Kile alichobaini na kukisema MH TWAHA JENERALI ULIMWENGU ni kitu kinachopaswa KILIHAMSHE TAIFA kama kauli ile itapita kimya basi tujue tumekwisha.
Maneno aliyoyasema Mwamba huyu katika UANDISHI wa habari ni maneno mazito yenye kuturudisha kwenye kumbukumbu nyingi za kujivunia UZALISHAJI wa vijana wengi WASOMI wenye maono makubwa kwa Taifa Lao
Je, hivi sasa tuko hivyo? TUNARIDHIKA na hali hiyo. Iko wapi ile MIDAHALO iliyokuwa ikiitishwa pale na kualika wahusika mbalimbali KUELIMISHA na kujibu HOJA.
NAKUMBUKA umaarufu mkubwa wa Marehemu MTIKILA naye alianzia pale baada ya kujenga hoja na kujibu maswali WANAFUNZI walimshangilia na kumbeba juu, juu wiki iliyofuata alikuwa pale JANGWANI wananchi wakajiuliza huyu ni nani, mpaka wanafunzi watata na wasomi wamekubali hoja zake kiasi cha kumbeba juu juu, akiwa JANGWANI aliwasha moto mkali neno GABACHOLI likazaliwa.
Marehemu DR JOHN POMBE MAGUFULI akiwa waziri katika serikali ya awamu ya 3, alipita pale chuoni na kukuta MDAHALO serikali ikiwa inashambuliwa na muendesha mdahalo akauliza kama kuna kiongozi wa serikali kwenye ule UKUMBI.
RIP MAGUFULI hakuwa mualikwa ukumbi ulikuwa umejaa, yy kasimama anachungulia kama wanafunzi wengine lkn DIRA ikamuulika na kumpeleka mbele ya UKUMBI na kujibu HOJA.
RIP MAGUFULI alijibu kila HOJA kwa ufasaha mkubwa mpaka wanafunzi walimshangilia mno, mwisho wakatamka wao waliamini WANASIASA ni waongowaongo lkn kumbe wana vitu vikubwa kwa maendeleo ya nchi.
Hiyo ni mifano midogo ya kutaka TUFUFUE chuo chetu, kiwe moto WATU TUNAO, CHUO KIPO, WANAFUNZI WAPO !!