Kaka hujaelewa bado? Virusi vinaua kwanza wazee, pili watu wengine wenye udhaifu kutokana na magonjwa au menginevyo.
Kote Afrika hadi sasa vifo vimekuwa vichache kwa sababu
1) wazee ni wachache, vijana ni wengi
2) watu wengi bado wako vijijini, hivyo hawasafiri sana, hawakutani na watu wengi sana, virusi huwa na nafasi ndogi kusambaa
3. watu wengi, hata Dar es Salaam, wanaishi hewani wazi, yaani hawana makazi ambako madirisha ya kioo yamefungwa (kule Ulaya hata masoko mara nyingi yamo ndani ya ukumbi)
Haidhuru kama ni Mzungu au Mwafrika. Umri, kiasi cha kuwa karibu na watu wengi na muda wa kukaa ndani ya vyumba vilivyofungwa ni sababu ya kuwa na maabukizi mengi au machache.
Kwa hiyo kwa chi kama Tanzania ni rahisi zaidi kuepukana na wimbi kubwa kama Ulaya. Ila tu wale wanaojitahidi wataambukizwa, wakiwa vijana labda bila dalili, lakini hata hao vijana wanaweza kuambukiza wengine, na hapo unaona hasa wazee na wenye magonjwa mbalimbali wanaathirika vibaya hadi kufa.
Na asilimia ndogo ya vijana wanaathirika pia;
ila tu, ukijua hisabati: Asilimia ndogo ya watu wengi = idadi kubwa kiasi.