Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Nimesikiliza hotuba ya Rais wetu leo kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani
Kwenye hotuba hiyo ambayo rais alikuwa katika mood ya kitofauti alisikika akiwaambia waandishi wa habari kuwa, 'ukinikuna nami nitakukuna, ila ukinikwaruza nitakuparura'
Kwa tafsiri rahisi ni kuwa anawaambia waandishi kuwa wakimuandika vizuri yeye pia atawapa favor, ila walimuandika vibaya watakiona cha mtema kuni
Hiki ni kitisho kwa waandishi kuandika habari zao kwa uhuru bila hofu ya kumkwaza Rais
Nadhani angewaasa kuandika habari kwa weledi zisizoegemea upande fulani, sio kumfurahisha