Rais Samia: Mbowe alijificha Nairobi aliporudi akaanza harakati za madai ya Katiba, nadhani ni Calculation akijua kwamba ana kesi

Rais Samia: Mbowe alijificha Nairobi aliporudi akaanza harakati za madai ya Katiba, nadhani ni Calculation akijua kwamba ana kesi

Mahojiano na Salim Kikeke. Inaonekana Rais yupo nyuma ya hii yote. Na yoote yanayofanyika anaangalia tuu.

Anyway Leo ndo nimemjua rais tulienae.

----
KESI DHIDI YA FREEMAN MBOWE

Kikeke:
Nazungumzia suala hilo la kisiasa kwa sababu kiongozi wa upinzania Freeman Mbowe amefikishwa Mahakamani, amefunguliwa mashataka ya Ugaidi, wananchi wake wanasema mashtaka haya yamechochewa kisiasa

Rais Samia: Mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa kwasababu navyojua Mbowe alifunguliwa Kesi mwezi wa Tisa mwaka jana (2020), kwa hiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi. Nadhani wenziwe kesi zao zimesikilizwa na wengine wameshapewa sentence zao wanatumikia. Yeye (Mbowe) upelelezi ulikuwa haujeisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea so amekwenda amefanya tumeingia kwenye uchaguzi, amemaliza uchaguzi nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao, wamemuhitaji waendelee na kazi yao, Lakini kwasababu na kama utakumbuka Mbowe hakuwepo nchini alikuwa Nairobi, sasa kwanini kakimbia sijui. Lakini alivyoingia tu nchini Kaitisha maandamano ya Katiba na madai ya katiba. Nadhani ni Calculation akijua kwamba ana kesi ya aina hiyo na hii vurugu ambayo ana-instigate akikamatwa aseme mmhh! kwasababu ya Katiba, kwasababu tumeitisha Katiba... nadhani sina hakika.

Lakini kwasababu jambo liko mahakamani, sina uhuru wa kulizungumzia kwa sana. Nadhani tuache Mahakama zioneshe ulimwengu kwamba hizo shutuma walizomshutumu zilikuwa za kweli au siyo za kweli Mahakama itaamua.
Nchi hii kamwe hatuwezi kuvumilia chokochoko ya uvunjifu wa amani ,amani ni tunu tuliorithishwa tutailinda kwa gharama yoyote .Uzalendo kwanza
 
Nchi hii kamwe hatuwezi kuvumilia chokochoko ya uvunjifu wa amani ,amani ni tunu tuliorithishwa tutailinda kwa gharama yoyote .Uzalendo kwanza
Mbona zinavunjwa wazi wazi na hakuna wa kuilinda?
 
Nimemsikiliza huyu mama na kweli amesema hivi. Na mimi pia nimemshangaa sana...

Kwanza alitaka kukwepa kulijibu swali hilo kwa kuwa liko mahakamani...

Lakini ghafla akajikuta anaanza kutoa maelezo ya kile kilichokuwa ndani ya moyo wake na kujikuta anatoa pre judgement ya mahakama...

Kama IGP Simon Sirro, huyu mama naye akajikuta anasema:

"....Mbowe alikuwa anajua ana kesi. Lakini alikuwa amejificha Nairobi Kenya. Aliporudi na kutoka huko alikokuwa amejificha Nairobi Kenya na akafikia ku - instigate fujo za maandamano ya kisiasa hapa nchini ili akikamatwa waseme amematwa ili kuzuiwa kufanya kazi zao kisiasa. Kwa hiyo hayo madai yao siyo kweli...."

Sasa ni wazi kabisa, ugaidi wa Mbowe ni ishu ya kubumba 100%. Lakini kosa la huyu kamanda ni kuongoza madai ya katiba mpya ya wananchi ambayo kwa tafsiri ya watawala ni "...kui - instigate fujo za kisiasa..."

The true colour of this woman has been revealed....
tulieni tuliii,nyumbu nyie,tatizo lenu poor thinking carpercity! yaani kila mda mko nyuma ya muda[emoji23][emoji23][emoji23].tatizo mlimuona ni mama Basi mtamgeuza mnavyotaka.kwa ninavyoona mbowe amecheza kalata chafu,hachomoki mtaniambia!
 
