Rais Samia muondoe ofisini haraka huyu jamaa wa EWURA

Shemeji anaondolewaje ?
 
EWURA hawahusiki na maswala ya tender za bulk procurement, hayo ni mamlaka ya PURA.

Issue ya kukosekana kwa dollar sio mpya labda limekuja public hivi sasa, waagizaji wa mafuta wana miezi kadhaa wanapata changamoto ya kupewa dollar wanazohitaji na kwa wakati sahihi kuagiza.

Bei mpya sio kukosekana kwa dollar tu, kuna tozo mpya pia bunge limepitisha kwenye budget iliyoisha ndio zimeingizwa kwa mara ya kwanza na bei ya mafuta imepanda katika soko la dunia japo kidogo sana.

Tatizo lilipo kwa sasa katika nchi lipo wazi tusisingizie watu wengine.
 
Mi nadharia yangu ni tofauti na hii yako.
Rais hawezi hata mara moja kumwogopa Makamba.

Nadharia yangu inajikita katika niliyoeleza hapo juu #6.

Ninayo picha nzuri sana juu ya jambo hili.
Hawapo timu moja.
Timu ya Makamba Jr ndio yenye nguvu saivi
 
Utajibiwa Kenya mafuta yalikopanda na dolari kuadimika, mkuu wa EWURA ya huko naye ni mume au mke wa Spika?

HOJA no 1, ibaki Bandari 🙏🙏🔥🔥
 
1. Katafute wanaounda hiyo Petroleum Bulk Procurement kama utamkosa EWURA.


2. Spika angeacha hoja ya Mbunge ifike mwisho kwa maslahi ya umma na Taifa.

3. Hiyo Tozo ya Bunge ni sh 100 tu, kubwa ni hiyo ujinga wao.
 
Jamaa abamchukulia Makamba jr. poa.
Kalamu anafikiria kanuni, za Rais hawezi kumuogopa mtu, anahisi ni tu ameamua kula pamoja nae.

Ikifika 2024 mwisho huko ndio ataelewa, kila timu inakusanya hela za maana.
Zingine hata mama hayumo, timu ni nyingi sana. Nchi ndio inaliwa.
 
1. Katafute wanaounda hiyo Petroleum Bulk Procurement kama utamkosa EWURA.


2. Spika angeacha hoja ya Mbunge ifike mwisho kwa maslahi ya umma na Taifa.

3. Hiyo Tozo ya Bunge ni sh 100 tu, kubwa ni hiyo ujinga wao.
Hakuna uhusiano wa PURA na EWURA

Bidding process ni open kila mtu anaona tender ya mwenzake.

Bei ya 400-toa Tozo 100-toa increase in exchange rate - toa increase in fuel prices.

Baada ya hapo zingatia watu wanaagiza less than usual kutokana na kukosa dollar, inaondoa economies of scale and profit margins. So ata bei ya kuuza nayo itakuwa kubwa.
 
Uache ubishi.
Uwe unapitia madesa ya hizi mamlaka ndio unakuja kubisha.

Wengine tunaandika kwa faida ya Taifa tu.

EWURA ndio msimamizi wa juu wa hiyo Agency ya kuagiza mafuta.

Sheria ninayo.

Ila kwa ufupi, pitia hizi


Hapa chini tena..



Mpaka hapo unaelewa nani anamsimamia mwingine.

NB: Ni PBRA, sio PURA kama ulivyoandika wewe.
 
Hii nchi imejaa aibu na ujinga mwingi sana.

Tuendelee kumuomba Mungu. Kila jambo lina majira na sababu zake
 
PURA ni agency wa kuagiza mafuta

EWURA anatajwa kama regulator (authority) jukumu lake ni kuhakiki kiwango cha mafuta yanayoagizwa na kutumiwa Tanzania. Lakini aihusiki na mchakato wa kuagiza mafuta.

Mafuta yana viwango tofauti, PURA wanahikikisha yanayouzwa Tanzania ni kwa viwango walivyoweka ndio maana huwa ata wanaweza vituo vya mafuta na kupima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…