PreGE2025 Rais Samia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa "Umoja Wa Wanaume Tanzania" utakaofanyika Dodoma

PreGE2025 Rais Samia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa "Umoja Wa Wanaume Tanzania" utakaofanyika Dodoma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mara paaap umoja huo wanaanzisha vicoba, wanaanza kukopeshana, kudhulumiana, wanarushiana ngumi umoja unakufa.
 
Kule kanisani kuna wwk, kwa muda mrefu hakukuwa na chama cha wanaume kanisani, juzi nao wameinuka na kutaka pawe na chama cha wanaume kanisani. Mambo ya kitaifa wanaume nao wanataka wawe na chama chao na kitambuliwe. Majukumu yake itakuwa nini? Watapata uwakilishi bungeni kama uwt?
 
Uanamume ni hela na utawala - mengine ni mbwembwe tupu.
 
Mkuu wa Mkoa anaweza kufunga milango halafu akamuambia Dokta awapime Tezi Dume sijui mtafanya nini mtaruka madirishani?!huu utawala wa CCM hauaminiki.
 
Wanawake waliomo humu wanasemaje kuhusu kuanzishwa umoja wa wanaume Tanzania?
 
Wanaume nawo wameanza kujitambua,maana wamebeba mizigo mingi sana kwa kisingizio cha gender.
 
Mmh utakuwa Hauna msaada wowote kwa wanaume ni ujanja ujanja tu wa 2025 msisahau ni mwaka huu Kuna tukio kubwa mtaona mengi...
 
Mwenye picha ya MKITI WA wanaume Tanzania Claude Benedict. Huyo mkiti alichaguliwa na nani na wapi
 
Muda unakwenda kasi sana, wanaume kweli umefika muda wa kujitafuta kudai haki hadi kuwa na umoja ni hatari.
 
Huu ni umoja wa kihuni ulioona fursa za kupiga hela za mama nyakati hizi za kampeni.
 
Nchi ya KIsanii katika Usanii, utadhani tuna muda wa kufanya vitu petty yaani yote ya maana tumemaliza...
 
Umoja wa Wanaume Tanzania unatarajia kuzinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi huu wa nne na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa umoja huo utakaofanyika Dodoma.

Malengo makuu ya umoja huo ni kuwaunganisha Wanaume wote ndani ya Tanzania na kuwa kitu kimoja ili washirikiane kupinga kwa nguvu zote aina zote za ukatili ndani ya Jamii hususani ni kwa Wanawake na Watoto na hata baadhi ya Wanaume wanaonyanyaswa kuanzia ngazi ya Familia na Jamii.

Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amesema hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe, wakati DC Gondwe alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego, kufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanaume Tanzania, ambao umefanyika Mkoani Singida ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkubwa utakaofanyika Mkoani Dodoma utakaombatana na uzinduzi wa umoja huo.

DC Gondwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, ametoa wito kwa Umoja wa Wanaume Tanzania kuwa chachu ya maadili mema kwa Vijana wa kiume na akina Baba

“Tumieni Umoja huu, kuwakumbusha Vijana wa kiume na akina Baba, kuwajibika katika Familia na nchi ili kupunguza madhara yanayotokea kwa kuharibi Famili, katika tamaduni zetu, Wamasai wana njia bora ya kulea Vijana wa kiume kuwa Wanaume, zipo tamaduni zetu bora zitunzwe”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wanaume Tanzania (CWWT), Claude Benedict Kim amekabidhi Katiba ya Umoja na Nyaraka mbalimbali za usajili na Gondwe ameahidi kuzifikisha kwa Mkuu wa Mkoa Halima Dendego ambaye amewaahidi kuwapa eneo la ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Wanaume Tanzania.

View attachment 3291212

Source: Millard Ayo
Hakunaga umoja wa wanaume kwakuwa wanaume hawana haja ya umoja wowote ule kuwahusu bali kuna umoja wa wanawake na mashoga tuu
 
Tanzania wanaume tumepungua(nasi tunahitaji kulindwa)

1970,Sheria ya ndoa(family law) ilitungwa mwanamke afikapo miaka 14 aolewe lengo kuu ni kumlinda na manyang'au

miaka 55 badae ,eti umoja wa wanaume umeundwa

Bangladesh kabisa

Mimi,kwasasa uholanzi
 
Back
Top Bottom