PreGE2025 Rais Samia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa "Umoja Wa Wanaume Tanzania" utakaofanyika Dodoma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hivi karibuni Makamu wa Rais Mpango na Waziri Gwajima walitoa wito wa Kutambuliwa Kwa siku ya Wanaume Duniani kama Sherehe rasmi ya Serikali kama livyo siku ya Wanawake.

Sasa inatarajia Rais Samia kuzindua mkutano Mkuu wa wanaume Dodoma ambapo huenda akatangaza Serikali kuanza kuadhimisha siku ya Wanaume Duniani kama Sherehe rasmi.

View: https://x.com/millardayo/status/1907394428605489608?t=CrnkL1k1f7KaDhiXfRTDqA&s=19

My Take
Wanaume mumefikiwa,Sasa huenda manyanyaso yakapungua maana Tutapata watetezi wengi.

Duh!.
 
Umoja wa Wanaume Tanzania unatarajia kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi huu wa nne na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa umoja huo utakaofanyika Dodoma.

Malengo makuu ya umoja huo ni kuwaunganisha Wanaume wote ndani ya Tanzania na kuwa kitu kimoja ili washirikiane kupinga kwa nguvu zote aina zote za ukatili ndani ya Jamii hususani ni kwa Wanawake na Watoto na hata baadhi ya Wanaume wanaonyanyaswa kuanzia ngazi ya Familia na Jamii.

Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amesema hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, wakati DC Gondwe alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, kufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanaume Tanzania, ambao umefanyika Mkoani Singida ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkubwa utakaofanyika Mkoani Dodoma utakaombatana na uzinduzi wa umoja huo.

DC Gondwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, ametoa wito kwa Umoja wa Wanaume Tanzania kuwa chachu ya maadili mema kwa Vijana wa kiume na akina Baba

“Tumieni Umoja huu, kuwakumbusha Vijana wa kiume na akina Baba, kuwajibika katika Familia na nchi ili kupunguza madhara yanayotokea kwa kuharibi Famili, katika tamaduni zetu, Wamasai wana njia bora ya kulea Vijana wa kiume kuwa Wanaume, zipo tamaduni zetu bora zitunzwe”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amekabidhi Katiba ya Umoja na Nyaraka mbalimbali za usajili na Gondwe ameahidi kuzifikisha kwa Mkuu wa Mkoa Halima Dendego ambaye amewaahidi kuwapa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Wanaume Tanzania.

View attachment 3291212

Source: Millard Ayo

Kama akiendelea kukubaliana na huu ujinga kuna siku ataalikwa kwenye Kitchen party Buguruni.
 
Taratiiibu mpaka tutaanza kusikia mwanaume akiwezeshwa anaweza. Tuendelee tu na hii michezo.
Hao watakuwa mashoga tu, wanaume wa kweli hawawezi kushiriki ujinga kama huo.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Hii nchi kila ukiamka vituko ni vipya haviishi
 
Umoja wa Wanaume Tanzania unatarajia kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi huu wa nne na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa umoja huo utakaofanyika Dodoma.

Malengo makuu ya umoja huo ni kuwaunganisha Wanaume wote ndani ya Tanzania na kuwa kitu kimoja ili washirikiane kupinga kwa nguvu zote aina zote za ukatili ndani ya Jamii hususani ni kwa Wanawake na Watoto na hata baadhi ya Wanaume wanaonyanyaswa kuanzia ngazi ya Familia na Jamii.

Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amesema hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, wakati DC Gondwe alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, kufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanaume Tanzania, ambao umefanyika Mkoani Singida ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkubwa utakaofanyika Mkoani Dodoma utakaombatana na uzinduzi wa umoja huo.

DC Gondwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, ametoa wito kwa Umoja wa Wanaume Tanzania kuwa chachu ya maadili mema kwa Vijana wa kiume na akina Baba

“Tumieni Umoja huu, kuwakumbusha Vijana wa kiume na akina Baba, kuwajibika katika Familia na nchi ili kupunguza madhara yanayotokea kwa kuharibi Famili, katika tamaduni zetu, Wamasai wana njia bora ya kulea Vijana wa kiume kuwa Wanaume, zipo tamaduni zetu bora zitunzwe”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amekabidhi Katiba ya Umoja na Nyaraka mbalimbali za usajili na Gondwe ameahidi kuzifikisha kwa Mkuu wa Mkoa Halima Dendego ambaye amewaahidi kuwapa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Wanaume Tanzania.

View attachment 3291212

Source: Millard Ayo
Kama ni kukumbushia wajibu wa uanaume hapo sawa. Isije ikawa yale ya sisi wanaume kuanza kulilia haki kama wanawake.

Endapo kama sisi wanaume tukifanya kosa kuruhusu kuanza harakati za kupiganiwa wanaume basi tutegemee kuzalisha kundi kubwa la mashoga.

Tukumbuke uanaume ni kupambana sio kulia, sio kulalamika, wala sio kuhitaji huruma kwenye jamii. Kama hayo hutaki jihesabu wewe sio mwanaume.
 
Hapo mimi siwezi kwenda kwa sababu mada kuu itakua uchaguzi.
Na kwa nini mgeni rasmi asiwe makamu wa rais au waziri mkuu, au ndio mwendo wa kuiga kwa mama zetu. Ni siku ya wanaume mama anakujaje?
 
Back
Top Bottom