Rais Samia: Majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru', hawana migogoro? Auliza nini kinafatwa kwenye tume huru

Mimi sitaki tume huru wala katiba mpya.

Nataka watu waelimishwe kwanza wajitambue kabla ya kuvipata vyote hivyo.

Hakuna tija ya kuwa na vifaa vipya kabla ya kujifunza kwanza kuvitumia.

Tuondoane ujinga kwanza ndio twende huko.
Kwani ile task force iliyokua inakwapua fedha za watu kwenye account na maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ilianza kutoa elimu kwanza.

Ukweli ni kuwa kwa tume hii ambayo ni favourable kwa CCM hawawezi ikubali ibadilishwe imagine yule Mahera kada wa CCM ndio mkurugenzi wa tume na bila aibu mnamleta awe mgeni rasmi wa hiyo TCD.

Ndio maana hata Bashiru alikua bold enough kusema watashinda uchaguzi 2020 kwa msaada wa dola na ndio kilichotokea mkasema mmeshinda kwa kishindo na matokeo yoyote ya ngazi hiyo mmeyapiga ban kutohojiwa kortini.

There is no any means for CCM to sanitize the evils of the current regime.
 
Mama anaweweseka. Anajua hawezi kushinda urais wa Tanzania kwa haki...

Kura za kwenye vikapu lazima zitumike na hakuna kupinga matokeo mahakamani!!
Kwahiyo kumbe lengo kubwa la Tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya Ni kushinda uchaguzi🤣🤣🤣
 
ukisikia UWEZO WAKO NDIO ULIPOISHIA ndio hizo kauli za mama. Yaani hapo ndio SKY
 
Tume huru isipoendana na Katiba inayo wezesha tume huru kuwa tume huru tutakuwa hatujafanya kitu. Lingine la muhimu ni kuwa na viongozi na wananchi wapenda na wapigania HAKI.
 
Tume inaongozwa na Hamad Rashid, apo ni usanii mtupu. Labda anadhani wananchi hawana uwezo wa kuchambua na kufahamu. Hata mie nisie na elimu kubwa ya sheria bado nina uwezo wa kujua mabadiliko yana usanii au ni mabadiliko ya kuchenguana.

Samia hadi sasa hana tofauti na watangulizi wake sarakasi, my basic definition sioni momentum ya mabadiliko ya sheria. Sheria ziko vile vile watu wanapiga soga na kujitokeza na vigurupu kazi.
 
Huenda kuna mambo yanakuchanganya sana kwenye demokrasia, wewe ni cynic wa kiwango cha juu, unafanya strawa man fallacy au appeal to extreme fallacy, lakini fahamu.

Hakuna kitu au mfumo perfect duniani,

Hakuna gari, ndege, treni,meli, rubani na dereva perfect lakini hiyo haiwafanyi binadamu rational wanaoweza kupata huduma za gari n.k kuendelea kutumia punda na farasi wakati huu.

Hakuna madaktari au dawa perfect lakini hilo halizuii watu kusisitizwa kwenda hospitalini zaidi badala ya kung'ang'ania mitishamba na waganga wa kienyeji.
Mifano iko mingi.

Ni uzwazwa na counterproductive kila mara watu wanapojaribu kuboresha jambo au hali halafu kuna mtu yeye anajaribu kuonyesha hakuna kitu perfect ili hali hakuna hata mtu mwenye madai hayo kwa kuanzia.
 
