Rais Samia: Mashtaka dhidi ya Mbowe sidhani kama yamechochewa kisiasa. Natamani kukutana na Wapinzani


Kwamba siyo Siasa?

1. Kwa nini wanazuwia watu kwenda mahakamani?
2. Kwanini alikamatwa usiku usiku pamoja na waliokuwa wamepanga kwenda kwenye kongamano la kisiasa?
3. Kwa nini kongamano hilo la siasa lilizuiliwa kufanyika kabisa na katika siku 2 tofauti?
4. Kwanini watu walikamatwa hata kwa kuvaa t-shirts tu za kongamano hilo la kisiasa?
5. Kwa nini kumekuwa na mizengwe mfululizo kwenye zoezi zima la kushikiliwa mheshimiwa Mbowe, kufikishwa mahakamani kumwona rumande au hata kumfikishia chakula?
6. Yapo mengi.

Mama anazidi kujiweka njia panda.

Hivi ile rebranding bado ipo au kwenye wave #3 haikuweza kufua dafu?
 
Rais SSH amehojiwa na Salim Kikeke wa BBC Swahili, kwa mtazamo wangu, yeye kama Rais hakutakiwa kutawaliwa na matumizi ya neno "nadhan"! Yaani majibu na maelezo yake yote yeye ni kudhani tu.

Kuna umuhimu wa kufundishwa namna nzuri ya kujibu maswali kama kiongozi wa nchi. Huku kudhani, unadhani means huna uhakika.

 
Kajifundishe Kiswahili,neno kudhani,katika kiswahili,lina maana nyingi,mojawapo unaposema,nadhani,ni kuwa na uhakika na unachosema.Ni kama mtu kuulizwa,"Utaendelea kusoma?"Na akajibu "Nadhani,hapa ndio mwisho".Ikiamanisha kuwa ana UHAKIKA,haendelei tena kusoma.
 
Kajifundishe Kiswahili,neno kudhani,katika kiswahili,kina maana nyingi,mujawapo unaposema,nadhani,ni kuwa na uhakika na unachosema.Ni kama mtu kuulizwa,"Utaendele kusoma?Na akajibu "Nadhani,hapa ndio mwisho".Ikiamanisha kuwa ana UHAKIKA,haendelei tena kusoma.
 
Urais ni taasisi ndugu yangu mambo mengine yanafanyika hata yeye "NADHANI" huwa hajui. Rais hasilaumiwe sanaa
 
Samia angeamua kufuata maamuzi yake binafsi hao wasaidizi wake wangekuwa upande wake watake wasitake, tatizo lako silka yake ya kutaka kumridhisha kila mmoja ndio inapelekea asieleweke na wengi anaowaongoza, ukimfurahisha kila mmoja lazima kuna maeneo utafanya maamuzi yatakayowashangaza wengi.
 
Huyu mama walimsifia, akajaa sifa. Walikua wanampamba anaupiga mwingi, akapiga hadi mpira ukapasuka.

Hayu mama hakua amejiandaa kwa high office, wala hakutegemea. Na hii ndio shida, vyama vya siasa wajitunze makamo wa rais one day anaweza kua rais. Sasa kama mnachagua makamo kwa sababu zisizo na msingi badala ya uwezo ndio haya yanayotukuta.

Maza magenge ya wahuni yamemuingiza kingi akaingia mzima mzima, sasa yanafanya yanachokitaka. Mama hana sauti, mama hana maamuzi yake indepently, inaonekana ni kama kuna watu wanamshinikiza.

Maza hata wale waliokua wanamuombea aongezewe muda zaidi sasa hawana ham nae tena.

Ngoja tusubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…