Rais Samia nakuomba umuondoe Mzee Kikwete kwenye nafasi ya Chancellor wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Kwani JK ndiyo DVC Academic wa UDSM? JK bado yupo yupo sana, kama humtaki hamia Burundi
 
Kuna pahala Vyuo vyetu Vikuu vinafeli, TCU pia imeshindwa kuleta tija na hivyo inabidi ijitathmini uwepo wake. Watoto wa Vyuo wamekuwa Wahuni kupindukia, Ubora wa Elimu ni zero, product zao ni kichekesho mpaka unabaki kusema Heeeeeeeeee
Ndo maana wakirudi mtaani wanakaa kusubiri ajira na si kujitegemea.
 
udsm imekuwa kama shule ya kata.

Hakuna midahalo.

Hakuna ushauri

Hakuna kukosoa hata kushauri

Hata hiyo mikataba yao ilitakiwa ichambuliwe pale.
 
Tatizo la mfumo wa elimu ni kama duka la reja reja ukianza kulichezea hutajua kama ndio linapotea ila final unajikuta umebaki na bakara zikiwa tupu bila bidhaa
Mfumo wa elimu umechezewa mda mrefu sana Sasa matokeo yameanza kuonekana
 
Kikwete sio mtendaji wa UDSM yeye ni ceremonial tuuu.....Prof Anangisye ndio ana kazi sasa kujibu hoja hizo....
Pengine hajui hata kama kuna hiyo course hapo chuo 😀 😀 😀 wadili na hao maprofesa uchwaraaa waliopo chuoni kwao
 
Hoja ya Jenerali Ulimwengu ni kwa vyuo vikuu vyote na elimu ya juu na sio Udsm pekee.

Ikiwa uongozi wa Kikwete umeshusha ubora wa elimu chuo kikuu Cha Dar es salaam, hivyo vingine vimeimarika?

Kama vimeimarika basi mna haki ya kumsema J.K ila kama vimeanguka navyo, hizi lawama kwa mtu mmoja ni chuki binafsi au roho mabaya ya nyoka?

Je ubora wa mijadala, fikra tunduizi, akili bandia, suluhisho la mikwamo ya kiuchumi limeimarika kwenye vyuo vingine?

Chuo kikuu kama Udom, Mweka, Kampala University, Moshi Cooperative, Mwenge University, Stella Maris Mtwara, Teofilo Kisanji University, Mbeya science na Tekinolojia vimeimarika au ni kidato Cha kumi?

Taasisi za elimu ya juu kama IFM, TIA,AIAA, DMI, DIT,ISW, WI, NIT vimeboreka?

Kama bado ni tatizo la nchi nzima kuhusu kushuka kwa ubora wa elimu ya vyuo vikuu ? au uongozi mbovu wa Kikwete UDSM?
 
Sina uhakika na Mh Kikwete anavyo tumikia wadhifa wake wa Chancellor hapo UDSM. Nadhani yote yalio semwa ni kazi ya uongozi wa chuo sio level ya Chancellor.
Kuwa na mtu kama Mh Kikwete kuna faida sana UDSM kwa uzoefu, mtandao alionao na ushawishi alionao yote haya yanaweza kuifadi sana UDSM.
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Kwa kweli Jakaya Kikwete kafeli pakubwa panahitaji kufumuliwa pale UDSM chuo changu kabisa nimepita pale na nna degree yao moja walinipa
Walilupa pole sana hukustahili ulipewa tu. Hawa ndio wale wale wasioweza kujibeba anakuambia digirii alipewa😂😂😂
 
Vipi hali ya vyuo vingine? Kama viko vizuri basi viongozi watatoka huko. Kama navyo ni vibovu, basi unakoelekeza tatizo siko.
 
Alale salama huyu mwamba. Moja ya watu wa kulaumiwa sana kwa kuifikisha yudii na vyuo vingine vya umma hapa vilipo ni huyu mwamba. Kwa sababu hakupenda kukosolewa, wakati wake wataaluma ni either aliwapa rushwa ya uteuzi ama aliwashughulikia kwa kutumia Dola wote waliotoa mawazo tofauti na yeye.
 
Kumuondoa italigharimu taifa pesa nyingi sana kuliko akiachwa, gharama zitatokana na kuweka matangazo nchi zote duniani ili aweze kujua kuwa ameondolewa, lile tangazo la popote alipo litamvunjia heshima, najua unadhani yuko Msoga kumbe huenda yuko ueskimoni akiangalia mazingira.
 
Kumuondoa italigharimu taifa pesa nyingi sana kuliko akiachwa, gharama zitatokana na kuweka matangazo nchi zote duniani ili aweze kujua kuwa ameondolewa, lile tangazo la popote alipo litamvunjia heshima, najua unadhani yuko Msoga kumbe huenda yuko ueskimoni akiangalia mazingira.
 
Chuo kimekuwa cha kihuni tu hivi sasa
 
Chuo kimekuwa cha kihuni tu hivi sasa
 
Huu uzi kila mtu ni product ya UDSM
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Subirini mletewe wakina zuchu na wakata mauno wengine mjirushe nao

Ova
 
wasomi wetu wa siku hizi haswa UD wengi wao ni mbumbuu ndio maana wanafeli sana mitihani, wengi wao wanatafuta digirii za kuchapa uhuni...........na ukahaba. Hakuna wasomi pale ovyo kabisa
WanafunI huko sahvi muda wote wanajadili habari za udaku...

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…