Nyie ndio kila kitu unachokisoma kwenye elimu ya kikoloni kuhusu Afrika unakibeba hook, line and sinker? Eti Ulaya na Marekani wamekufa wazee wengi na Afrika hatujafa kivile kwa sababu tuna idadi kubwa ya vijana? ...
Kaka nilikuomba utumie mantiki ya wastani.
*Nilieleza kwa sababu gani watu wa Afrika hawaathiriki vibaya kama watu wa Ulaya, unajibu ni "elimu ya kikoloni"
* unaeleza "mainstream media" wanasema Afrika ni tatizo kubwa la Corona.
Ipi sasa??? Ama propaganda ya kaskazini inasema Afrika ina faida kwa sababu ina vijana wengi sana kuliko Ulaya (ambayo huwezi kupinga) AU propaganda ya kaskazini inasema Afrika ni tatizo kubwa ya Corona?
Kuhusu lifestyle nakubali kiasi. Kama Wamarekani weusi, pia Malatino wanakufa wengi kuliko Wamarekani weupe ina uhusiano na lifestyle yaani makazi, kazi na chakula (ingawa hapa hujalenga). Maana si swali la rangi lakini swali la umaskini, na pamoja na matajiri kama Obama n.k. asilimia ya weusi kati ya maskini wa Marekani ni kubwa kuliko asilimia yao kati ya wananchi wote.
Watu maskini wanaishi kwenye nafasi ndogo wanapobanana zaidi, tena huko katika nyumba zilizofungwa kabisa (tofauti na hapa Dar, wengi hatuna madirisha ya kioo) ambako virusi vina nafasi nzuri kubaki hewani, tena wanafanya kazi ya moja-kwa -moja kama wauzaji madukani, kupeleka barua an vifurushi kwenye nyumba za watu, ilhali idadi ya hao wanaoweza kufanya home-office kupitia kompyuta ni ndogo kuliko wastani. Yote nafasi ya kuambukizwa zaidi.
Pamoja na chakula cha maskini (lifestyle!) maana huko watu maskini wanakula zaidi fast-food kuliko watu wenye pesa, kwa hiyo watu maskini wako wanene kuliko watu wa wastani (tofauti hapa TZ), hivyo wanaathiriwa zaidi na usukari (soma:
Factors contributing to higher incidence of diabetes for black Americans), hivyo wakiambukizwa na Covid wako hatarini zaidi.