Rais Samia kwa tamaa kubwa ya Vyeo CCM Kwako, nakushauri uwe Unawaficha wale Uwapendao na unaotaka kuwa nao kuanzia 2025

Rais Samia kwa tamaa kubwa ya Vyeo CCM Kwako, nakushauri uwe Unawaficha wale Uwapendao na unaotaka kuwa nao kuanzia 2025

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Labda nikuambie tu Rais Samia kuna Uteuzi Mmoja wa Kimkakati umeufanya Jana ila sasa Umeshamsababishia matatizo Mhusika kwani kama hajarogwa awe Mweusi kuliko alivyo sasa ili Usiwe unamuona au Kumkumbuka kama yuko basi wanaweza Kumaliza Shughuli kabisa na hiyo 2025 asiione au akiiona atakuwa si huyu tena.

Kama kuna Chama hapa Tanzania kina tabia ya mwonekano wa Mto Wami ambao ukiuangalia kwa Juu unaona Maji yake yametulia tuli ila kwa chini yanaenda Kasi ya Hatari basi ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho Wewe ndiyo Mwenyekiti wake/ wao Taifa.

Ukitaka Unafiki utaukuta CCM, ukitaka Majungu utayakuta CCM, ukitaka Kusagiana Kunguni utakukuta CCM, ukitaka Utapeli / Uwongo utaukuta CCM, ukitaka Wivu usio na sababu baina ya Wanachama utaukuta CCM, ukitaka tabia ya Kuchongeana ili Kuharibiana Uongozini / Madarakani utakukuta CCM, ukitaka Uchawi na Ushirikina uliokomaa / uliotukuka utaukuta CCM na ukitaka UMAFIA kwa Kuwahishana mazima Udongoni Kinondoni / Kisutu pia utaukuta CCM.

Namuonea mno Huruma uliyemteua.
 
Pacha ni muungwana sana yule jamaa, ila nawasiwasi na wale wazee wa lindi wataalam wa moshi uliomkimbiza baba jesca na kukatisha ziara yake enzi zile.

Hata wana namungo nao ni waungwana na sidhani kama wana mpango na 2030. Kwa msingi huo, naamini watafanyakazi kwa umoja sana.

all in all kesho kwenye hotuba ya mwana kizimkazi itatoa majibu yote. Si unajua naye ni 'muungwana' hawezi kupasuka, lazima atajikoshakosha.
 
Angesubiri tu 2025 aisee.kumficha hawezi kwa sasa.
 
Umenikumbusha kisa cha Nabii Yusuph na Baba yake Nabii Yaakub

Mapenzi makubwa ya Nabii Yaakub kwa Mwanae Yusuph yakapelekea chuki kwa Nduguze Yusuph kumchukia Mwenzao kwa kuwa tu ni kipenzi cha Baba yao hadi wakamtosa kisimani


Mapenzi hayo ndio yaliyomgharimi Hayati Mzee Kawawa kwa Nyerere, Hayati Kighoma Malima kwa Mzee Mwinyi, Hayati Dr Abdallah Kigoda kwa hayati Mzee Mkapa, Hayati Benard Membe kwa Jakaya na Makonda kwa Hayati JPM


Bosi akikupenda sana lazima Wajumbe wakufanyishie

akina Balozi Getrude Mongela walimkomesha Mzee Kawawa 1985 hadi akaukosa Urais kwa kuwa tu alikuwa kipenzi cha Hayati Kambarage
 
Mhusika kwani kama hajarogwa awe Mweusi kuliko alivyo sasa ili Usiwe unamuona au Kumkumbuka kama yuko basi wanaweza Kumaliza Shughuli kabisa

Itoshe kusema tu jamaa anapendwa sana na MAZERI ,umempa ushauri mzuri ,awe makini sana isije parapanda ikalia mapema kwake.
 
Acheni fikra potofu,katika utawala ambao kiongozi wa nchi hajawahi kuonesha kumpenda mtumishi wake zaid ya wengine ni huu.

Iko hivi,uteuzi wa kugawana majukum katika kile kiti ni kutokan na baadhi ya watumishi mpaka ngazi za chini kabisa kutokuwa waaminifu katika kutimiza majukum yao ndy maana ikabidi wawe wawili ili kumpunguzia majukum mengi huyu aliyekuwepo.

Utakumbuka kwamba namungo fc amekuwa akilalamikia san watendaji kwa rushwa na mambo mengine na ndicho atakachoendelea nacho ndyo maana huy msaidizi atashughulika na mambo ya kuiwakilisha serikali kweny international issues tu lakini huku kwenye kupambana na madc,ded,ras sijui na wengine ndyo huyu mzee wa namungo ataendelea nako
 
Back
Top Bottom