PreGE2025 Rais Samia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa "Umoja Wa Wanaume Tanzania" utakaofanyika Dodoma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Umoja wa Wanaume Tanzania unatarajia kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi huu wa nne na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa umoja huo utakaofanyika Dodoma.

Malengo makuu ya umoja huo ni kuwaunganisha Wanaume wote ndani ya Tanzania na kuwa kitu kimoja ili washirikiane kupinga kwa nguvu zote aina zote za ukatili ndani ya Jamii hususani ni kwa Wanawake na Watoto na hata baadhi ya Wanaume wanaonyanyaswa kuanzia ngazi ya Familia na Jamii.

Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amesema hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, wakati DC Gondwe alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, kufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanaume Tanzania, ambao umefanyika Mkoani Singida ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkubwa utakaofanyika Mkoani Dodoma utakaombatana na uzinduzi wa umoja huo.

DC Gondwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, ametoa wito kwa Umoja wa Wanaume Tanzania kuwa chachu ya maadili mema kwa Vijana wa kiume na akina Baba

β€œTumieni Umoja huu, kuwakumbusha Vijana wa kiume na akina Baba, kuwajibika katika Familia na nchi ili kupunguza madhara yanayotokea kwa kuharibi Famili, katika tamaduni zetu, Wamasai wana njia bora ya kulea Vijana wa kiume kuwa Wanaume, zipo tamaduni zetu bora zitunzwe”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amekabidhi Katiba ya Umoja na Nyaraka mbalimbali za usajili na Gondwe ameahidi kuzifikisha kwa Mkuu wa Mkoa Halima Dendego ambaye amewaahidi kuwapa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Wanaume Tanzania.



Source: Millard Ayo
 
Hivi karibuni Makamu wa Rais Mpango na Waziri Gwajima walitoa wito wa Kutambuliwa Kwa siku ya Wanaume Duniani kama Sherehe rasmi ya Serikali kama livyo siku ya Wanawake.

Sasa inatarajia Rais Samia kuzindua mkutano Mkuu wa wanaume Dodoma ambapo huenda akatangaza Serikali kuanza kuadhimisha siku ya Wanaume Duniani kama Sherehe rasmi.

View: https://x.com/millardayo/status/1907394428605489608?t=CrnkL1k1f7KaDhiXfRTDqA&s=19
My Take
Wanaume mumefikiwa,Sasa huenda manyanyaso yakapungua maana Tutapata watetezi wengi.
 
Hii nchi imerogwa sijui na nani,kha!.Huo umoja wa wanaume unaozinduliwa na mwananke una manufaa gani kwa Taifa au ni kujikombakomba kila mahali.
 
Ila nyie wanaume anayezindua s raisi wa nchi sasa mmefikiwa maneno tena yamekua memgi, iwepo na kailo mbiu ya baba na wanae, kila baba atunze mtoto ama watoto wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…