Huenda kuna mambo yanakuchanganya sana kwenye demokrasia, wewe ni cynic wa kiwango cha juu, unafanya strawa man fallacy au appeal to extreme fallacy, lakini fahamu.
Nani kasema mimi ni cynic wa demokrasia..., faida moja kubwa ya demokrasia ya kufanya watu waridhike na kutokufanya fujo au kulalamika is the price worth paid..., ila haimaanishi tuseme kwamba kinachopatikana katika muundo na utendaji ndicho kilicho kwenye theory..., democracy has its pros and cons kila mtu anajua ila hatuwezi tukabadilisha cons na kusema ni pros sababu tu its the best way of ruling....
Hakuna kitu au mfumo perfect duniani,
Nani kasema upo ?
Hakuna gari, ndege, treni,meli, rubani na dereva perfect lakini hiyo haiwafanyi binadamu rational wanaoweza kupata huduma za gari n.k kuendelea kutumia punda na farasi wakati huu.
Je inamaanisha huyo dereva asiendelee kupata mafunzo ya mara kwa mara au kuangalia kama anaweza kuboresha anachofanya.
Hakuna madaktari au dawa perfect lakini hilo halizuii watu kusisitizwa kwenda hospitalini zaidi badala ya kung'ang'ania mitishamba na waganga wa kienyeji.
Mifano iko mingi.
Kwahio doctors kila siku hawa-perfect their trade ? To perfect and look better ways ndio development, haimaanishi tuseme sababu demokrasia its not really power to the people haimaanishi turudi kwenye aristocracy hapana bali ni jinsi gani tunaweza tukamuwezesha mwananchi zaidi kwenye decision making
Ni uzwazwa na counterproductive kila mara watu wanapojaribu kuboresha jambo au hali halafu kuna mtu yeye anajaribu kuonyesha hakuna kitu perfect ili hali hakuna hata mtu mwenye madai hayo kwa kuanzia.
Hakuna Demokrasia ya kweli mpaka sasa thriving to reach that goal is the way to go..., Sasa ni Uzwazwa kusema tumefika wakati hatujafika sababu hapo hauwezi kuboresha....

Without knowing or admitting there is a problem how can one solve such problems ? Wewe una-thrive ili uwe kama USA, Canada na Ulaya mimi nakwambia even theirs is not perfect and can be perfected..., which means am thriving for something better than theirs.....
 
Inatakiwa Tume huru yenye uhuru kamili, na siyo uhuru isiyo na uhuru kama ile ya Jecha.
 
Ikiwa default setting ya mifumo ya tawala za kibinadamu ni uimla(autocraticism), kivipi demokrasia in it's purest form inaweza kuleta shida kama hizo za tyranny of majority? Kwamba kwenye autocraticism minority rights zina uhakika wa kuheshimiwa sana AU ulimaanisha demokrasia bado inaweza isiziondoe hizo shida?

Madhara ya Lobbying za interest groups na blah blah nyingine ulizozitaja hapo chini ni malalamiko yako tu(ambayo ni petty) dhidi ya mifumo ya demokrasia , sio kila mtu anaona Lobbying za makampuni/wafanyabiashara (kwenye kodi, udhibit , mazingira wezeshi n.k), Lobbying za vyama vya wafanyakazi n.k ni mbaya.
 
Mtu yeyote anayehisi hatuhitaji mabadiliko ya katiba Kama nchi ni MSALITI lazima tuweke baadhi ya vitu sawa. Hatutakiwi kuwaza Leo tu huo ni ubinafsi watu wanatetekeza mali za umma, watu wanatumia Nafasi zao vibaya wananchi hatuna chakuwafanya wote tunasubiri Rais ndo aamue this is not fair. Siungi mabadiliko ya katiba kwa sababu ya CHADEMA ila ni kwa mapenzi tu ya Taifa langu TANZANIA.
 
Kinachomfanya aogope tume huru sio migogoro ila kupoteza nafasi. CCM ni waoga sana kwenye kupoteza madaraka ya nchi maana wanajua uchafu wao huko ni mwingi na hawana uhakika atakayekuja kama atawaacha salama.
 
Wasiohitaji mabadiliko au katiba mpya ni wale wanufaika wa katiba iliyopo. Huwezi amini samia aliyekuwepo kwenye bunge la katiba 2014 eti leo anajifanya hamnazo na kudharau takwa hili kisa yupo madarakani.
 
Maana-Chombo free kitakachosimamia shughuli za uchaguzi na utangazwaji wa washindi.....Je ikiwa upinzani wamewahi kukiri kuwa; baadhi ya makada wake yenyewe, wakiwamo wenye nyazifa za juu; kununuliwa na CCM, hawatailalamikia tume hiyohiyo kuwa imehongwa na ccm? siku mambo yakiwa tofauti? coz being free sio kigezo cha kutohongeka.
 
Fikiria hizo ni kauli za mkuu wa nchi. Maana yake Mkuu wa Nchi haifikirii Tz ya kesho anawaza CCM Vs Chadema tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…