Rais Samia nakuomba lifumue jeshi la Uhamiaji na taasisi zake

Nani kasema asiyekuwa raia haruhusiwi kununuwa plot?
Kwa mujibu wa Sheria za Ardhi za Tanzania (Sheria Na. 4 & 5 za Mwaka 1999, Mtu ambaye siyo Raia wa Tanzania haruhusiwi kumiliki Ardhi nchini Tanzania isipokuwa kwa sababu za Matumizi ya Uwekezaji tu chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 1997.
 
Kwa kweli mambo ya aibu kabisa kuhusu hili swala la wachezaji , nchi inakuwa kichaka tu ukija unapewa tu uraia , huyu kesho ataomba ubunge au kazi nyeti halafu anatuuza maana kiukweli hana uchungu na nchi na tumeeuhusu wenyewe kwa ujinga wetu na tamaa zetu za muda mfupi
 
Jambo hili Lina madhara hasi zaidi kwa nchi kuliko faida.
Taasisi za Serikali ambazo zinapaswa kulaumiwa kwa kuliingiza Taifa kwenye majanga makubwa kutokana na kitendo cha kutoa kiholela Uraia wa Tanzania kwa wageni ni:-
1. Jeshi la Uhamiaji.
2. TISS.
3. Jeshi la Polisi.

Kuna hatari kubwa sana kutoa uraia kiholela kwa Watu wa nje. Hivi wanajua sababu mahsusi ambazo Rais wa Marekani Donald Trump katika awamu yake ya kwanza aliamua kuwapiga marufuku Raia wa Tanzania kupewa Viza au Uraia kwa njia ya GreenCard kwenye nchi hiyo? Wanazijua sababu zake?

Uhamiaji, TISS na Polisi wanajaribu kuweka rehani usalama wa umma wa waTanzania, ni hatari kubwa sana. Hivi ni kwa nini hasa Serikali ya Tanzania inakataa kuwaruhusu diaspora wa Tanzania kuwa na uraia pacha lakini wakati huo huo inaruhusu kiurahisi kabisa bila ya kufuata Sheria kuwapa uraia wageni ambao kamwe hawakuwahi kuwa na vinasaba kabisa na nchi ya Tanzania?
 
Inawezekana hao wachezaji ni wazuri sana kiasi ambacho wanastahili uraia haraka sana
 
Inawezekana hao wachezaji ni wazuri sana kiasi ambacho wanastahili uraia haraka sana
Wazuri kwenye Nini?
Kauli yako hii ni 'tungo tata.'

Usalama wa Umma kwanza, uzuri baadaye!
Public security must be given a top and the foremost priority.
Je, unakumbuka kwamba huko nje ya Tanzania ziliwahi kukamatwa Meli za mizigo zinazomilikiwa na mataifa ya nje lakini zilisajiliwa kiholela na Serikali yetu na meli hizo zilizopeperusha bendera ya Tanzania zilibeba shehena kubwa ya madawa ya kulevya aina ya bangi? Je, unakumbuka mkasa huo? Kutokana na kisa hiki, unafikiri 'image' ya Tanzania ipoje katika anga za kimataifa kuhusiana na masuala haya ya kiusalama????
 
Tuko pamoja Mkuu, nakumbuka Sana hiyo scandal ya Meli, nimeuliza hivyo ili kujua labda hao wachezaji ni special sana uwanjani kiasi kwamba imebidi wapewe uraia haraka haraka , maaana sijaona sababu ya msingi ya kuwapa hao wachezaji uraia
 
Haruhusiwi, halafu isipokuwa!! Sasa ndio inakuwa.
Narudia tena kusema kwamba Raia wa kigeni haruhusiwi kumiliki Ardhi nchini Tanzania isipokuwa kwa sababu za Uwekezaji tu chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 1997.

Chini ya Sheria ya Uwekezaji, Raia wa kigeni anaruhusiwa kutumia Ardhi kwa kigezo cha "derivative rights" only, and not otherwise.
Please Elewa point hii.
 
Nawakumbusha watanzania wenzangu wenye uwezo na msio na uwezo jitahidini mnunue maeneo...muwe hata na hati miliki ya vijiji zile barua na mihuri yao...baadae Ardhi itakua haishikiki...
 
Ajabu ni pale mtanzania mwenyewe halisi anapohitaji hizo huduma kuzipata ni kazi. Kupata tu kitambulisho cha Taifa kazi. Hivi wanasheria hawezi kufungua kesi mahakamani kupinga uraia wa hawa watu? Tanzania ndo imebaki nchi pekee ambapo wakenya wanaona ni rahisi kupata documents za kiserikali kuliko nchini kwao. Nenda Arusha huko, njoo Dar Wasomali na wahindi wanavyopewa pasport kama wananunua machungwa kariakoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…