Kufungua nchi ni jambo zuri sana eeh, kama halitafanywa kiholela. Tafadhali rejea tajriba za nyuma: Mwinyi, Mkapa, JK wote walifungua nchi, matokeo yakawa si maendeleo bali wizi wa kutisha na almost kuuzwa nchi. Gorbachev pia alifungua nchi akaleta Galsnost matokeo yakawa kuvunjika kabisa kwa Soviet, na wizi wa kutisha. Lau si kudirikiwa na viongozi Wazalendo Urusi leo isingekuwa dola kubwa tena.
Ni vigumu kufungulia nchi maskini yenye raia maskini wa kutupwa, bila ya kukaribisha ufisadi, upotevu wa mali asili, mikataba mibovu nk. Haya tumeyapitia. Wanasema kosa si kukosa bali kurudia kosa.
Kwa uchache mambo haya yanabidi kufanyika kabla ya 'kufungua' 1- Mishahara ya kuweza kuishi ya civil servants, hasa wana usalama, polisi etc.
2- Mikataba mikubwa iwekwe wazi kwa taifa na ijadiliwe bungeni bila ya kuwekwa pressure.
3- Wawekezaji wazawa ndiyo wapewe kipa umbele, wapendelewe, wasaidiwe kifedha .........wataweza.
4- Kuwe na sheria ngumu sana dhidi ya rushwa, TISS ishirikiane na TAKUKURU badala ya kukimbizana na wapinzani.
Sharti ya kwanza ni muhimu sana. Ukifuatia kufeli kwa 'ufunguzi' wa nchi kulikofanywa na predecessors, utakuta mishahara isiyokidhi maisha ndiyo sababu kuu, kiasi watuishi wa serikali wakawa hawaheshimu kazi wala majukumu waliyopewa.