Rais Samia kuzindua Mradi wa Kihistoria wa Bwawa la Mkomazi wenye thamani ya Bil 18. Mradi uliobuniwa zaidi ya miaka 50 ilopita

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Ningependa kutoa taarifa rasmi kuhusu hafla muhimu ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Bwawa la Mkomazi na utiaji saini wa mikataba miwili (2) ya ujenzi wa Skimu za Mkomazi na Chekelei Wilayani Korogwe, mkoani Tanga ambayo itafanyika tarehe 24 Februari 2025, ambapo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa mgeni rasmi.
IMG-20250223-WA0174.jpg

Mradi wa Mkomazi ni wa kihistoria, uliobuniwa zaidi ya miaka 50 iliyopita lakini umekuwa ukisuasua kutekelezwa kwa muda mrefu. Serikali ya wamu ya sita (6) chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha kwa ajili ya kuutekeleza mradi huu ili kuwanufaisha wananchi zaidi ya 20,000 kutoka kata saba za Mkomazi, Mkumbara, Mazinde, Mombo, Chekelei, Makuyuni na Magila Gereza.

Mradi wa Mkomazi unagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 18 utahudumia vijiji 28 katika kata saba (7) katika wilaya ya Korogwe. Aidha, mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 2025. Kazi zinazotarajiwa kufanyika ni pamoja na ujenzi wa tuta la udongo la kuzuia maji, ujenzi wa barabara kuelekea eneo la mradi, na ujenzi wa ofisi ya meneja wa mradi.
IMG-20250223-WA0177.jpg

Wakati wa hafla hiyo, Rais Samia pia atashuhudia utiaji saini Mkataba wa ujenzi skimu ya Mkomazi yenye jumla ya Hekta 9,000 ambayo itahudumia kata hizo na vijiji 28 na kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 48.3. Vilevile, Rais atashuhudia utiaji saini wa mkataba wa mradi wa Chekelei ambao ni ujenzi wa bwawa na skimu yenye ukubwa wa hekta 1049 ambayo itawanufaisha wananchi kutoka vijiji vinne(4) vya Madala, Madumu,chekelei na Chepete ambayo itagharimu Shilingi Bilioni 31.2.

Tuna imani kuwa miradi hii itachochea maendeleo na kuboresha maisha ya wakazi wa Korogwe na maeneo jirani. Tunawashukuru wote kwa ushirikiano na tunawaomba muendelee katika juhudi hizi za kimaendeleo, kupitia kilimo cha Umwagiliaji

Raymond Mndolwa

Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)
 
Ningependa kutoa taarifa rasmi kuhusu hafla muhimu ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Bwawa la Mkomazi na utiaji saini wa mikataba miwili (2) ya ujenzi wa Skimu za Mkomazi na Chekelei Wilayani Korogwe, mkoani Tanga ambayo itafanyika tarehe 24 Februari 2025, ambapo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa mgeni rasmi.
View attachment 3246515
Mradi wa Mkomazi ni wa kihistoria, uliobuniwa zaidi ya miaka 50 iliyopita lakini umekuwa ukisuasua kutekelezwa kwa muda mrefu. Serikali ya wamu ya sita (6) chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha kwa ajili ya kuutekeleza mradi huu ili kuwanufaisha wananchi zaidi ya 20,000 kutoka kata saba za Mkomazi, Mkumbara, Mazinde, Mombo, Chekelei, Makuyuni na Magila Gereza.

Mradi wa Mkomazi unagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 18 utahudumia vijiji 28 katika kata saba (7) katika wilaya ya Korogwe. Aidha, mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 2025. Kazi zinazotarajiwa kufanyika ni pamoja na ujenzi wa tuta la udongo la kuzuia maji, ujenzi wa barabara kuelekea eneo la mradi, na ujenzi wa ofisi ya meneja wa mradi.
View attachment 3246514
Wakati wa hafla hiyo, Rais Samia pia atashuhudia utiaji saini Mkataba wa ujenzi skimu ya Mkomazi yenye jumla ya Hekta 9,000 ambayo itahudumia kata hizo na vijiji 28 na kugharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 48.3. Vilevile, Rais atashuhudia utiaji saini wa mkataba wa mradi wa Chekelei ambao ni ujenzi wa bwawa na skimu yenye ukubwa wa hekta 1049 ambayo itawanufaisha wananchi kutoka vijiji vinne(4) vya Madala, Madumu,chekelei na Chepete ambayo itagharimu Shilingi Bilioni 31.2.

Tuna imani kuwa miradi hii itachochea maendeleo na kuboresha maisha ya wakazi wa Korogwe na maeneo jirani. Tunawashukuru wote kwa ushirikiano na tunawaomba muendelee katika juhudi hizi za kimaendeleo, kupitia kilimo cha Umwagiliaji

Raymond Mndolwa

Mkurugenzi Mkuu, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)
Jifunze kuleta habari, ni mradi wa maji tu au wa umeme pia?
 
Miradi chini yake huyu mama aimaliziki. Mfano Bwawa la Nyerere linasuasua, Mwendokasi Dar es salaam ipo ICU kabla hata ya kumalizika
Bila kusahau mradi wa bonde la mto msimbazi hakuna kinachoendelea ilhali world bank walishatoa hela
 
Back
Top Bottom