Rais Samia "muondoe "Mwigulu wizara ya fedha..

Hivi kwanini awamu hii hua hatajwi moja kwa moja huyu Raisi kuhusika na haya yaendeleayo?Je ni mahaba ya watu kwake?au ni kitu gani!

Wengine wanaenda mbali sana kwa kusema eti anahujumiwa kua yeye hana macho wala masikio asisikie wala kuona sasa yuko hapo kufanya nini?Eleweni huyu mheshimiwa rais anajua,na amebariki unafikiri hakuwaambia hili la tozo nendeni mkalifanyie kazi kama mlivyonisimulia hapa.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Aondoke kabisa huyo mtu hafai.

Yaani kanifanya nimchukie hata Samia mwenyewe.

Inakuwaje watu tunalalamika maisha magumu, tunalipa kodi, halafu bado mnachomeka mikono yenu kwenye account zetu kuchukua visavings vyetu?

Mnyororo wa kodi kwenye visenti vyetu ni mrefu sana, humo ndani kuna double na triple taxation lakini huyu waziri wa fedha anajitapa eti kama hatutaki tozo twende Burundi.

Samia, ondoa huyo Mwigulu kabla hatujaanza kukuchukia zaidi au kukudharau!
 
Unafiki uliochanganyika na mahaba ndio tatizo la hao watu unaowazungumzia, wana tabia za kuchagua watu wa kuwalaumu kulingana na "vigezo" vyao walivyojiwekea, ukiwafuatilia kwa makini utagundua hivyo vigezo.
 
Reactions: nao
Mwigulu hajiamulii yeye kwanza ukiona kitu kama hiki kimepitishwa jua kilishapitishwa muda mrefu pia acha kulalamika kuusu Tozo, tozo ni kwaajili ya maendeleo yetu wenyew
 
Tozo ni kwa maendeleo yetu acha kulalamika na kujenga chuki
 
Likiwa nzuri la namba moja mabaya ya wasaidizi. Unlock your mind think properly.
 
Ili akuweke wewe au?

Kodi hamlipi sasa mtalipa kwa njia ya tozo na tafiti zinaonyesha hivyo 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220823-170206.png
    61 KB · Views: 4
Akikuelewa nitag
 
Mpango unapelekwa na waziri husika,baraza linajadiri.
 
Mpango unapelekwa na waziri husika,baraza linajadiri.
Hata kama Baraza la Mawaziri linakutana pendekezo linaletwa na waziri husika. Yeye ndiye mtaalamu katika mambo ya uchumi na itabidi atetee pendekezo lake kwa nguvu ya hoja.

Atatakiwa aeleze kwa ufasaha uhalali, lengo na faida ya pendekezo ili aungwe mokono. Kama utata wowote utatokea huko mbele ya safari wa kuwajibika ni yeye. Hivyo ndivyo ilivyo.

Hatakuwa wa kwanza kujiuzulu ama kutumbuliwa kwa kulipotosha baraza hilo na Mwenyekiti wake. Kikawaida inatakiwa achukuliwe hatua mapema kabisa kabla ya boti kuzama.

Hawezi kujificha nyuma ya baraza, ama ni yeye kama waziri au ni serikali nzima. Bosi wake akisita kumwajibisha basi naye asubiri kuwajibishwa na bosi mkubwa zaidi, WANANCH.
 
Hill ni jibu tosha. Maandamano ndiyo suluhisho la serikali na raia. Siku moja kazi inaisha na tutapata muafaka wa kupata katiba mpya.

Huu wizi wa tozo hhhhaukubaliki.
 
Mwigulu ni mnamuonea tu. Maamuzi ya tozo hayaanzii kwa Mwigulu na kuishia kwake. Lazima yawe na chimbuko pamoja na baraka za mwenye nchi.
Aliyekuwa anazunguka na bahasha ya kaki na madokezo ya tozo ni nani? Si waziri wa fedha?

Aliyeitisha hicho kikao ni nani? Lazima abebe lawama zote kwa kuidanganya serikali na raia wake. Angekuwa ni mwelewa angelifanyia utafiti kwa kushirikiana na wenye makampuni ya mitandao, taasisi za kiraia na mashirika yaliyokaribu na raia.

Angechukua majibu yao kwenye vikao vyao. Nadhani rais asingekubali kupitisha vikao viendelee kuhusu tozo.

Zungu mbabe kweli kamchomekea Nape tozo la bando. Kammaliza Mwingulu Sasa Nape.

Mtaalamu Nape vijana mavyuoni wanakusubiria kuhusu tozo ya bando.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…