Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

Rais Samia: Msikubali wanaotaka kuanzisha chokochoko, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani

1. Viongozi wa taasisi nyeti wote, rais anateuwa. Matokeo yake hawatendi kwa haki au Sheria bali atakavo rais!!!!

2. Ukistaafu, ccm wamehodhi mpaka mafao uzeeni, mtu hupati haki yako mpaka ufe, eti, Akiba uzeeni utachukuwa ufikapo 60....65, kazi umekatizwa at 40yrs!!!!

3. Wabunge wanalipana mamilion, majimboni hawapo, na hawaendi

A) kupitisha makodi yasiyoeleweka bungeni
B) kututungia sheria kandamizi..... mfano zakimtandao nk

4. Katiba mbovu ilimruhusu pombe, kuzuwia mishahara na madaraja kazini ya watu wasipandishiwe kibabe miaka-5, bila kujali inflation wala katiba inasemaje

5. Watu walipotezwa, kila kona, ilikuwa sawa tu..... sababu katiba inamfanya rais wa Tz kama Mungu

6. Wakulima wanadhibitiwa na kunyimwa uhuru wa mazao yao kuyauza watakavyo. Mfano korosho huko mtwara na mahindi ruvuma

Mlolongo ni mrefu sana wa kiunyanyasaji, wachangiaje tuacha mahaba hebu tupingane kwa hoja.

Katiba mpya inaweza kupunguza baadhi ya hizi kero, bila kusahau kubambikiana kesi, watu kuwekwa vizuizini muda mrefu bila kufikishwa mahakamani, utesaji, nk
Sasa hivi wala hatuhangaiki na kuwafahamisha tena. Nyinyi si mnajifanya hamna akili mandezi?? Mtapelekwa hivyo hivyo kindezindezi.

Yaani kwa upole, upendo na busara tele Mheshimiwa rais anawaambia suala la katiba nipeni muda kidogo, maana yake anajua kwamba linahitajika halafu nyinyi mnaanza kumtukana na kumtolea maneno yenu ya kifedhuli yasiyo na Staha eti tutamlazimisha!!!! Haya mlazimisheni sasa.
 
Bavicha ndio wanaotaka kuleta vita, lala nao mbele hao hawana maana
Niki unawashwa sana wewe, nakushauri tulia hapo Kisarawe, wewe tokea Carbood akugongee umekuwa Pimbi sana
 
Nawe unajiona una akili kwa comment uliyotoa hapo juu? Kwamba taharuki hata kama ni za kisheria ni taharuki?
Taharuki ni taharuki tu.

Iwe ya kijamii, kisiasa, kizalendo, kidini, sijui ki nini zote ni taharuki tu na ndani ya nchi hii hatuzitaki.
 
Tunahitaji katiba mpya, siyo ombi bali ni hitaji la Taifa. Tume ya Warioba, kwa ushahidi, ilithibitodha kuwa Watanzania wanataka katba mpya.

Waleta chokochoko na wasiolitakia mema Taifa letu ni wale wasiotaka kutekeleza hitaji la wananchi
Kama wao hawataki kutekeleza si mtekeleze wenyewe.

Kama mnahitaji katiba mpya kwa namna mnavyotaka nyinyi njia nyeupe si mkae ndani muitunge halafu muanze kuitumia?? Shida iko wapi??
 
Wewe utamfanya nini huyo keshakuwa rais ndugu yangu,hivyo vyama sijui CCM sijui Chadema ni upuuzi mtupu africa kuna demokrasia?nakushauri weka nguvu kwenye kazi zako tu achana na mambo hayo au kwa vile upo nyuma ya keybord?bora uwe unaandika humu humu usije kuingia kwenye magenge ya vyama hivyo ndugu ukahatarisha uhai wako au viungo vyako hao wote wapo kimaslahi yao.Saka pesa.
Akijifanya mbishi muache aingie barabarani hahahaahah
 
Sasa hivi wala hatuhangaiki na kuwafahamisha tena. Nyinyi si mnajifanya hamna akili mandezi?? Mtapelekwa hivyo hivyo kindezindezi.

Yaani kwa upole, upendo na busara tele Mheshimiwa rais anawaambia suala la katiba nipeni muda kidogo, maana yake anajua kwamba linahitajika halafu nyinyi mnaanza kumtukana na kumtolea maneno yenu ya kifedhuli yasiyo na Staha eti tutamlazimisha!!!! Haya mlazimisheni sasa.
Hivi , Nyie mwajiona mna nguvu Sana mbele ya wananchi kisa , vyombo vya dola, mabunduki, na magereza, KWA sababu ya kujitia upofu kisa utam wa keki ya taifa umewakolea

Ipo nguvu ndani ya wananchi inayoonekana na isiyo onekana, kwamba hata mtumie vifaru, dola, n.k hamwezi shinda nguvu hiyo, ni HAKI kwenye taifa Ndo itashinda sio Ubabe, vinginevyo endelea tuone mwisho wake ,

Watu wanataka katiba mpya, mnasema chokochoko, mikutano ya adhara ya vyama vya Siasa, nayo mwasema nini vile,?

