Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

Rais Samia: Nakwenda kufungua Nchi, mmekuwa mkinitukana sana mitandaoni

Acha wasiwasi mkuu...tumpe mama ushirikiano wa kutosha atatufikisha mbali..Mama tangu ameanza kuongoza nchi yetu ameonesha uwezo mkubwa kuwaongoza serikali na ninaamini atatupeleka kule wengi tunatamani..kufika..kila la kheri mama Sasa..tupo nyuma yako tunakuunga mkono kwa dhati..tukifanya kazi kwa bidii na uaminifu mkubwa..Mungu ibariki Tanzania
 
... wazee wa legacy fake Mkuu! Hawaamini mambo muhimu Mama aliyoyafanya ndani ya muda mfupi tangu akalie kiti. At least furaha imerejea nchini kwao ni uchungu kweli kweli wazee wa visasi!
Hata waliozoe kupigapiga watu wakafuge mbwa na paka waendelee na hilo zoezi. Hakuna mtu wa kupigwa sasa.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema anakwenda kufungua Nchi akisema, "Mmekuwa mkinitukana sana kwenye mitandao! Unakwenda kubomoa yaliyojengwa kwa muda mrefu".

Akizungumza na Wafanyabiashara wa Tanzania Nchini Kenya Mei 05, 2021 Rais amesema anaamini hakuna Nchi inayoendelea ikiwa peke yake.

Ameeleza, anajiandaa kufanya mkutano na Sekta Binafsi kuzungumzia kero mbalimbali zikiwemo za Kodi, Vibali vya Kazi (Work Permits), kuchelewa kupata ardhi kwenye Uwekezaji ili kuona namna ya kuziondoa.

Rais amesema maeneo ya kujenga Uchumi yapo lakini mchakato umekuwa ukienda polepole, akitolea mfano eneo la "Industrial Parks" alilosema haoni sababu kwanini zinazuiwa.

Msikilize hapa:



Ameshindwa kuifungua twitter mapaka uwe na VPN ataweza kuifungua Nchi kweli???
 
Kama hatukuwahi kuinuka, basi tutakwenda chini zaidi.

Maana anayoyafanya leo, JK aliyafanya miaka 10 na nchi ikawa ya hovyo kabisa.
Mataga utapata tabu sana awamu hii! Ukiona mambo ni magumu, ni bora ukachukua tu maamuzi magumu ya kunywa sumu au kujinyonga, ili umfuate mungu wako huko kuzimu.

Muachie Rais atekele majukumu yake kwa mujibu wa katiba. Yule mungu wako alikuwa ni kiumbe hopeless na useless kabisa kuwahi kutokea nchini!
 
Kama hatukuwahi kuinuka, basi tutakwenda chini zaidi.

Maana anayoyafanya leo, JK aliyafanya miaka 10 na nchi ikawa ya hovyo kabisa.
Mama afanye anayoona yeye ni sahihi ili mradi tufike jk alifanya mazuri Tena mengi na upande mwingine alifanya ovyoo hata mwendazake Kuna mamabo alifanya vzur Kuna mambo alifanya hovyo haijwai tokea
 
Huyu atatupeleka sehemu ambayo hatutakaa tuinuke tena.
Yaan kwenda Kenya kufungua fursa za kibiashara ndio "anatupeleka sehemeu ambayo hatutakaa tuinuke tena" mawazo mgando kabisa haya. Mtu wa hivi hata nyumbani kwake na mkewe bila shaka hawana maelewano, maana haelewi chochote. Bado akili mgando za "mwendazake" zimemuathiri.
 
Nchi iko free kuwekeza mnaopiga kelele nan kasema wazawa hawaruhusiw kuwekeza wageni wakija
Pepo la mzeee linawatafuta vibaya watu
Tatizo ninaloliona kwa Watanzania ni umasikini wa akili na maisha, imagine mtu hatokei tu kama mimea anatoka kwenye ukoo wa mababu zake na hao mababu ndo walitakiwa kumiliki Ardhi na maeneo makubwa na watoto wangepewa wakaendeleza na kurithisha wajukuu Ili kutunza falme zao na koo zao sasa kinachotokea mababu walikuwa na maeneo madogo kwaajili ya wao tu na wengine walipanga tu vijumba bila kutengeneza koo zao na kuziwekea urithi wa Ardhi sasa watoto au wajukuu ndo wanahangaika kwenda kununua Ardhi sehemu zingine wajenge ndo maana tunapata kelele za wivu wa Ardhi kwamba itakwisha, kinachotakiwa kufanywa ni kutungwa Sheria za kusimamia vizazi na mali za familia Ili zitumike kwenye familia husika na wale ambao hawakuweka urithi wa familia zao kwa kupenda au kutopenda basi wawajibike kuishi hivyo hivyo Kama watu pori, Jukumu la kuwa na Ardhi liwe la lazima kila familia na mtu awe na watoto kulingana na Ardhi yake na kila mtoto amuwekee Ardhi yake ambayo watarithi wajukuu hiyo hiyo hapo kelele za Ardhi zitapungua na kuzaliana ovyo kutapungua.
 
