Kila nchi ina shetani wake.
Shetani wa Tanzania ni CCM.
Wezi wa mali za umma ni CCM .
Mapolisi wenye agenda za binafsi za kujipendekeza ili wapate uteuzi kwa kuwaumiza wapinzani wapo CCM
Waliouza mali za umma na kujimilikisha wenyewe ni CCM.
Wanaotumia katiba mbovu kutesa watu huku wao wakiishiaisha ya starehe ni CCM. Wanaovuruga uchaguzi kwa mitutu ya bunduki halafa wanasema uchaguzi umeisha hatutaki siasa njoni tuchape kazi ni CCM. Waliopandikiza Viongozi wa taasisi za dini na kuwatumia kuhalalisha uovu wao kwa faida binafsi huku haki ikikanyagwa ni CCM.
IGP anatumiwa na CCM kuumiza watanzania na kuwafanya waishi kwa Chuki kwa faida ya watu wawili au wa Tatu ndani ya Taifa bila kujifunza kuwa kundi la S. Gang na akina Sabaya waliumiza watu na kuua watu kwa ajili ya kumfurahisha mtu mmoja na sasa hayupo akerudi mavumbini na nafsi yake moja tu. Kuua au kutesa watu wengi kwa sababu ya mtu mmoja anayetumia katiba vibaya ni dhambi kubwa sana inayofurahiwa na shetani CCM.
Mafuta wanapandisha na tozo za simu halafu wanatumia mabilioni kufanya masherehe ya kukimbiza mwenge usio na roho wala nafsi lakini unazungushwa nchi nzima kama ibada ya Sanamu ya CCM halafu kwa unafiki wanamtumia Gwajima kujifanya kama vile Mungu anaishi Tanzania tena ni mwana Chama wa CCM.
Ninaamini kuwa Mungu wa Kweli atasimama kuhukumu kwa Haki. Na pia ninaamini kuwa Mungu hawezi kukaa kimya miaka yote akaangalia tu Shetani CCM inavuruga uchaguzi halali ,inaua watu ili matokeo yabadilishwe , inanyanganya watu fomu za uchaguzi, inatumia hila kulinda katiba mbovu inayowalinda watu wachache wafanye wanayotaka bila kuhaojiwa.
Nchi imekua ni ya kupeana ulaji tu kwa kuteuana nafasi za mishahara minono bila kufanya applicationi ili watu wote wawe huru kuomba.
Mungu anauwezo mkubwa kuliko CCM na majeshi yake yote na kila kitu kitapita isipokuwa yeye. Ipo siku Mungu atawainua watu wenye mioyo ya kupenda Haki kuliko Maisha yao huo utakua ndio mwisho mbaya sana kwa CCM na vizizi vyake na ushetani wao.
Mungu hajawahi kukosa watu wa kuingia ndani ya moto na kutoka bila kuungua kwa ujasiri mkubwa. Mungu hawezi kutukuzwa kwa Dhulma. Janga la Korona linaua bila ubaguzi lakini CCM inaua watu wasio na hatia kibaguzi na kutesa watu kwa dhulama.
Demokrasia ipi ya kutumia Bunduki kuiba masanduku ya kura?
CCM na akina Siro na Wale waliombambikia mbowe Kesi ya Ugaidi wangeweza kuepuka hasira itakayokuja kama wangekua wanafanya hayo kwa haki bila kuangalia maslahi yao lakini wanawashitaki watu kwa uongo ili kulinda nafasi zao na maslahi yao waliyoyapata kwa dhulma na rushwa. Mungu hatakaa kimya kama sio kwa ni kwa watoto wao.
Hivi kwe enzi za Magufuli kuna mtu angeweza kutengeneza njama za kuua viongozi asikamatwe kwa ushahidi kabla hata hajaamka kitandani asubuhi.? Kwa nini mashitaki watu kwa uongo? Siro ni Mkristo uliyesoma Uru Seminari ,je ,huko ndiko kumwakilisha Kristo kwenye nafasi kubwa uliyopewa ya kusimamia haki za watu kikatiba? Umri wako ,maisha yako ,kazi nzuri uliyoiganya kwa kipindi kirefu hukustahili kabisa kukubaliana na huu ujenzi wa chuki miongoni kwa Watanzania unaofanywa na CCM na Magenge yake yaliyojificha kwenye vyombo vya dola.
Dunia ilitoka kwenye ushenzi wa madikteta na wafalme katili walioua watu kama mbu na wengine mpaka kuzikwa na watu hai eti wanawalinda huko kaburuni. Zama hizo zilipita kidogo kidogo mpaka sasa Demokrasia inawapa nguvu wananchi na kuwafanya wawe kama binadamu na sio wanyama mbele ya watawala.