Rais Samia "muondoe "Mwigulu wizara ya fedha..

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Kwanza kabisa masuala ya uchumi WA nchi hayapaswi kuwa chini ya mtu mmoja....zamani tulikuwa na Tume ya mipango ambayo waziri alikuwa sehemu ya tume hiyo...jopo la tume hiyo ndo lilikuwa linaendesha uchumi...

Mwigulu ana weakness ya kuongea Kwa kukera watu na ana history ya kutokuwa team player..
Je haya matozo anayoibuka nayo kutwa yamepitiwa na wataalam wote wa wizara husika?....

Nafikiri wakati sasa hiyo wizara ipate mtu mwingine na turudishe tume ya mipango ya Taifa ambayo waziri atakuwa anatekeleza Tu maagizo ya Tume na sio waziri kuwa ndo "muendeshaji mkuu"WA uchumi wa Taifa hasa Kama waziri huyo ana ajenda zake binafsi za kisiasa... Mwigulu atolewe hapo haraka...
 
Halafu amuweke nani na wakati yeye anatimiza matakwa ya aliyemuweka?
Nani atakuwa tayari kupingna na matakwa ya boss wake ili atumbuliwe??
Alishaawambia wachape kazi, wasisikilize maneno ya wanaowakosoa. (mwanangu mwigulu, mwanangu nape...) Na ndio maana akina Nape wanajibu wanavyojisikia.
 
Hakuna kitu chochote kikubwa (kama kuleta matozo) ambacho Mwigulu anaweza kukifanya bila baraka za kamati kuu ya CCM na ruhusa ya Mama Samia. Kifupi tu unapaswa ujue Mwigulu yupo tena yupo sana kwenye serikali. Why? Anatekeleza ilani!

Ni ukweli mchungu kwangu, kwako na mamilioni ya watanzania.
 
Watu wanajifanya kufumbia macho na kumlaumu waziri pekee.

Hizi tozo ujue zilijadiliwa na Baraza la mawaziri ambapo mwenyekiti ni raisi wa nchi na katibu wake ni katibu kiongozi.

Kwa nini asilaumiwe mwenyekiti ila mnamlaumu mjumbe ambaye kwa hapa ni waziri wa fedha.

Unafiki tu
 
Anzeni Kwanza Kumshtakia kwa Rais Mstaafu Kikwete ambaye ndiye anamlinda na kataka Mama ( Rais ) yenu amuweke hapo ili alinde Maslahi yake kupitia Kampuni ya GSM na Klabu yake pendwa ya Yanga huku Mwanae Ridhiwani nae akifanya mengineyo. Kifupi Mama ( Rais ) hawezi Kumtoa hapo kwani yuko Kimkakati zaidi hivyo mnapoteza tu muda wenu kila Siku kumuanzishia hapa Threads za Kumsakizia Rais amtumbue.
 
Sahihi kabisa, Mwigulu hawezi kuibuka na tozo hizo peke yake tu bila baraka za wakubwa wake, hivyo tatizo sio yeye binafsi.
Basi wajiuzulu wote TU hakuna namna Wala Nini! Nalo hilo wakalitizame upya!
 
Siyo atolewe tu , pia akamatwe kwa wizi wa Tozo za benki
 
Bajeti haiwezi pitishwa au pelekwa bungeni bila baraza la mawaziri kupata dondoo.
Rais ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo anajua kila kitu
Baraza lipi la Mawaziri , hili la akina Simbachawene ?
 
Mimi nadhani hali bado ni nzuri sana ikiwezekana waongeze tozo maradufu ndio Watanzania wataamka usingizini na kubaini kazi ya kutetea haki zao siyo ya vyama vya Siasa, au Mbowe, Lisu na Zitto Bali ni jukumu la wananchi wenyewe, na maandamano huwa hayaombwi Bali mnapoumizwa na jambo ni kuingia barabarani na wanasiasa mnawaweka pembeni.

Kunahitajika maandamano makubwa ya kiraia badala ya kugombea jezi za Simba na Yanga na upuuzi wa lete mzungu
 
Hapo amewekwa ajichafue ila akija kujitambua tayari keshachafuka Hui ndo ccm yangu.
Unatengenezewa mazingira kama unapendwa kumbe kuna team inakufuatilia ya kukusifia mwisho kwisha habari ktk yale mawe na madaraja yaliyoandikwa Mwigulu Rais.
Na huyu hana muda ataondolewa ni muda tu utasikia Kinana na Shaka wakiongelea swala tozo ndo utajua siasa ni mipango
 
Hivi huyu ana pesa gani mpaka amiliki timu ligi kuu? Au tozo zetu zinakwenda Singida big stars?
 
Unaamini zile tozo ni za Mwigulu na siyo huyo Mama. Kazi ipo.
 
Kama wewe unajua unadhani wao hawajui hilo? Nchi hii viongozi wana shida ya uongozi sababu ya pesa. Wapo pale kuchota pesa, mambo ya kesho wanamwachia Mungu.
 
Kunahitajika maandamano makubwa ya kiraia badala ya kugombea jezi za Simba na Yanga na upuuzi wa lete mzung
Hii ndio njia pekee ambayo kilio cha wananchi kingesika, maana mwananchi wa chini ndo anaumia.
Waangalie pia namna ya kupunguza matumizi ya viongozi huko juu, ikiwemo ununuaji wa magari ya kifahari
 
Kuna tatizo huko serikalini kwa sasa na Mwigulu ni sehemu ndogo tu ya hilo tatizo, na kwa mtazamo wangu, sasa nimeanza kuona chanzo cha hilo tatizo ni "soft treatment" plus "short sightedness" aliyonayo boss wao, sasa wameanza kujiamini wanafanya vile wanavyojisikia wakijua hakuna kitu kitakachowapata.

Unazungumzia kauli za Mwigulu kama ndio chanzo cha tatizo, vipi zile kauli za Nape na Makamba ambao nao kila wakiulizwa kuhusu mambo ya wizara zao [gharama za data na Nyerere Dam] wanatoa majibu ya hovyo kwa waowauliza?

Akifanya kama unavyotaka kumuondoa Mwigulu hapo alipo, basi tatizo litahamia mahala pengine either kwa Nape au Makamba, then tuanze kulalamika tena.

Tatizo letu serikali ya CCM imeshatufanya watu wa kuzoea matatizo mpaka sasa tumekubali matatizo hayo yawe sehemu ya maisha yetu, dawa ni kuifumua yote tuanze moja kama taifa, na hili halitafanywa na Mbowe wala Lissu, linatakiwa kuanzia kwetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…