi—pia inaweza ikatumika.

Watu au kundi hilo linakuwa na kauli zinazovaa sura ya kizalendo lakini kwa undani ni maslahi binafsi. Mtu anayeipenda nchi yake kiukweli huijenga na sio kuibomoa"

 
Screenshot_20260706-111052.png
 
Back
Top Bottom