Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Viongozi Wateule katika ukumbi wa Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 04 Aprili, 2024.
RAIS SAMIA: MAWAZIRI MKAJIBU HOJA ZA CAG
RAIS SAMIA: BILI ZA MAJI NI KILIO KWA WANANCHI, NAAGIZA WALIPE KAMA WANAVYOLIPA UMEME
Soma: Napendekeza meter za maji zifungwe mifumo ya ‘LUKU’
RAIS SAMIA: MAKONDA UMEKICHEMSHA CHAMA, NINA IMANI NA WEWE
Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Mabadiliko katika Mfumo wa ulipaji wa Huduma za Maji akielekeza mchakato ufanyike ili malipo yafanyike kadiri Mtu anavyotumia kama ilivyo kwenye ununuaji wa Umeme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Deogratius John Pancras Ndejembi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa mkoa wa Mara kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Viongozi mbalimbali Wakiapa Kiapo cha Maadili kwa viongozi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.