Rais Samia kwa hili la kuruhusu Mashirika ya Umma kuajiri nakupa pongezi sana

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
“Kuna mashirika ambayo wenyewe wangehitaji ajira za harakaharaka lakini unaambiwa subiri Tume ya Utumishi ikae, subiri sijui utumishi ifanyeje mwaka mzima taasisi kwa mfano TRA inataka watu wakakusanye mapato mwaka mzima watu hawajapatikana, vivyo hivyo TANESCO, REA wanataka watu utumishi paka izunguke iseme ifanye mikutano ifanye semina, hapana hatuendi hivyo.

Kama wanataka wafanyakazi mishahara ya kulipa wanayo haitoki hazina wanataka wafanyakazi kwa ajili ya mradi au kazi fulani wapewe ruhusa wafanye. Wapewe ruhusa wafanye sabahu ajira hizi wala nyingine sio za kudumu mradi ukimalizika na ajira imekwenda. Kwa hiyo wapewe ruhusa waajiri ili miradi ikatekelezwe kwa haraka.” Rais Samia Suluhu Hassan

Napenda kujikita hapa kwa TRA: Nafasi za kazi za TRA zilitangazwa mwezi wa nne 2022, watu wamekuja kuitwa kwenye usaili mwezi wa 12 2022. Wakati huohuo watu wameitwa kazini mwezi wa pili 2023. Muda mwingi umepotea hapo.



Msisahau kurejea huu uzi:
 
Moja ya vikwazo vikubwa vya maendeleo nchini ni wizara ya utumishi! Imejaa watu wenye urasimu uliokithiri kiasi hata mtu mwingine ukihamishiwa hapo unaambukizwa!

Ni vema wizara hii ifumuliwe kabisa kuanzia katibu mkuu hadi muhudumu vinginevyo hali hii itaendelea na wanaoathiriwa ni wananchi!
 
Hatutaki.
 
Dola ya Tanzania isiruhusu hili jambo. Huyu mama aache haraka haraka. Haraka haraka haina baraka. Atapotea. Apewe ile ripoti ilipropose kuanzishwa kwa utaratibu wa ajira unaotumika sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…