Mi nadhani haya mambo tunachanganya madesa au tunajisumbua bure!!
Mama Samia sio kwamba anabadili sheria bali anahamasisha FDI! Hata hao USA, EU na Uchina bado wanazitafuta FDI! Kuna wakati Canada ukionesha financial ability, na unafanya biashara, fasta wanakupa Resident Permit ili mradi tu kuvutia FDI!
Na watu wanapohamasisha Foreign Direct Investments haimaanishi Watanzania wanatupwa nje ya ulingo wa uwekezaji! Na wenyewe wapo, na ndio maana Samia anataka pia kukutana na local business community!
Sasa kama Mtanzania anataka kumiliki na kuliendesha kibiashara shamba kubwa hakuna atakayemzuia ili mradi tu asifanye mtindo wa akina Mo Dewji wanaomiliki maelfu ya ekari lakini badala ya kuzitumia kwa shughuli kusudiwa, anatumia kwenda kuombea mikopo NJE!
Na hata huko kwenye umiliki wa viwanda, as of now, Samia atatumia sheria zile zile alizokuta! Kama sheria zinasema 51% inabidi imilikiwe na m-TZ basi ndo itakuwa hivyo hadi pale tutakaposikia sheria zimebadilishwa!
Hata hivyo, huwezi kuweka fixed 51% kwa sababu, tuchukulie tu kile kiwanda cha kusindika gas kule Lindi! By 2015, kilitarajiwa kingegharibu USD 30 Billion!
Tajiri namba 1 wa Tanzania HANA hata 10% ya hiyo USD 30 Billion, na ndo maana sehemu kama hiyo ni serikali ndiyo inatakiwa kuingia!