Ni kwamba akiifungua nchi na mwekezaji akamilikishwa ardhi na kutokana na economic strength yake , itakuwa shida sana kuipata ardhi hiyo au kwa gharama mara mia ya bei aliyonunulia. Angalia matatizo ya ardhi yalio pelekea mapigano ya kikabila, ambapo Uhuru aliahidi kutoa kiasi lakini sijasikia kutekeleza ahadi hiyo
Mama amesema waliohodhi ardhi kubwa bila kuiendelezaa watachukua. Hii ni vizuri
 
She is hopeless and one term president!Badala ya kujishughulisha na kufuta zile sheria kandamizi za uwekezaji za mambo ya task force na kadhalika ambazo alizitunga yeye pamoja na Magufuli anaongea vitu ambavyo ni non-sense.

Hakuna mwekezaji ambae atarudi kuwekeza Tanzania kwa sheria zile!Nchi ilifungwa kwa sheria kandamizi za uwekezaji kwa hiyo inapaswa kufunguliwa kwa kufutwa sheria hizo kandamizi.
Amesema sheria tumetunga wenyewe kwa nini tushindwe kuziondoa
 
Task force ziondolewe
A task force is a group of people who come together from diverse branches, positions, and points of view to facilitate the development of ideas, create new opportunities, answer questions, or solve a problem.



A task force is a unit or formation established to work on a single defined task or activity. Originally introduced by the United States Navy, the term has now caught on for general usage and is a standard part of NATO terminology.
 
Mama amesema waliohodhi ardhi kubwa bila kuiendelezaa watachukua. Hii ni vizuri
Sheria ya Ardhi inasemaje? Na baada ya hapo inafanyiwa nini?? Na sababu za kuchukua hatua hizo ni nini ?
 
She is hopeless and one term president!Badala ya kujishughulisha na kufuta zile sheria kandamizi za uwekezaji za mambo ya task force na kadhalika ambazo alizitunga yeye pamoja na Magufuli anaongea vitu ambavyo ni non-sense.

Hakuna mwekezaji ambae atarudi kuwekeza Tanzania kwa sheria zile!Nchi ilifungwa kwa sheria kandamizi za uwekezaji kwa hiyo inapaswa kufunguliwa kwa kufutwa sheria hizo kandamizi.
Umesikiliza hotuba yake kweli au huna bando?
 
Mie nimependa hapo mwisho,
Akanyooshe na bungeni.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema anakwenda kufungua Nchi akisema, "Mmekuwa mkinitukana sana kwenye mitandao! Unakwenda kubomoa yaliyojengwa kwa muda mrefu".

Akizungumza na Wafanyabiashara wa Tanzania Nchini Kenya Mei 05, 2021 Rais amesema anaamini hakuna Nchi inayoendelea ikiwa peke yake.

Ameeleza, anajiandaa kufanya mkutano na Sekta Binafsi kuzungumzia kero mbalimbali zikiwemo za Kodi, Vibali vya Kazi (Work Permits), kuchelewa kupata ardhi kwenye Uwekezaji ili kuona namna ya kuziondoa.

Rais amesema maeneo ya kujenga Uchumi yapo lakini mchakato umekuwa ukienda polepole, akitolea mfano eneo la "Industrial Parks" alilosema haoni sababu kwanini zinazuiwa.

Msikilize hapa:
"Mwenda bure si sawa na mkaa bure". Mwendazake alikuwa mkaa bure ndiyo maana alikuwa busy kusikiliza simu na kusoma SMS za watu wengine na kupekua taarifa za account za benki za watu. Wacha mama aende bure ni zamu yake sasa hao wasiopenda waache kudemka. Namuunga mkono Rais wetu atuletee Suluhu ya vikwazo vya biashara nchini - nchi unayotakiwa kuanza kulipa kodi, hata kabla hujafungua biashara, ili upate leseni ya kufungua biashara.
 
Hivi vitu vinatakiwa kwenda pamoja ndio maana kuna Maneno kama urari wa biashara kati ya A na B ni fulani. Nafikiri kwa haya maneno Machache utakuwa umeelewa.
Nakubali lakini urari waweza kuwa unafaidisha mtu mmoja tu na ukauona uko vizuri wakati majority wa chini hawambulii kitu

MfanoTuchukulie Tanzania iliuza Kenya bidhaa za milioni 80 na Kenya ikauza bidhaa kwa Tanzania za milioni 80 pia ukitzama hapo urari unauona umekaa vizuri sana

Unatakiwa kwenda deep unaajiuliza nani walipeleka bidhaa zote hizo Kenya? Unakuta ni kampuni moja tu mfano ya AZAM ya BAKHERESA halafu unaenda Kenya kufanya analyisis je wao nani aliuzia bidhaa Tanzania unakuta kuna makampuni ya watu tofauti elfu moja!!! Urari ume balance lakini kuna maneno.Tanzania ni mmoja tu kule maelfu

Ndio maana urari usiishie tu kwenye vitabu je wafaidika ni wangapi wa hizo biashara kati ya mataifa mawili? Wa level ipi wa juu peke yao au hadi wa chini?

