Pre GE2025 Rais Samia: Machifu waambieni wanasiasa ukweli vyeo havipatikani kwa kuua watu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sijui tumeamua kuwa nchi ya Wasirikina au tumeamua kurudi Zama za mababu. Kazi ambayo imewashinda Polisi baada ya kuwa watuhumiwa No.1 Leo wamekabidhiwa Machifu. Labda Amiri Jeshi amegundua kweli Polisi ni wahusika au hawana uwezo.
Kwenye hii kazi wangeongezwa Waganga wa kienyeji tungemaliza tatizo mapema.
 
Mh rais nimemuelewa , machief ni sehem ya jamii ,kwa maana nyingine jamii ianze kushughulika na watekaji, maana yake ukitaka kutekwa piga mwayo majambazi hao ili wakipate cha mtema kuni ,ni kwa maono yangu tu
 
Kuna dogo kapotea muimbili huu mwezi wa sita sasa kimya
 
Mtemi Isike akiwakamata watekaji atawapa adhabu ya kutafuna mawe hadi yawe unga na ndio wataacha.. ndio maana Hangaya kawarudia
 
Sijui Nina matatizo ya ubongo Ila sijawahi kujivunia kuwa mtanzania, naishi Tanzania kwa vile Sina mbadala!
 
Wanatekana kutokana na kumomonyoka kwa maadili, lazima machief waingilie Kati, hayo mambo huji yakuta kwa chief wa mbeya na chief mkwakwa Iringa
 
kwamba polisi na intelijensia imeshindwa hadi tuombe msaada kwa hao wachawi.
 
Rais Dkt Samia amesema hayo wakati akizungumza na Mchifu wenzake huko Ikulu Dodoma. amesema anasikitishwa sana na vitendo vya kikatili vinavyo endelea nchini vya kuuwa watoto na kunyofoa viungo vyao.
amesema kuwa Vitendo hivyo kwa asilimia kubwa yanahusishwa na Uchaguzi/Chaguzi.

hivyo amewaonya wale wote wenye uchu wa vyeo au madaraka kutokutumia njia za kishirikina kama vile kusaka viungo vya binaadamu ili kupata cheo au uteuzi.
amesisitiza kuwa Vyeo havipatikani kwa kuuwa au kwa njia za kishirikina.

Utafiti usio rasmi unaonyesha kuwa viongozi wengi katika nafasi mbalimbali wanatumia ushirikina ama kupata cheo au kulinda nafasi walizo nazo. viongozi wengi sana wanaendekeza ushirikina kuliko kutegemea Imani ya Mungu. ndio maana tunapata viongozi wababaishaji wasio jiamini.

tupinge ukatili unao endelea, tuwafichue wahusika wote katika maeneo yetu.
 
Nadhani Mheshimiwa Rais ameongea maneno mazuri pale na sasa watu wananukuu maneno yake out of context,na kusababidha Rais alaumiwe.
Kuhusu hayo mambo yanayoitwa mambo ya uchawi,Rais anawaalika machifu kutoa msaada ili huu uovu uweze kuthibitiwa,ili haya mambo ambayo hayana mantiki yakomeshwe.
 
Wanatekana kutokana na kumomonyoka kwa maadili, lazima machief waingilie Kati, hayo mambo huji yakuta kwa chief wa mbeya na chief mkwakwa Iringa
Kuna mkoa Una matukio ya upotezaji watu kuzidi Mbeya? Kuchuna ngozi Mbeya, kuua Wenye upara Mbeya, kunyofoa korodani Mbeya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…