Rais Samia kwa hili la kuruhusu Mashirika ya Umma kuajiri nakupa pongezi sana

Dola ya Tanzania isiruhusu hili jambo. Huyu mama aache haraka haraka. Haraka haraka haina baraka. Atapotea. Apewe ile ripoti ilipropose kuanzishwa kwa utaratibu wa ajira unaotumika sasa.
Ndio hivyo tuna raisi aliyekauwa makamu wa raisi lazima awe ni mtu anayefaham mambo sasa anashinswa nini kutafuta sababu zilizofanya ajira ziwe centralized
 
Nilivyomuelewa ni kwa yale mashirika ambayo yana miradi ya kimkakati tu na bajeti ya mishahara hausishi hazina ndiyo wawe na Uhuru wa kuajiri Ili kuchochea kasi ya utekelezaji wa miradi.
 
Mashirika mengi hasa yasiyopokea ruzuku ya serikari, mishahara yao haitokei hazina. Nahao naongelea permanent and pensionable employees
 
Syo kitu kigeni.
wakati wa mkapa alibadilisha sheriia kuruhusu mashirika kuajiri na kujilipa kwa jinsi wanavyozalisha.
sheitwan alipoingia kaanza ujinga bila hata,sheria kubadilishwa.
anachotaka mama ni ile sheria kufatwa
Mfumo wa ajira kupitia sekretariati ya ajira ulianza 2007 wakati wa uatawala wa awamu ya tano. Sidhani kama ulikusudia kumuita nani shetwani. Ni JK? Unachangia bila takwimu.
 
Nilivyomuelewa ni kwa yale mashirika ambayo yana miradi ya kimkakati tu na bajeti ya mishahara hausishi hazina ndiyo wawe na Uhuru wa kuajiri Ili kuchochea kasi ya utekelezaji wa miradi.
Kwani ajira za mikataba ya muda mfupi inayopitia sekretariet ya ajira?
 
Kupata kazi ndio kutoboa, Lengo la kazi ni kutuibia wananchi au?
 
mm nimeelewa kuwa hizo ajira ni za muda mfupi na si za kudumu ndo maana kasizitiza kama taasisi ina pesa za kuwalipa na si kutoka hazina waendelee.kama mshahara utatoka hazina utaratibu utabaki kama ulivyo kwa sasa.naunga mkono tume ya ajira inahitaji mabadiliko makubwa sababu kuna ukiritimba mkubwa sana wa kusaili na kuwaita wasailiwa kazini,pia nako kuna upendeleo mkubwa,vimemo vya wakubwa vimezidi kiasi kwamba vinawakatisha tamaa watoto wa walalahoi.unaona kabisa aliyeshinda usaili nii kilaza kabisa tena wakati mwingine mlisoma naye halafu usaili kashinda,darasani alikuwa mtu wa mabomu.hii si haki.chombo hicho kiangaliwe tena upya.
 
Mfumo wa ajira kupitia sekretariati ya ajira ulianza 2007 wakati wa uatawala wa awamu ya tano. Sidhani kama ulikusudia kumuita nani shetwani. Ni JK? Unachangia bila takwimu.
Naomba uniwekee hapa mkuu nione kama hiyo sekretarieti ilipewa majukumu kwa ajira za MASHIRIKA YA UMMA au ni serikali kuu na serikali za mitaa
 
Hapa wenye nacho ndiyo wanaongezewa,kama huna connection huna haja ya kuapply popote,fanya mambo mengine tu
 
Me nafanya kazi serikalini ila hili boko bab kubwa ndugu yangu, Fanya research kwa miaka miwili itakayokuja kutatokea upuuz hauwez amini, hapa watoto wa maskini wanaenda kuzurumika, amini kwamba
Mkuu kwani ajira sa mashirika ya umma zilikuwa zinafanywa na tume toka mwaka gani, na je wakati kabla sekretarieti haijaanza ajira zilikuwa kwa kina nani. watoto wa walala hoi walioko vijiweni toka wakati huo ni wangapi
 
Hizi ni dalili za mtu ,amefikia mahali anasema liwalo na liwe,watajijua na Kijiji Chao ,na familia zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…