Twende tu
 
Rais Samia amewataka wananchi wa Morogoro wasikubali chokochoko zinazoanzishwa na baadhi ya watu.

Amesema hao wanaotaka kuanzisha vurugu wameshaandaa na wanajua watakavyojitibia ikitokea wamepata madhara.

Amewataka wananchi kutokubali na kutunza amani iliyopo. Amesema hayo akiwa Morogoro kwa ziara ya siku mbili.

NB: Possibly Rais anawaasa wanaotaka katiba mpya.



===

Rais Samia: Niwaombe sana tulinde amani, vijichokochoko vimeanza naomba msivipokee, wanaokuja na vijichokochoko walishajua matumbo yao yanajaaje, chakula chao wanatoa wapi, pesa za matibabu watatoa wapi, nawaomba wasije wakawaingiza kwenye huo mkenge”

Rais Samia: “Pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani na Watoto wako na Mama Watoto na msijue chakula mnatoa wapi, msijue Mtoto akiumwa mtakwenda kumtibu na pesa gani, niwaombe sana tulinde amani yetu, Nchi yetu itulie tuendelee na maendeleo yetu

Sisi raia werevu tunalijua hili Mama usihofu
 
Kwahiyo Uhuru mnaoutaka ni wakina Mdude kuporomosha matusi??
Hakuna njia nzuri za kudai haki zao pasi na kuporomosha matusi?

Muacheni mama achape kazi,msitake kumpelekesha,,ana ratiba zake na vipaumbele..
Mbona mnataka kumpelekesha wakati alishasema mumpe muda!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wanajifanya wehu hawa.

Dawa yao ni kwenda nao hivyo hivyo kiwehu wehu.

Yaani mama aache kushughulikia Watanzania wote wapate umeme aanze kushughulikia matakwa yao wao. Ikifika 2025 waanze kumuuliza mbona umeme hakuna????

Tutakwenda nao wanavyotaka wao
 
Hivi , Nyie mwajiona mna nguvu Sana mbele ya wananchi kisa , vyombo vya dola, mabunduki, na magereza, KWA sababu ya kujitia upofu kisa utam wa keki ya taifa umewakolea

Ipo nguvu ndani ya wananchi inayoonekana na isiyo onekana, kwamba hata mtumie vifaru, dola, n.k hamwezi shinda nguvu hiyo, ni HAKI kwenye taifa Ndo itashinda sio Ubabe, vinginevyo endelea tuone mwisho wake ,

Watu wanataka katiba mpya, mnasema chokochoko, mikutano ya adhara ya vyama vya Siasa, nayo mwasema nini vile,?

Twende tu
Wewe unaongea nini?? Sisi ndio hao wananchi sasa. Sisi wananchi hatutaki kuhadaliwa na Genge la wahuni wachache. Watoto wetu wanasoma bure kabisa na maisha yanakwenda. Leo mnataka tuwaruhusu kina mbowe waturubuni tuanze kudai vitu vya ajabu kwa maslahi yao ili wao tu waingie madarakani???

We are better than that ndugu yangu na wala hatutoingia huo mkenge
 
Yaliyomo kwenye ilani ndiyo yanayowahusu wananchi..


Kama mnadhani matusi yatawapa katiba mpya basi endeleeni kutukana.

Halafu kama nyie mashujaa jitoeni kimasomaso ingieni mtaani,,siyo mnaongea tu huku kwenye keyboard na I'd feki mmejificha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena yaliyomo kwenye ilani ndiyo yaliyotufanya sisi tukaichagua CCM. Tumeshamkumbusha Mama kwamba hatukukichagua chama chake ili kianze mambo yasiyo ya msingi. Tumekichagua ili kitekeleze waliyotuahidi kupitia ilani.

Ni imani yetu kuwa imani itatekelezwa na hizi kelele za hawa wahuni zitapuuzwa
 
Kudai katiba mpya ni kutaka kuharibu amani ya nchi? Ni hivi, hiyo mama urais wake ni wa urithi, hivyo sitegemei aamue lolote tofauti na genge la yule kiongozi muovu kwani ndio linalomzunguka. Hivyo wanaodai katiba mpya wasiaachie, washikilie hapo hapo maana ni madai halali.
Wanaodai??? Wewe hudai mkuu?
 
Dawa ni kufuata sheria ili kuepuka hizo chokochoko, ila mkiwaumiza wanaoleta chokochoko wanaofuata sheria ili kudai haki zao mnawaonea, tumieni madaraka yenu vizuri kwa kuheshimu haki za wengine.
Wewe utakuwa sukumagang
 
Back
Top Bottom