Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania, umesema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuongoza sherehe za Siku ya Sheria Februari 2, Chinagali jijini Dodoma, badala ya Februari Mosi, 2022.
Hatua ya kuahirisha sherehe hizo zilizokuwa zifanyike Februari Mosi imetokana na sababu zisizoweza kuzuilika.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Jaji Mkuu kitengo cha habari, Elimu na Mawasiliano, Tiganya Vicent kauli mbiu ya mwaka huu ni Zama za Mapinduzi ya nne ya Viwanda; Safari ya Maboresho kuelekea Mahakama Mtandao.