Kuna watu may be umri wao mdogo, ama wajinga au wapo kwny Propaganda
Makanisa mara zote huwa wanatoa matamko makali sana ma Rais wa Nchi wanapokuwa sio watu wa dini yao baada ya muda maisha yanaendelea kama kawaida
kwa waliopevuka kiakili baada ya uchaguzi wa 2010 may be naweza kuwajulisha kuwa Kanisa lilitembea bega kwa bega na Katibu wao wa zamani Wilbroad Slaa kuhakikisha wanamuangusha Rais Jakaya Kikwete
Walitoa Waraka nyakati za Kampeni kutaka Wakristo wote wachague Mgombea Mchamungu ( Dr Slaa) lakini kama ilivyo kawaida yetu Raia wa kawaida…tunawasikiliza Viongozi wetu wachochezi, tunawashangilia lakini ikifika wakati wa Maamuzi huwa tunaamua kwa Maslahi ya Nchi yetu
Waraka umesomwa utajadiliwa na utakuwa talk of the town kwa wiki kadhaa baada ya hapo Maisha yataendelea kama kawaida.
kama kuna Mtu ana rekodi ingependeza sana angetuwekea ma nyaraka kadhaa yanayotolewa na kanisa yaliwahi kumtisha Rais gani wa Nchi hii?
Tena kile ki Mzee Mwinyi ndio Hatare kabisa …anawasikiliza mnavyomtukana vyema sana na hata ikibidi anaweza akawaomba radhi lakini akitoka hapo anaendelea na mambo yake kama kawaida
Alimfanyia hivyo Nyerere kwny kufuta Azimio la Arusha na kuruhusu Uhuru wa watu kujieleza …kanisa nalo likamsakama sana lakini aliwaheshimu sana lakini hakuruhusu wachezee Mamlaka yake ya ki dola, the same to Mwana kijiji mwenzangu wa Msoga …tena mnakutana kwny Vikao mnampangia mikakati, kabla ya kutoa press release ya Waraka tayari yeye ana nakala kupitia Wandani wake waliopo Kanisani
Dola inazijua sana Taasisi za kidini pamoja na mapungufu yake, hayati JPM alipoanzisha heka heka ya vyeti feki na kukagua Fedha za Serikal kila eneo ikiwemo zinazokwenda kwny Taasisi za Kidini alikutana na Madudu mengi sana hadi Yule Sister Mkuu wa Idara ya Fedha na Bajeti wa pale Bugando alijirusha kutoka ghorofani na kufariki papo hapo
Wadanganyeni usafi wenu Waumini ila dola inawajua vizuri sana