Rais Samia kwenye ziara yako huko Misri kuwa makini na ishu ya maji ya ziwa victoria

Kinachonichukza katika enzi hizi za mitandao ya jamii: utakuta mtu hata hana ufahamu wa issue, lakini atataka kuchangia, tena kana kwamba maoni yak tu ndiyo bora na sawa.
Aliyeleta makala hii namsifu kwa kulifahamu suala hili . I hope kuw kiongozi wetu analifahamu suala hili. Lakini pia nadhani kuimarisha mahusiano na Misri, nchi ya tatu kwa uchumi mkubwa Afrika, ni jambo la lazima. Wamisri pia wana techinical know-how kubwa, hasa katika masuala ya uhandisi wa maji. Basi awatake tu watusaiie kufufua mito yetu na mabwawa yaliyokauka kwa uzembe na kutopatiliza, kama bwawa la Mabatani, Muheza.
 
Asipofanya kama ulivo shauri utafanyaje? We kausha tu, hivi vitu viko nje ya uwezo wako. Haki inapiganiwa haiombwi, utalalamika mpaka mda wa kuishi duniani unaisha we bado unalalamika
 
Kwa taarifa yako maji yanayofika Misri asilimia kubwa yanatoka Ethiopia na sio lake Victoria.
Ndio utaona Uganda walipo amua kujenga bwawa la pili wala Misri haikulalamika tofauti na Ethiopia inapojenga bwawa la Reinancess kesi imefika UN na Marekani ndio msuluhishi
Tusijipe umuhimu mkubwa tusiostahili.
 
Umenikumbusha kakitu muhimu sana sana! Misri ipo radhi iingie vitani kwa sababu ya hayo maji. Umenifunua macho kuhusu mgogoro wa Ethiopia! Kwa hakika hawa jamaa wana mkono wao pale.
Hawa jamaa hawataki tutumie maji ya Ziwa Victoria kwa shughuli zetu, hata ule mradi wa bomba la maji toka Mwanza kwenda Kahama ilibidi Waziri wa Maji enzi hizo, Bwana Laigwanan, afanye kichwa ngumu tu na jeuri ya lubega ndio maji yaende ila Misri walikuwa hawataki. Sasa nasikia Serikali ina mpango wa kupeleka maji toka Ziwa Victoria kwenda Dodoma, huenda General wa Misri analijua hilo na akalichomekea.
Haiingii akilini ati tuna maji tusiyatumie kwa kuwa Misri wana sijui mkataba wa mwaka 1910; wakachukue maji Uingereza huko siyo kwetu.
 
Mbona walipiga yowe tulipochukua maji ya Ziwa Victoria kwenda Kahama?
 
Yaani Misri imemwita Rais Samia kwa sababu ya mto Nile,hakuna jingine kwenye ziara hiyo,kwa uboya wa Samia mtakuja kusikia muda si mrefu,hakuna kutumia maji ya ziwa Victoria kwenye kilimo,
 
Kwa hiyo unaushauri Tuwakabidhi kabisa mto Nile sisi Tuachane nao si ndiyo?
 
Wamisri ndo wanaamini hivyo, kuwa mto Nile utakauka
 
Asije kusema hatukumtahadharisha. Hao waarabu wanaonaga sisi mafala na kwamba wao wajanja sana. Mama asije kurudia makosa kama yale ya kumpa yule mkora tony blair mkataba wa kutusemea halafu anatusemea mambo hajatumwa. Mama awe makini asije tia saini kuhusu chochote maji ya victoria.
 
Sielewi! Mungu kanipa chanzo kizuri cha maji katika mji wangu, eti nipangiwe na jirani namna ya kutumia maji yangu. Nasema kwa kujiamini! Natumia maji yangu ila kiasi kinachobaki nakuachia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…