Rais Samia kwa hili la kuruhusu Mashirika ya Umma kuajiri nakupa pongezi sana

Rais Samia kwa hili la kuruhusu Mashirika ya Umma kuajiri nakupa pongezi sana

Najiuliza maswali mengi tu...na itanichukua muda kupata majibu niweze kujiridhisha na machache aliyosema, ingawaje ni makubwa ki mantiki... n.k


Je, kuna uwezekano wa mpango huo kuwa ni wa- kubadilisha mfumo mzima wa nini na nani ni Taasisi ya Serikali.... Kwa manufaa ya nani?

Je, waweza hatarisha Usalama wa Taifa?

je Mpango huo ukifanikiwa utaweza kurahisisha ubinafsishaji wa Idara za Serikali? i.e TRA? REA? Mashirika ya Umma i.e TANESCO? alimradi hazichoti fedha Hazina?

Because it will set precedent- kama haichukuwi hazina....Ruksa kwenye mambo mengi baadae?

Are we chipping away our sovereign state?



Hizo Tume alizozitaja ni Tume zilizo na Nguvu Kikatiba?

Anaweza Kuwa anavunja KATIBA?

Je, Kauli yake ndio itakuwa ndio hivyo? Mwisho? yaani Ruksa sasa.?

Bunge linashauri vipi?

Hivi kuna Mbunge au Wabunge watakao peleka muswada kuhusu ubadilishaji wa Sheria hizo?
Je, itahusisha na mabadiliko madogo ya Kikatiba? au kwa yale aliyosema ndio Sheria, Ruksa? bila ya kuzingatia hayo juu?

Kama ni ya Kikatiba na Sheria, Mh Tundu Lissu ana lolote la kusema kuhusu 'Ruksa' hiyo au... 'Mungu watu' wengine ni 'Ruksa' Je, ana play Double standards?....hivi ni kweli ana visasi binafsi?


Kulikuwa na sababu gani za msingi Tume hizo ziwe na nguvu Kikatiba....Usalama wa Taifa?


Dah nimekumbwa

Kitaeleweka.

Ni jambo jema, na nina uhakika atakuwa amepata ushauri mzuri na usio na lengo lolote lingine ispokuwa kupunguza makali ya Ajira nchini. Natamani iwe kwa ajili kuwaajiri 'Watanzania' na sio kufanya Ujio mpya wa 'xpatriate'.

Muda utaeleza.
 
Back
Top Bottom