Rais Samia kupokea ndege mpya ya ATCL Julai 30, 2021

Rais Samia kupokea ndege mpya ya ATCL Julai 30, 2021

Wange cancel hizi Ndege hela tukazipeleka kwenye kujenga barabara maana hizi ndege ni hasara.
 
Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan kesho atapokea ndege mpya ya ATCL.

Ndege hiyo ni miongoni mwa zile 11 zilizoagizwa na serikali yy awamu ya 5 chini ya hayati Magufuli

Mtanikumbuka - JPJM

Mungu ni mwema wakati wote!
hivi hizi pangabobya zina faida kwetu kweli? kwenye mkoa nilipo havifiki na sijawahi kuvipanda.
 
Nilishausahau huu mchezo kumbe bado unaendelea, zile zilizopo mpaka ripoti ya mwisho ya CAG zilikuwa zinatengeneza hasara, labda hiyo mpya itakuja na mambo mapya.
Fedha ilishatolewa awamu ya 5.....
 
Dah afu ukiangalia haya mengine yanavyopiga ruti za serikali tu unaweza ukasema bora hata yale mav8 undeshaji wake ni nafuu kuliko mandege
 
Tuliingizwa hasara tu, mwisho wa siku hazina haina kitu wakati ndege zilizopo zinaingiza tu hasara
 
Hizi zilishawekewa order kwenye awamu ya JPM kwahiyo hatuna ujanja lazima zije tu zote.

Najua order iliwekwa kipindi cha awamu ya tano. Lakini hawaoni haya wakafanya kimyakimya haya mapokezi?

Lakini ikiwa wizara ya afya wamebadili gia angani, ina maana yeyote anaweza kujitoa ufaham wakati wowote.
 
Hivi hawa watu hua wanatuonaje?
CAG anaongea hadi koo linakauka anagonga glass ya maji ya baridi mbele ya kamera akisisitiza shirika letu la ndege ni hasara mwanzo mwisho...tukiwa bado tunaugulia maumivu ya tozo, unapigwa kanzu na mapokezi ya dege jingine.
Ripoti ya CAG ilisemaje kuhusu hesabu za vyama vya siasa including chadema.

Ukitoa majibu ndio uje uhoji hesabu za atcl .

Halafu hizi ndege ni za serikali ya tanzania sio atcl.
atcl amekodishiwa tu.ni mkodishwa tu kama anavyoweza kuwa fastjet & nk

Akivurunda once again
Atafurumishwa.
 
Ripoti ya CAG ilisemaje kuhusu hesabu za vyama vya siasa including chadema.

Ukitoa majibu ndio uje uhoji hesabu za atc...
Haukatazwi kuhoji ripoti ya CAG kuhusu chochote ikiwepo vyama vya siasa.

Hapa ajenda ni kupokea ndege, jikite kwenye hoja inayojadiliwa. Kingine, ni kosa kumpachika mtu uana chama wa chama chochote cha siasa.
 
Back
Top Bottom