Rais Samia mgeni rasmi Simba Day, Agosti 6, 2023

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187


Karibu kwenye kilele cha Wiki ya Simba.

Karibu kwenye Simba Day, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hii ni siku muhimu kwa Klabu ya Simba na wapenda michezo wote nchini Tanzania.

Tunakushukuru na tanakukaribisha kwa furaha kubwa isiyo na kifani. Kwa kipekee kabisa, tunakushukuru sana kwa mchango wako mkubwa kwenye sekta ya Michezo na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Karibu sana Mheshimiwa Rais.
 
Anenda kuwapa moyo tu uyo ni Mwananchi ...
 
Nilijua tu Alikiba Kaenda Simba na Alikiba kwa wasanii ndio Kipenzi cha Mama basi Na Mama atapenda awepo.

Mama anampenda Alikiba sana na amekubali na anakuja kwa Ajili ya Alikiba sio Simba.

Mimi mshabiki kindakikandi wa Yanga, ila bila simba hakuna Yanga imara, napenda uimara wa Simba ili kuwe na ushindani.

Hili ni jambo jema sana, na hongereni watani zetu, rais ni wa wote, ni wakati wenu na nyie kumfurahia rais wetu kwenye matukio yenu.
 
Mh. Rais akija kwenye mechi za Yanga, Yanga huitwa ni timu ya CCM. Sasa Rais anakuja kwenye mechi ya Simba, tuambieni ni lini Simba nao walichukua kadi ya uanachama wa CCM.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Vitu vingine visikuzidishie mapigo ya moyo.
Simba,Yanga,KMC,Namungo,Ruvu shooting n,k zote kuna mikono wa serikali.
 
Safi sana ,nimependa hii angle ya kumpa Mama nafasi ya mgeni rasmi, akili imetumika bien hapa , itamsaidia mama sana
 
Mh. Rais akija kwenye mechi za Yanga, Yanga huitwa ni timu ya CCM. Sasa Rais anakuja kwenye mechi ya Simba, tuambieni ni lini Simba nao walichukua kadi ya uanachama wa CCM.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Hujaelewa, Samia akienda Yanga amekwenda kama mwenyekiti wa CCM na ndio maana hata bendera za CCM uliziona.
Lakini Samia kwenye sherehe hii ya Simba day anakwenda kama Rais ndio maana hutaiona bendera ya CCM uwanjani.
 
Mkataba wa bandari vipi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…