Punguza hasira na stress. Tatizo lako unaiogopa CCM na kuiambia ukweli unaona uwashtumu wapinzani ambao hawapo bungeni, Wala hawana jeshi, au TISS. Yani unawastumu wapinzani kwa lipi?. Nchi hii imeongozwa na TANU na CCM mpaka Leo, lakini kwa unafiki wako unaona wanaonstahili kulaumiwa ni wapinzani.
Punguza unafiki, unaona fahari kuwashtumu wapinzani na kuwalamba miguu CCM wenye mamlaka ndani ya bunge, kwenye Halmashauri zote, kwenye Dola na Taasisi zote. Unawalaumu wapinzani kwa lipi?. Kwa sababu serikali imetoa kibali Cha uwindaji hivyo tuwalaumu wapinzani kwa Nini hawakuzuia hicho kibali. Be serious na upunguze makasiriko kwa watu wasiofaa.
Pia unadai Upinzani wanahangaika na katiba mpya ili wapate madaraka. Kwanza nikuulize unajua lengo la chama Cha siasa?. Lengo la chama Cha siasa ni kushuka madaraka, ulitaka wafanyeje kuliko kuhangaika na lengo kuu. Pia, katiba mpya hawapewi wapinzani pekee bali wananchi wote. Kwa hivyo wapinzani wataangalia maslahi yao, wafanyakazi wataangalia maslahi yao etc, hivyo isiwe mbinafsi.
Mwisho, wapinzani unawalaumu humu wamepita changamoto nyingi, wameibiwa kura, wamepigwa risasi, wameharibiwa biashara zao, wengine waliopewa kesi za ugaidi rwakatare na Mbowe, wengine wamepotezwa na kuawa kabisa. Sasa nikuulize wewe unacho walaumu hawajafanya ni kipi?. Akina hans pope walitaka kupindua nchi mliwafanyaje zaidi ya kuwadhihaki. Akina Mbowe walipewa kesi za ugaidi mkamtukana mpaka mkachoka, alipokaa kimya klmkaanza kudai amelemba asali, Lissu kalimwa risasi Leo anadhihakiwa na kutukanwa na wengine kumwita mlemavu. Mkiambiwa muandamane kuupinga Jambo Fulani mnajificha ndani , ila mmekaa kuropoka hakuna upinzani. Punguza unafiki.