Mama anafungua nchi!

Mama anarudisha hela mtaani ili sisi mibavicha tuwe tunaziokota

Mama anaupiga mwingi sana! Uchumi uko juu, mafuta bei chini, bidhaa bei chini.

Mama anawakomesha mataga, sukuma gng na kufuta legacy.

Bashiru na Polepole wanakiona cha moto.
Mwendazake kichaa Kwisha habari yake
Mama naye atapotea tu muda ukifika
 
Hiyo kesi ilikuwepo tokea siku ya matokeo kutangazwa eti walipanga kulipua vituo ghafla akaachiwa yeye na Boniface Jacob!! Eti leo ndio ushahidi unapatikana baada ya kudai katiba??

Btw Mbowe alikua Kenya na kina Mudavadi na Lissu na ile convention ilikua public kabisa na akarejea bongo. Sasa kujificha huko ndio vipi?? Alishiriki chadema dijitali mwezi mzima.... Akaenda kanda zote.... Kaenda kwa mazishi.... Kahudhuria kongamano la katiba ndio eti alikua anajificha??

Huyu mama ni shetani na anguko lake linakaribia
Sipingi mtazamo wako mkuu, ndiomaana kwenye comment yangu nimesema kuna uwezekano(inawezekana) Mbowe asiwe gaidi kama jinsi anavyotuhumiwa.

Nilikuwa napinga hoja ya niliemquote,aliosema kuwa Mbowe hakuwa Kenya anasingiziwa.
 
Yule mama hatari sana
Polisi na CCM huwa wanasaidiana kufichiana aibu. hii kauli ya Samia na ile ya Sirro ukiangalia kwa makini utaona wote wana mtazamo unaofanana.

Kama Mbowe alijificha Nairobi waliwahi kusema? kuna Interpol kwanini hawakutangaza ili wasaidiwe kumtafuta?

Nashawishika kuamini Rais ameongea uongo, analeta propaganda kwenye haki za binadamu, kusema Mbowe alijificha Nairobi wakati muda wote alikuwa Dsm na Moshi kumzika ndugu yake ni maneno ya kisiasa tu.
 
Yaani mtu kwenda kupumzika wewe jinga unasema kakimbia?
Kwani Mbowe ni mara ya kwanza kwenda Kenya au nje ya nchi na mara zote hizo huwa anakimbia kesi?? Kwa ushirikiano uliopo kati ya Tz na Kenya mbona ni rahisi sana kumkamata gaidi au mtuhumiwa yeyote anayehitajika pindi awapo Kenya.
Ni akili za ajabu sana hizi.Tumieni ubongo kufiki na sio kiungo kingine.!!
Kwanza sijaku-quote wewe, ila nashangaa umeijibu hoja yangu kwa Matusi.

Haya basi umenitukana kuwa mimi ni mjinga, wewe mwenye akili zitumie kumtoa Freeman Mbowe huko aliko.
 
Kwa mahojiano ya leo na BBC natafakari inawezekana vipi Ndugu DPP kusema "hana nia ya kuendelea na kesi"..??

Natafakari pia ni Jaji yupi anayeweza kusema Ndugu.Mbowe hana hatia hivyo Mahakama inamuachia huru..
 
Mbona ninyi mmeshamtoa mdisi na kusema kesi ni ya kubambikiwa? Kwani huko siyo kuhukumu?
 
Hiyo kesi ilikuwepo tokea siku ya matokeo kutangazwa eti walipanga kulipua vituo ghafla akaachiwa yeye na Boniface Jacob!! Eti leo ndio ushahidi unapatikana baada ya kudai katiba?...
Mkuu zitto junior hoja zako zinafikirisha isipokuwa hitimisho lako hili Huyu mama ni shetani na anguko lake linakaribia limeharibu uzito wake.

Aliyeyasema hayo, tena hadharani, ni Rais wa JMT anayepata habari nyingi kuliko mimi na wewe humu JF. Tusubiri yatakayojiri kesi itakapoanza kusikilizwa
 
Back
Top Bottom