Rais Samia mpandishe cheo Kanali Benard Paul Mlunga

Rais Samia mpandishe cheo Kanali Benard Paul Mlunga

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Aliyekuwa mpambe wa wa Rais Magufuli, Kanali Benard Paul Mlunga akimsikiliza Brigedia Jenerali Ibuge (hayupo pichani) ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa.

Kanali Mlunga alijipatia umaarufu enzi ya hayati Magufuli kea uchapaji wake kazi uliotukuka.

Nilijua alishapanda cheo kumbe amebakia kuwa Kanali. Rais Samia mpandishe cheo kama ulivyofanya kwa ADC wako wa sasa Brigedia Jenerali Mashauri
IMG_4251.jpeg


Soma pia: Rais Samia ampandisha cheo mpambe wake (ADC) sasa ni Brigedia Jenerali
 
Inshort wale waliokua karibu sana na JPM nilijikuta nawapenda sana kwasababu walikua wanamuhudumia rais wangu kipenzi. Walinzi wote, mpambe, dereva na hata walinzi wa mama Janeth, hii post imenisononesha mpaka nimemkumbuka JPM wangu ingawa kilasiku ni lazima niwaangalie YouTube

..vipi waliokuwa kwenye genge lake la watekaji, na wauwaji? Nao unawaonea huruma kwa kuondokewa na Sponsor wao?
 
Acha kukariri wewe mimi nilifikiri ni suala la kisheria kumbe ni desturi.

..Maofisa wa jeshi kuanzia ngazi ya Brigedia Jenerali wanatakiwa kuwa na wasaidizi wa kijeshi / wapambe.

..sasa yule Mpambe wa Raisi ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali naye anatakiwa awe na mpambe.

..hiyo ndio mantiki ya BigBro kushauri afisa mwingine wa jeshi ambaye hajafika ngazi ya Jenerali ateuliwe kuwa mpambe.

.
 
Namjua na issue yake naijua ila sina ushahidi wowote wa aliyemfanyia hivyo


..unafahamu eneo aliposhambuliwa ni la makazi ya viongozi wa bunge na serikali?

..hufahamu kwamba maeneo ya aina hiyo hupatiwa walinzi wa serikali?

..yeye Lissu ambaye ni mhanga, na shahidi namba moja wa tukio, amesisitiza kwamba walinzi wa eneo hilo waliondolewa siku aliposhambuliwa.

..Je, unadhani inawezekana mtu aliye nje ya mifumo ya ulinzi wa maeneo ya serikali, angeweza kuwaondoa walinzi ili washambuliaji wapate fursa ya kumdhuru Tundu Lissu?

..huoni kwamba mazingira hayo, ukichanganya na Polisi kutofanya juhudi za kuchunguza, ni kiashiria kwamba jaribio la kumuua Tundu Lissu lilikuwa na baraka za watu wakubwa serikalini?
 
..Maofisa wa jeshi kuanzia ngazi ya Brigedia Jenerali wanatakiwa kuwa na wasaidizi wa kijeshi / wapambe.

..sasa yule Mpambe wa Raisi ambaye amepandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali naye anatakiwa awe na mpambe.

..hiyo ndio mantiki ya BigBro kushauri afisa mwingine wa jeshi ambaye hajafika ngazi ya Jenerali ateuliwe kuwa mpambe.

.
Hao unaosema ni wale ambao wapo makambini au kwenye vikosi lakini huyu mpambe wa Rais yeye yupo kazi maalum
Vilevile, sio kila Brigedia General ni lazima awe na mpambe kama unafika ofisini na kusoma magazeti na kuondoka mpambe wa nini? inategemea na majukumu aliyokuwa nayo mfano Mkuu wa operation na mafunzo, Mkuu wa Brigedi nk. Maana hata kanali anaweza kupewa Mpambe inategemea na majukumu ya Idara aliyopewa kwa wakati huo.
 
Tatizo la samia hajielewi,anatoa vyeo kwa watu wake wa karibu tu.mfano juzi kati nimeona kampandisha cheo yule mama mkuu wa misafara yake kuwa SACP wakati yule mama anatakiwa kustaafu.
 
Magufuli alikuwa anapandisha vyeo hovyo hovyo, unaweza kukuta huyu alimtoa kwenye u-Saa-Meja. Pengine kijeshi ndio inagoma kumpandisha mpaka aende kozi kadhaa
unajua mambo ya jeshi kiongozi?yaani saa meja,apande cheo aende wapi?saa meja 2(WO2),akipanda anakuwa WO 1,hapo ndo mwisho kwa vyeo vya maaskari wa chini.
 
Back
Top Bottom