Rais Samia: Mgao wa maji unatokana na ubishi na ukaidi wa binadamu pia na kudra za mwenyezi Mungu

Rais Samia: Mgao wa maji unatokana na ubishi na ukaidi wa binadamu pia na kudra za mwenyezi Mungu

Janga gani na wewe? Yaani huoni haya mabadiliko ya tabia ya nchi? Joto kali sana na maeneo mengine kama Morogoro mvua haijanyesha kabisa, na hii ni November inaenda mwishoni. Yeye afanyeje kama maji yamepungua kutokana na sababu hizo? Kazi tu kukariri corus bila ya kufanya tafakari.
Kwahiyo hapo wewe ndo umejiona umetafakari saana sivyo!!?
Aah am sorry mkuu, Kumbe janga sio Rais pekee.🚶🚶
 
Hii ni moja ya ID za kimkakati
Hakuna cha mkakati wala nini. Penye ukweli acha usemwe na si kumlaumu mtu kwa vitu vilivyo juu ya uwezo wake. Ungekuwa na hoja ya maana kama ungehoji juu ya mipango ya sasa kwenda mbele katika hali hii ya mabadiliko ya tabia ya nchi ningekuelewa.
 
Kwahiyo hapo wewe ndo umejiona umetafakari saana sivyo !!?
Aah am sorry mkuu, Kumbe janga sio rais pekee.🚶🚶
Ndiyo mkuu. Acha kuwa mwepesi wa kulaumu bila kufanya analysis ya hali halisi.
 
Aisee wewe jamaa wa ajabu sana. Kwa hiyo ulitegemea Mama Samia awe amefikisha maji ya ziwa victoria Dar na maeneo mengine ndani ya kipindi kifupi alichoshika madaraka? Mbona walaumu bila kuwa na sababu za msingi? Au ni chuki zako tu kwake? Au hujui pia mabadiliko ya tabia ya nchi yaweza kusababisha hata kina cha maji ya ziwa kupungua sana na kuicha mitambo ya kutape maji ikielea tu?
Wewe ndo wa ajabu kuliko Huyo unayemuona wa ajabu. Mwanza na Shinyanga kuna mgao, nako wanategemea maji ya mito?
 
Ukisikia ng'ombe wa maskini hazai ndio kama haya tunayoyaona kipindi hiki. Aibu tupu.
 
Aisee wewe jamaa wa ajabu sana. Kwa hiyo ulitegemea Mama Samia awe amefikisha maji ya ziwa victoria Dar na maeneo mengine ndani ya kipindi kifupi alichoshika madaraka? Mbona walaumu bila kuwa na sababu za msingi? Au ni chuki zako tu kwake? Au hujui pia mabadiliko ya tabia ya nchi yaweza kusababisha hata kina cha maji ya ziwa kupungua sana na kuicha mitambo ya kutape maji ikielea tu?
Soma tena ulichoandika na ulinganishe nilichokuuliza.....
Ngoja nibadilishe swali ili unielewe
Dar wanategemea mto Ruvu, mto Ruvu maji yamepungua. Nakubaliana na mgao.
Mikoa ya Kanda ya ziwa wanategemea maji ya mradi wa ziwa Victoria, mradi ulishaisha na maji yalishaanza kutoka. Ila Sasa hivi hayatoki. Ndio nikakuuliza huko napo sababu ni nini?
 
Dar es Salaam kuna mgao mkubwa wa maji kwa sababu mto Ruvu umevamiwa na binadamu na kuchepusha maji.

Pili maelfu ya mifugo yanayoingizwa kwenye mito kunywa maji yamepunguza kiasi cha maji
Naagiza Wakuu wote wa mikoa kuweka ulinzi katika mito yote ili kulinda maji ya watu wetu……… waagize wakasimamie upandaji wa miti kwenye vyanzo vya maji badala ya kwenda kulinda mito tu.
 
Vipi huko mama leo hajazungumzia tena kuhusu mambo ya wanaume kuchangia mbegu...😃😃🙈🙈
 
Mvua zinanyesha Mwanza muda huu😍
Dar es salaam kuna mgao mkubwa wa maji kwa sababu mto Ruvu umevamiwa na binadamu na kuchepusha maji.

Pili maelfu ya mifugo yanayoingizwa kwenye mito kunywa maji yamepunguza kiasi cha maji kwani ng'ombe mmoja kwa mfano hunywa lita 40 za maji kwa siku.
 
Kwahiyo hao watu wamevamia Magu alipofariki au?
Huyo Magu wako Nani katika hii Nchi??! Kama alikuwa jabali mbona hakugoma kutolewa roho na malaika wa mahuti? Yaani kila kitu, eti mbona kipindi mungu Magu haikuwa hivi, huko TBC mmesikia ubazirifu wa mabilioni ya Fedha,Tena kipindi Cha huyohuyo mtu wenu

Acheni kumuabudu huyo mungu wenu,

Rais Samia ameongea vizur Sana,kuwa mengine ni kudra za Mungu, na pia Kuna uvamizi wa vyanzo vya maji
 
Back
Top Bottom