Kwa upande wa Kenya wafaidiika ni makundi yote toka juu hadi chini.Tanzania tofauti kutokana na hivyo vikwazo vya kuanzia upataji passport Kubwa za muda mrefu ,permit na viza

Kenyatta alichofanya anataka asaidie hawa wa chini ambao kikweli wako wengi sana wanavuka na bidhaa zo chache kwenye mabasi nk na kufanya kazi za kawaida kenya na wao wafaidi lakini pia watanzania ni cheap labour kuliko wakenya hivyo wakenya wengi huwahitaji kwa kazi za majumbani ,magereji ,udereva nk

Uraia usiishie tu kuangalia namba tu za kwenye makaratasi kuna makundi tena makubwa yaweza yasiwemo kwenye huo urari.KUU BALANCE LAZIMA U TAKE ON BOARD WOTE JUU HADI CHINI NA NDIO MAANA YA EAST AFRICAN COMMUNITY SIO EAST AFRICAN COMPANIES!!!!
 
Watu wamenuna hao... yaani hawataki tushirikiane na Kenya kwa sababu tu JPM hakutaka ushirikiano mwema nao!!
Mbongo mwenye hela na connection ndani ya KE anatabasamu sahi, hao wengine wacha wabishane tu, haitawasaidia in the long run.
 
Mama Samia asipoleta timu mpya ya serikali na ndani ya chama chake atafelishwa na lile genge la uzaledo feki.

Tujiulize kwa ni watu ni wale wale lakini wanaonekana kama wanamkejeli kuliko hata wapinzani?

Hivi kweli kazi za wakuu wa vitingo, wakuu wa mikoa ,wakuu wa wilaya hawana jambo la kufanya zaidi ya ujinga waliokua wanaufanya wa kutisha na kuweka watu ndani kwa kuuliza maswali ?

Nchi yenye ardhi na rasilimali nyingi kama Tanzania imebaki kuwa na watu wa kushabikia umaskini wa watu badala ya kujenga taasisi imara za uzalishaji?

Tuna JKT na JKU hawa kazi yao sio ulinzi bali ni kujenga nchi.

Hivi inaingia akilini kweli vijana waanzishe shamba ekari 20,000/- za Korosho,mkonge, Mahindi ,Alzeti, mabwawa ya samaki,ranchi zaifugo halafu baada ya miaka mitatu wanarudishwa nyumbani kama vile walikua gerezani badala ya kuwaajiri na kuwalipa kama vibarua kwenye mashamba hayo ya umma ambayo yanaweza kuzalisha na kuuza nje ya nchi kwa urahisi sana.?
Tatizo ni kuweka wakuu wa vitengo kindugu bila kujali visheni zao na maono yao kwa Taifa.

Wakuu wa mikoa na wilaya wana maeneo wanayoweza kuyatumia kwa ajili ya kuweka masoko na uzalishaji mkubwa na kuwajenga vijana kwenye ajira.

Tukianza kurudi kwenye zama za kuteuana kikabila bila kujali uwezo na uzoefu na maono basi tutawaogopa wakenya.

Wakenya wanawaogopa wahaya ,Wachaga Wakurya na Wajaluo, hawa tuwape nafasi kwenye Miradi ya ushindani na nchi ya kenya na ubabe wa kibiashara na sio kuwakimbia waKenya . Wale ni watu kama watu wengine.
Tulianza kuwakazia Wakenya badala ya kushindana tukawabagua . Baada ya kuwashinda tukahamia kwa wachaga na kuwaita wezi huku tukijua wazi kuwa ni kabila lililoweza kushindana na kupenya kila mahali penye Fursa kama Wahindi,Tulipaswa tuwatumie na kuwahamasisha kuwa wasijipendelee bali walipendelee Taifa kwa kutumia uwezo wao.
Wahaya pia tungeweza kuwatumia watu kama akina Rugemalila badala ya kuwafunga.
Angeambiwa aanzishe kiwanda kikubwa badala ya kujaribu kumfilisi.

Watu wabaya kabisa ni wale waliojipanga kuitafuna nchi kupitia madaraka.
Unakuta mkuu wa mkoa ana msafara kama Waziri mkuu. Hawa ndio wajujumu uchumi halisi mana wanafuja kodi za wananchi. Bahati mbaya walipewa mamlaka makubwa ya kufanya wanayotaka na kumdhalilisha wasiyemtaka.
 
... wazee wa legacy fake Mkuu! Hawaamini mambo muhimu Mama aliyoyafanya ndani ya muda mfupi tangu akalie kiti. At least furaha imerejea nchini kwao ni uchungu kweli kweli wazee wa visasi!
Yaani mama kabla ya siku 100 tayari keshanitua mzigo wa Deni la zaidi ya milioni 6 ambalo mwendazake alililpachika kwenye mkopo wa bodi
 
Back
Top Bottom