Rais Samia, kunyamaza kuhusu matatizo ya Watanzania ni kufurahia shida zao

Nsanzagee

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2023
Posts
2,209
Reaction score
4,769
Ni kweli kabisa sisi TANZANIA ndo wa kuhangaika kutafuta kituo kipi chenye mafuta, hapa Tanzania, kweli kabisa Rais?

Umeme, vibarua wote wanaofanya kazi kwenye viwanda, wanalaza njaa watoto wao, gereji, salon, wanaishi kwa tabu sana kwa sasa

Mungu akupe moyo wa kutovumilia haya mateso ya Watanzania kwa kushindwa tu kuwakemea wafanyabiashara na Mawaziri wazembe!

Mimi nakataa kabisa kwamba, eti sisi tuna upungufu wa mafuta, nakataa kabisa kwamba, nchi yetu ina tatizo la upungufu wa kuzalisha umeme?

Huyo Mwenzenu aliweza vipi kwenye suala la umeme?
 
Kama hizo hela ziliingilia mdomoni basi zitatokea mahali popote palipo wazi!!!" Magufuli.


Waliojigeuza marketing officers wa kampuni la DP world na madalali wote waliokula hizo hela za kuhongwa ujumbe uwafikie.

Kama mlikuwa mnanunua magari na kuyaandika majina yenu mtakiona cha mtema kuni safari hii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Shida ilianza pale alipoanza kutoa vijembe.

Huyu Maza anauswahili Swahili SANA.
Kiufupi andharau SANA.
Huwezi mambo ya msingi kama mafuta unakakmya.
 
😭😭😭
 
Je kukaa kimya ni kuto kuchukua hatua?
 
[emoji2][emoji2]kwa watu wa mwambao neno”kukaa kimya”

Maana yake ni”kelele za chura hazimnyimi tembo kunywa maji”

yeye anendelea na harakati zake bwabwajeni mkichoka mkalale.

17/match tulipigwa kama taifa.
 
Ni kweli kabisa sisi TANZANIA ndo wa kuhangaika kutafuta kituo kipi chenye mafuta, hapa Tanzania, kweli kabisa Rais?

Umeme, vibarua wote wanaofanya kazi kwenye viwanda, wanalaza njaa watoto wao, gereji, salon, wanaishi kwa tabu sana kwa sas...
Kwenye hili simlaumu Samia pekee bali ni mfumo mzm wa utawala wa CCM!! Mfumo haujawahi kua na nia ya dhati ya kumkomboa mtanzania. Tanesco kile ni kitengo, maji bado ni kizungumkuti tang uhuru, huduma za afya tembelea vijijin na maeneo mengine ya mjin hakuna huduma strictly wala madawa, watanzania wa leo angalau wapo waojitafutia riziki kupitia mitandao sasa check rungu walilopigwa kweny bando 🀣🀣🀣🀣🀣!!
 
Uongozi ni kuonesha njia siyo kunyamaza. Ukiona kiongozi ananyaza kwenye masuala mazito ya kitaifa yanahitaji akili na maamuzi makini ujue hana misuli na misingi ya kiongozi.

Mtu kama huyu tegemeo lake kubwa ni muda ndiyo ufanye maamuzi. Jambo lolote liwe baya ama zuri litakalojiri yeye kwake sawa tu
 
Wengi wao watu wa hivyo ni zero brain, na pia ujumbe wake anasema hana akili hajui cha kusema kwa kuwa ni kilaza hana cha kusema amefika mwisho wa akili yake.

Au ni kejeli kwamba nimewaacha nyie tumbili muongee ila mimi najua cha kufanya
 
MAMA NYAMAZA USIWAJIBU WAJINGA WAJINGA
DP WORLD KARIBUNI TANZANIA
 
Mwanzoni nilikuwa siamini kuwa ukimya wa rais kwa wanaotoa matusi kwake kuhusu suala la bandari kuna watu unawaumiza na kuwakosesha amani, ila kwa post yako hii nimeamini wewe ni mmoja wa wanaosumbuliwa kisaikologia na ukimya wa rais.
 
Anatusemea Jk
 
Jibu lake " NIMEAMUA KUKAA KIMYA"

hiyo ndiyo busara na chawa wanampongeza πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

Akili za hovyo sana.
 
Wabongo tunapenda kulialia kama mtoto anayeogopa sindano hakuna maendeleo yanayokuja kirahisi tu.
 
Rais kunyamaza ni ishara ya kwamba hakufaa kuwa rais.Nchi imeharibika kila sehemu lakini hakuna hatua yeyote aliyochukua.suluhisho hapa ni katiba.katiba izuie marais wa kurithi.kurithishwa kitu ambacho hujakipambania huwa hakithaminiwi hasa hawa watu wa mwambao wa bahari ya hindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…